Chukua muda wa kuzipumzisha hisia

Chukua muda wa kuzipumzisha hisia

Usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya baada ya kuumizwa na mtu uliyempenda sana uliyemwamini sana, uliyemsaidia sana na uliyemvumilia sana na bila huruma akaamua kuondoka ama kukuumiza wakati ulipokuwa unamhitaji sana

Mapenzi yanaumiza mapenzi yanatesa lakini ni muhimu kuangalia ulikotoka.. Maisha yako ni muhimu kuliko yeye.. Hakuwapo Kabla... Kisha akaja... Mwache aende... Future yako yaweza kuwa muhimu kuliko yeye...

Umewekeza kwake sawa... Ulimkabidhi moyo wako sawa.. Lakini kama hana hisia nawe, kama hana shukrani... Kama hakupendi tena na kama kakutenda mwambie waweza kwenda... Akuachie japo pumzi yako... Isifike mahali nayo akaondoka nayo...!!!

Ili kutambua upande wa pili wa mapenzi ni lazima kuumia ni lazima kuumizwa.. Usione ndio mwisho wa maisha, chukulia kama ni changamoto... Mitihani ya dunia

Wewe si wa kwanza hutakuwa wa mwisho... Vumilia... Muda pekee ndio utayaponya majeraha ya mapenzi... Usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya unaweza kuingia chaka... Utafanya hivyo kwa ghadhabu na bila fikra timilifu.. Unaweza kuongeza tatizo badala ya kuponya majeraha....

Zipumzishe hisia... Mapenzi yanachosha sana... Jipe muda wa kutafakari upya... Ulipokosea ulipopatia, uliposhindwa kutimiza wajibu... Ulipotenda kwa weledi na chochote utakachoweza kutafakari... Baada ya kuona umepata nguvu ya kuanza tena... Fanya hivyo bila papara... Epuka uzuri wa mkakasi.....

Zijapopita siku za furaha usihuzunike bali ufurahi kwakuwa zilikuwako.. [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji779] [emoji781] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770]
Yaaani mkuu kweli,nikunyanyua moyo na kuuweka juu ya msalaba wa YESU (kwa imani yangu)na kumwambia Bwana na hili nalo jambo hebu shughulika.shika moyowangu maana bila ww mimi siwezi,simama mwenyewe maana ww ndio unawajua watu ulio waumba.ila chamsingi ni KULINDA SANA MOYO KULIKO VYOTE ULINDAVYO.Mithali 4:23

~Moyo sawa na mwanaume duniani,moyo ukiumia,waweza kuwa masikin,kichaa,usie na malengo,ulie jikinai,usie ijua kesho yako.na maisha unaweza kuyaendesha km mnyama wa porin usie sikia jua wala mvua.
 
Daah huu uzi umenigusa sana aiseeh, natamani mpaka kulia ila namshukuru Mungu kwakweli hili nalo LITAPITA.
IMG_20180116_155836_155.jpg
 
Mapenzi yanauma ila kumwacha aende ndo suluhisho ya yote!!!

We mwache aende, kuna furaha zaidi mbele yako kuliko yeye!! Siku zote amini hakuwa wako na wakati ukifika ukifika utampata wa kufanana nae....

Just let her/him go!!!!!!
Usimwache T
 
Ndugu mshana jr, ni muda gani unafaa kuzipumzisha hisia baada sokomoko la mapenzi? mwezi, mwaka miaka...!!??
 
[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Back
Top Bottom