Chukua muda wa kuzipumzisha hisia

Chukua muda wa kuzipumzisha hisia

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya baada ya kuumizwa na mtu uliyempenda sana uliyemwamini sana, uliyemsaidia sana na uliyemvumilia sana na bila huruma akaamua kuondoka ama kukuumiza wakati ulipokuwa unamhitaji sana

Mapenzi yanaumiza mapenzi yanatesa lakini ni muhimu kuangalia ulikotoka maisha yako ni muhimu kuliko yeye hakuwapo kabla kisha akaja mwache aende future yako yaweza kuwa muhimu kuliko yeye.

Umewekeza kwake sawa ulimkabidhi moyo wako sawa lakini kama hana hisia nawe, kama hana shukrani kama hakupendi tena na kama kakutenda mwambie waweza kwenda akuachie japo pumzi yako isifike mahali nayo akaondoka nayo.

Ili kutambua upande wa pili wa mapenzi ni lazima kuumia ni lazima kuumizwa usione ndio mwisho wa maisha, chukulia kama ni changamoto mitihani ya dunia

Wewe si wa kwanza hutakuwa wa mwisho vumilia muda pekee ndio utayaponya majeraha ya mapenzi usikimbilie kuanzisha mahusiano mapya unaweza kuingia chaka utafanya hivyo kwa ghadhabu na bila fikra timilifu unaweza kuongeza tatizo badala ya kuponya majeraha.

Zipumzishe hisia mapenzi yanachosha sana jipe muda wa kutafakari upya ulipokosea ulipopatia, uliposhindwa kutimiza wajibu ulipotenda kwa weledi na chochote utakachoweza kutafakari baada ya kuona umepata nguvu ya kuanza tena fanya hivyo bila papara epuka uzuri wa mkakasi.

Zijapopita siku za furaha usihuzunike bali ufurahi kwakuwa zilikuwako [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji779] [emoji781] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770] [emoji770]
 
Mapenzi yanauma ila kumwacha aende ndo suluhisho ya yote we mwache aende, kuna furaha zaidi mbele yako kuliko yeye siku zote amini hakuwa wako na wakati ukifika ukifika utampata wa kufanana nae.

Just let her/him go!!!!!!
 
Mwambie kwa upole
36bc43decb9c124581ef96c7c3fa28ef.jpg
 
Back
Top Bottom