Chuki ya Afande Sele Kwa Joh Makini na Nikki wa Pili ni Chuki Kali Mbaya Mno

Chuki ya Afande Sele Kwa Joh Makini na Nikki wa Pili ni Chuki Kali Mbaya Mno

images (15).jpeg
 
Baba T, Simba zee, kwakusema sio muoga, sijui bangi zinampa ujasiri, sungu walipishana kidogo, alimchana wakati ndio aliemtoa bila kuogopa Wala Nini, kipindi kile alivyopata ufalme wasanii wenge walichukia live maneno yaliwatoka Sana tu, hasa ukizingatia huyo DC kupewa tuzo, mwenye nacho anaongezewa, wangempa hata Roma, stamina nk.
 
Nimepita kwenye mtandao flani hivi nikaona kuna mtu kaweka interview ya Afande Sele akiwatukana na kuwaponda joh makini na Nikki wa Pili.
Ina muda kidogo Ila leo nilipoiona basi nikasema ngoja niseme jambo huenda wengine mtaona hii chuki kubwa iliyopo. Hawa ni wa kimya na wapole sana, hivyo mashabiki zao tutawasemea iwe usiku au iwe mchana.

Afande amefikia hatua anasema tuzo za KTMA zilikufa sababu ya joh makini kupewa tuzo(video chini). Afande anasema hawa watu wanabebwa sana, hivi kweli mtu atabebwa kama hana uwezo? Joh Makini katoka Arusha kuja dar akiwa hana ndugu wala rafiki, kaishi gheto magomeni akiwa hajui atakula nini, katembea kwa mguu kutoka magomeni hadi masaki kutafuta appointment na master j.

Mtu kama huyu ambae hakua na connection yoyote anawezaje kubebwa? zaidi ya uwezo wake alionao? Anasema kasikia Nikki kapewa ukuu wa wilaya basi abaki hukohuko asiguse muziki wao, yaani Afande kajipa umiliki wa muziki Tanzania.

Ukiacha hii chuki Kali kabisa ambayo Afande anayo kwa hawa vijana, pia Kuna wasanii wengine ambao walipambana sana kuwatukana na kuwasema vibaya Joh makini na Nikki wa Pili

Roma
Huyu ndio alikua wa kwanza kuanza kupambana na hawa watu, baadae sijui aligundua nini au sijui alichoka maana akaachana nao. Nikki na Joh hawakuwa kumjibu popote waliamua kumpotezea

Fid Q
Huyu alikwepa mtego wa chuki hadharani na kwenye media, huyu alikua na chuki pembeni tu. Alikua akiamini alizimwa ili joh makini achukue nafasi(kitu ambacho sio kweli). japo baadae aliamua kuachana na chuki na maisha yakaendelea

Nikki Mbishi
Mpira ukatoka kwa roma ukahamia kwa Nikki Mbishi a.k.a underground wa milele. Huyu alitokwa povu kweli kwa mambo binafsi hadi akawa anampost joh makini akiwa na demu gheto amelala. Kila akihojiwa ilikua ni joh makini na Nikki wa Pili tu, hakua na kilio kingine zaidi ya hao. Kuna siku akihojiwa na EATV alitoa kilio kikali kwa nini kila kitu ni Nikki wa Pili tu

Dully Sykes
Huyu alifikia hatua anapigia simu wasanii wezake na kuwafokea kwa nini wanamshirikisha joh makini kwenye nyimbo. Alihifadhi chuki Ila baadae akaiweka wazi. Bahati mbaya akampigia TID kumuuliza kwa nini anashirikiana na joh makini, uzuri TID sio mswahili basi akapambana nae

Chiddi Benz
Ni kama wanapokeza, maana mpira ukahamia kwa chidi benz, huyu alionyesha chuki kali mno aliyonayo ya miaka mingi sana kwa hawa jamaa wawili joh na Nikki wa Pili. Chidi alikua anaongea hadi anakaza shingo kwa nini kina joh na Nikki wa Pili wanaonekana sana. Sijui kosa la hawa mabrother wa Arusha ni nini. Kila interview ilikua ni kulalamika tu kwamba kwa nini kila kitu ni joh na Nikki wa Pili, anahoji wao kina nani bwan. Hadi interview ya karibuni hapa bado analia tu kuhusu joh na Nikki wa pili

Mr.Blue
Huyu sijui alikumbwa na nini akaanza nae kuwaponda watu ambao hawana uhusiano wowote na yeye. Nikki wa Pili kwa busara tu aliwahi kumpigia blue na kumuuliza kwani shida nini, blue akawa mpole.

Nyandu Tozy
Huyu nae sijui sababu nini alianza from nowhere kuwatukana hawa jamaa bila sababu zozote. Alipowahi kuuliza akakosa jibu

Young Killer
Huyu bwana mdogo nae akaingia kwenye huu mkumbo, sijui huwa wana kundi kabisa wametengeneza kupambana na joh na nikki? Maana sio kawaida. Huyu dogo nae akaanza kuwaponda na kuwasema vibaya joh na nikki wa Pili. Naona sasa hivi kachoka

Fido Vato
Huyu ni muhindi flani hivi yupo Arusha ambae karukia muziki hajui kuandika hata verse 1. Nae kila akipata nafasi ya interview basi ataishia kuwaponda joh makini

Mh. Temba
Huyu nae bila sababu akaamua nae kufuata mkumbo. Ni Kama chuki ilikua kifuani inatafuta namna ya kutoka. Alipoppata nafasi ya kuitoz chuki basi akaiachia.

Afande Sele
Huyu ndio baba wa chuki kwa hawa watu, yeye anawachukia kuanzia muziki hadi maisha yao binafsi.

List ni ndefu ambayo imejaza watu wenye wivu na chuki kwa vijana wenzao, alafu wala hawana time ya kulalamika wala kumjibu mtu
Nikki wa Pili wakati anaingia studio na kushiriki wimbo wake wa kwanza kabisa wa Niaje Nivipi alioshirikishwa na Joh Makini Kuna mstari aliimba".....nivipi bro, natabiri hawatonipenda hakuna aijuaye kesho hata mtunzi wa kalenda....." Ni kama alikua mbele ya muda

Guys ukiona unafanya Jambo alafu hakuna wanaochukia basi jua unakosea

Chini nimeweka interviews za afande sele, chidi benz, Nikki Mbishi. Muone jinsi wanavyoumiza na hawa vijana wawili joh makini na Nikki wa Pili. Kabisa wanalalamika kwa nini Nikki wa Pili ni msomi[emoji23], sasa sijui kuwa msomi ni dhambi.








View attachment 2606791View attachment 2606792View attachment 2606793
Sawa Bro Joh Makini Na Dogo uliyechapiwa mke, Nikki wa Pili. Vp dogo umepata jiko lingine? Vipi utathubutu kujitamba tena mitandaoni kuwa mkeo mzuri kuliko wote? Mpost tena na huyo tumtomb£
 
Baba T, Simba zee, kwakusema sio muoga, sijui bangi zinampa ujasiri, sungu walipishana kidogo, alimchana wakati ndio aliemtoa bila kuogopa Wala Nini, kipindi kile alivyopata ufalme wasanii wenge walichukia live maneno yaliwatoka Sana tu, hasa ukizingatia huyo DC kupewa tuzo, mwenye nacho anaongezewa, wangempa hata Roma, stamina nk.
Secretary hujambo 😁😁😁😁😁😁😁
 
[emoji16]Sasa nimefahamu kwanini ulikataa mkatoliki apewe maua yake. Joh namkubali tokea enzi hizo anakuja uwanja wa Ilboru secondary akiwa star af haringi wala mnini, Nikki nakubali historia yake hustleling za kitaa kupambana na kitabu.

Wasanii wote wanao pambana na hawa gurus ni wivu wa maendeleo yao kwenye music industry na kimaisha. Hakuna kingine, ukiona mtu anakuchukia kiasi cha kutangazia umma ujue umemzidi kila kitu alafu unaachana nae.

Kuhusu Fid alitengenezewa zengwe tu ili aonekane ana chuki na Joh. Ila Ngosha ni mtu poa hana negative personal feelings. So yeye pamoja na joh walilitambua hilo wakafanya chuki iliyo pandikizwa kuwa biashara, kwa bahati nzuri Joh akajipanga zaidi kutengeneza network kwenye media zika mbrand kama mfalme wa hiyo industry. Hapi ndipo wakajitokeza wachawi live wale waliosuka chuki, ikawa nongwa sana.

Baadae tunakuja kuwaona hadi Redindian na kagenge kake anataka kujulikuna kupitia kumtukana Joh, ila ukweli Joh ndiye aliyefanikiwa kufanya hiphop ya Arusha kuwa biashara, kipindi hicho nako walijaribu uhuni ukawa mwingi, cha ajabu leo Fido na genge lake wanataka kuiharibu hiphop na kuirudisha kuwa uhuni, no wonder ata N2N wenyewe wanamkazia, wanajua uwezo wake mdogo sana.
Tupo pamoja bro. Joh kapambana sana na huu muziki alafu kuna wajinga wachache wanamchukia bila sababu

Huyu muhindi redindian ni mshamba sana, wewe ni wa chuga na Kama unakumbuka vizuri huyu muhindi ndio chanzo cha Lord eyez kupigwa kisu kipindi kile.
 
kama kweli hawa wote wamewahi kuwa na bifu na joh makini (narudi tena kama ni kweli ) joh makini ana matatizo

yaani kundi lote hili likuchukie wewe hapana
Ukifanikiwa lazima uchukiwe, ukiona unafanya jambo alafu hakuna wanaokuchukia basi jua unafeli.

Hata diamond ndio msanii anayechukiwa sababu ya mafanikio yake
 
Ukifanikiwa lazima uchukiwe, ukiona unafanya jambo alafu hakuna wanaokuchukia basi jua unafeli.

Hata diamond ndio msanii anayechukiwa sababu ya mafanikio yake
joh makini ana mafaniko gani ya ajabu kushinda hao wengine
diamond na kufanikiwa kwake ajachukiwa kama jamaa yako

kubali kataa, jamaa ana shida flani
 
Back
Top Bottom