Chukua muda wa kuzipumzisha hisia

Chukua muda wa kuzipumzisha hisia

Tunaruhusiwa kuvumilia na kuvumiliana ktk MAHUSIANO, lakini ili tuvumiliane, kuna masharti lazima yazingatiwe! 1. UVUMILIVU huo lazima utambuliwe, uheshimiwe na pia upewe mrejesho chanya! 2. UVUMILIVU wako kwa mwenza wako ni lazima uwe na dalili za kukulipa hapo mbeleni! 3. UVUMILIVU wako usikuumize ama kuwa sababu ya madhara kwako ikiwemo majeraha ya kimwili au iwe sababu ya kuharibika kwa maisha yako ya baadae, coz maisha ulikuwa nayo kabla yake na yataendelea baada yake!
5. VUMILIA huku ukijua hatakiwi kuvuka mstari! Elewa kwamba kuna mstari kati yako na uvumilivu, mstari huu usivukwe!
 
Mapenzi yanauma ila kumwacha aende ndo suluhisho ya yote!!!

We mwache aende, kuna furaha zaidi mbele yako kuliko yeye!! Siku zote amini hakuwa wako na wakati ukifika ukifika utampata wa kufanana nae....

Just let her/him go!!!!!!
Shida inakuja moyo unapokuwa radhi lakini mwili ukawa dhaifu ukakosa ujasiri wa kumwacha aende very very painful n difficult decision to make
 
Shida inakuja moyo unapokuwa radhi lakini mwili ukawa dhaifu.. Ukakosa ujasiri wa kumwacha aende.. Very very painful n difficult decision to make
Moyo ukikubali mwili utazoea tuu kuna mahali uvumilivu hufikia kikomo ni maamuzi yanayoumiza lakini kwa usalama wa moyo na nafsi ni lazima umwache aende.
 
Usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya baada ya kuumizwa na mtu uliyempenda sana uliyemwamini sana, uliyemsaidia sana na uliyemvumilia sana na bila huruma akaamua kuondoka ama kukuumiza wakati ulipokuwa unamhitaji sana

Mapenzi yanaumiza mapenzi yanatesa lakini ni muhimu kuangalia ulikotoka.. Maisha yako ni muhimu kuliko yeye.. Hakuwapo Kabla... Kisha akaja... Mwache aende... Future yako yaweza kuwa muhimu kuliko yeye...

Umewekeza kwake sawa... Ulimkabidhi moyo wako sawa.. Lakini kama hana hisia nawe, kama hana shukrani... Kama hakupendi tena na kama kakutenda mwambie waweza kwenda... Akuachie japo pumzi yako... Isifike mahali nayo akaondoka nayo...!!!

Ili kutambua upande wa pili wa mapenzi ni lazima kuumia ni lazima kuumizwa.. Usione ndio mwisho wa maisha, chukulia kama ni changamoto... Mitihani ya dunia

Wewe si wa kwanza hutakuwa wa mwisho... Vumilia... Muda pekee ndio utayaponya majeraha ya mapenzi... Usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya unaweza kuingia chaka... Utafanya hivyo kwa ghadhabu na bila fikra timilifu.. Unaweza kuongeza tatizo badala ya kuponya majeraha....

Zipumzishe hisia... Mapenzi yanachosha sana... Jipe muda wa kutafakari upya... Ulipokosea ulipopatia, uliposhindwa kutimiza wajibu... Ulipotenda kwa weledi na chochote utakachoweza kutafakari... Baada ya kuona umepata nguvu ya kuanza tena... Fanya hivyo bila papara... Epuka uzuri wa mkakasi.....

Zijapopita siku za furaha usihuzunike bali ufurahi kwakuwa zilikuwako.. [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji779] [emoji781] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770]
Ahsante sana kaka mshana Jr. Nime kuelewa vizuri sana Ngoja nipumzishe hisia zangu.
 
tafiti-kuoa-jpg.669170
 
Back
Top Bottom