Chuki ya Afande Sele Kwa Joh Makini na Nikki wa Pili ni Chuki Kali Mbaya Mno

Chuki ya Afande Sele Kwa Joh Makini na Nikki wa Pili ni Chuki Kali Mbaya Mno

😁Sasa nimefahamu kwanini ulikataa mkatoliki apewe maua yake. Joh namkubali tokea enzi hizo anakuja uwanja wa Ilboru secondary akiwa star af haringi wala mnini, Nikki nakubali historia yake hustling za kitaa kupambana na kitabu.

Wasanii wote wanao pambana na hawa gurus ni wivu wa maendeleo yao kwenye music industry na kimaisha. Hakuna kingine, ukiona mtu anakuchukia kiasi cha kutangazia umma ujue umemzidi kila kitu alafu unaachana nae.

Kuhusu Fid alitengenezewa zengwe tu ili aonekane ana chuki na Joh. Ila Ngosha ni mtu poa hana negative personal feelings. So yeye pamoja na joh walilitambua hilo wakafanya chuki iliyopandikizwa kuwa biashara, kwa bahati nzuri Joh akajipanga zaidi kutengeneza network kwenye media zika mbrand kama mfalme wa hiyo industry. Hapo ndipo wakajitokeza wachawi live wale waliosuka chuki, ikawa nongwa sana.

Baadae tunakuja kuwaona hadi Redindian na kagenge kake anataka kujulikuna(cheap popularity) kupitia kumtukana Joh, ila ukweli Joh ndiye aliyefanikiwa kufanya hiphop ya Arusha kuwa biashara, kipindi hicho nako walijaribu uhuni ukawa mwingi, cha ajabu leo Fido na kagenge kake wanataka kuiharibu hiphop na kuirudisha kuwa uhuni, no wonder ata N2N wenyewe wanamkazia, wanajua uwezo wake mdogo sana.
 
images (20).jpeg
 
Back
Top Bottom