hibiscus interior
JF-Expert Member
- Jan 13, 2016
- 1,168
- 595
Usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya baada ya kuumizwa na mtu uliyempenda sana uliyemwamini sana, uliyemsaidia sana na uliyemvumilia sana na bila huruma akaamua kuondoka ama kukuumiza wakati ulipokuwa unamhitaji sana
Mapenzi yanaumiza mapenzi yanatesa lakini ni muhimu kuangalia ulikotoka maisha yako ni muhimu kuliko yeye hakuwapo kabla kisha akaja mwache aende future yako yaweza kuwa muhimu kuliko yeye.
Umewekeza kwake sawa ulimkabidhi moyo wako sawa lakini kama hana hisia nawe, kama hana shukrani kama hakupendi tena na kama kakutenda mwambie waweza kwenda akuachie japo pumzi yako isifike mahali nayo akaondoka nayo.
Ili kutambua upande wa pili wa mapenzi ni lazima kuumia ni lazima kuumizwa usione ndio mwisho wa maisha, chukulia kama ni changamoto mitihani ya dunia
Wewe si wa kwanza hutakuwa wa mwisho vumilia muda pekee ndio utayaponya majeraha ya mapenzi usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya unaweza kuingia chaka utafanya hivyo kwa ghadhabu na bila fikra timilifu unaweza kuongeza tatizo badala ya kuponya majeraha.
Zipumzishe hisia mapenzi yanachosha sana jipe muda wa kutafakari upya ulipokosea ulipopatia, uliposhindwa kutimiza wajibu ulipotenda kwa weledi na chochote utakachoweza kutafakari baada ya kuona umepata nguvu ya kuanza tena fanya hivyo bila papara epuka uzuri wa mkakasi.
Zijapopita siku za furaha usihuzunike bali ufurahi kwakuwa zilikuwako [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji779] [emoji781] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770]
Hiyo itakuzidishia maumivu mkuu,aliyeamua kuondoka ukimlazimisha mwisho wa yote aweza kukutoa roho.Lipi jema ni kumpa ruhusa,iguza donda iko siku napona yenyewehapo kwenye kumuacha aende ndio pagumu,nakula nae sahani moja tu.
naona umeamua kufukua makaburi kaka kila nipitako nakutana nakabur lako
Pole sana dear!Daah huu uzi umenigusa sana aiseeh, natamani mpaka kulia ila namshukuru Mungu kwakweli hili nalo LITAPITA.
oooho hapo mekuelewaNi kwa ombi maalum.... Kuna mtu anapita katika bonde la uvuli wa kuumizwa kihisia
Dah sijui umeniona ila sawa bhan umenitia nguvu San shukraniUsikimbilie kuanzisha mahusiano mapya baada ya kuumizwa na mtu uliyempenda sana uliyemwamini sana, uliyemsaidia sana na uliyemvumilia sana na bila huruma akaamua kuondoka ama kukuumiza wakati ulipokuwa unamhitaji sana