Ndugu tatizo la sisi wabongo ni wanafiki sana, tunayajua sana haya lakini ili tuonekane watakatifu kwa watu basi tunajifanya innocents behind the keyboards, most of people hapa hasa wanaoside upande wa mama Dai they sound so hypocrisy! Watu wanapenda sana kujifanya akina mother teresa humu ikiwa in reality they are not.
mambo ya familia za watu msipende sana kuyatungia sentensi ndefu ndefu ni bora tu kutumia maneno mafupi mafupi kama la hasha! Looh! Kumbe! Mhhhh! n.k (if you know what I mean) [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Jamani hasa kwenye familia zetu hizi za kiafrika kuna tatizo kubwa sana Kati ya mtu na wakweze/ mawifi. Na mara nyingi hakuna sababu ya msingi ya hayo matatizo kutokea, na ikiwa watu wataelewana na kila mtu ajue nafasi yake kwa mhusika basi hakuna ugomvi wowote utakaotokea, lakini pia ugomvi ni kitu cha kawaida kabisa kutokea hivyo ni vyema sana kuchukuliana (kubebana), ila kwakuwa binadamu tuna tabia nzito basi tutaendelea kugombana until forever ends.
Back to my testimony, mi nina wifi yangu ( mke wa kaka) ambae naweza sema ni the best wifi kupata kutokea mtoto wa watu kwanza kazuri, kapole, kanajituma, hakana dharau inshort sionagi shida yake kubwa, pungufu lake pekee nilijualo ni mzembe fulani hivi sometimes, of which ukijaribu kuiasses tabia yake utagundua ana mazuri mengi kuliko mabaya, lakini the prob is haelewani kabisa na mamangu (mkwe wake) mara kwa mara namuona mama anamtupia tupia vijineno bila sababu ya msingi tu, Ndo nikagundua kuwa mtu anaweza kukuchukia tu bila sababu. Muda mwingine namwambia mama mbona unamsema huyu dada bila sababu za msingi? hana lakujibu,
kipindi sijaolewa wifi angu alikuwa ananiambia "wifi unaishi vizuri sana na mimi nakuombea ukiolewa ukakutane na mawifi na wakwe wenye roho kama yako, lakini dah salaleeee bahati hiyo sina pia yaani mama mkwe wangu ni mkorooofiiii hapana mfano hata umbebeje utamtua tu kuna siku.
Yaani huyu mama hajawahi kunipenda since day one ananiona, nikaona isiwe tabu kila mtu aishi maisha yake, mambo yalivyo mengi muda wakumuimpress mtu nautoa wapi, mi kwa kweli kuishi maisha ya uongo kumfurahisha mtu naweza lakini huwa sitaki na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Mimi pia mi si kamilifu, nina matatizo yangu nami mengi tu. Lakini huwa najua kuwa mama mkwe ni mamamkwe tu kamwe hataweza kulala na mwanae so huwa sina haja yakugombana nane kabisa, lakini anavyoufource ugomvi na anapenda vishindo kiasi kwamba nishagaona ni bora tuishi mbali mbali tu ili mambo yaende, tunashirikiana kwenye mambo ya lazima tu kama misiba, n.k sitaki hata mazoea.
Kwenye hili wanaume lazima mjue pakusimama ili
Kufanya mambo yaende, leo hii unajifanya unamsikiliza sana mamaako hukujua umeoa kwa ajili gani au umsikilize sana mkeo hujui kuwa una mama? Kila mtu asikilizwe kwa wakati wake kwa nafasi yake.
Back to mama Dai, hahha jamani nini tatizo? kama imemuua zari kununuliwa nyumba kwanini asielewe kuwa hiyo nyumba wajukuu zake tiffah na kijacho wataishi na wao? Diamond akinunua nyumba kwa ajili ya zari si inakuwa kwaajili ya wanae pia (familia) huko sio kuhonga its all about being a responsible father, ambalo ni jambo zuri, kama wanafikiri zari anamchuna Dai wao wanamtaka nani ambaye hata mchuna Dai? Yaani mwanamke gani wa diamond ambae hataspend hela za diamond?
Btw Zari sio mkaaji kwanini wasivumiliane tu kwa hiki kipindi kifupi anachokuwepo? Katika hili ntaendelea kuamini Mama Dai na Esma wake ndio wenye matatizo. Tatizo lao wanahisi zari anawarusha sana roho, yaani jamani mtu asifanye kitu wanarushwa roho, bongo shida sana. Leo nimeongea kama mke siku nikiwa mkwe pengine ntaongea mengine, ngoja niweke akiba ya maneno kwani hata mi nimezaa.