Chukua tahadhari unapokwenda kununua bati kwenye kiwanda cha wachina TAZARA

Changamoto2015

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2012
Posts
773
Reaction score
314
Sina lengo la kuwaharibia biashara. Lakini pia sipendi yakukute yaliyonikuta.

Kiufupi tu:

Bei ya bati geji 28 kwa metre moja ni Tshs 8500/=. Kofia Max 3 metres= Tshs 15,000/=.

kilichotokea:
Bati nilizonunua mwanzoni zimekuja nyepesi sana na kwa mujibu wa fundi sio Geji 28. Maana bati hazikutosha na hivyo ikalazimu ziongezwe zingine.

Mbili, upana (width) wa bati zilizokuja mwanzoni zinatofautiana na upana wa bati za mara ya 2.

Tatu, bati zimekuja bila muhuri wa kuthibitisha geji. Hili nimeambiwa na agent mmoja baada ya kumuelezea kilichonitokea. Akaniuliza hizo bati zimepigwa muhuri wa kuthibitisha geji? Nilipokagua sikuona muhuri.

Nne, nilipoomba risiti ya TRA nilipewa ambayo hai reflect bei halisi. Nilipohoji niliambiwa hiyo bei niliyopewa haina VAT na kama nahitahitaji yenye bei halisi basi niongeze pesa Tshs 9000 kwa metre. Kumbuka wakati huo bati zimeshatoka nipo kwenye harakati za kupakia.

Kuhusu Fundi:

Mafundi wanaiba sana bati. Ni muhimu kuwepo site wakati kazi inaendelea. Na kila siku baada ya kazi hesabu idadi ya bati zilizobaki.
Nimeyagundua haya baada ya kupungukiwa na bati, jumba ya jirani ilianza kupauliwa kabla yangu. Wiki moja baadae nami nilianza. Baada ya kuwa nimepungukiwa bati niliambiwa kwa jirani yangu kuna bati zilibaki, hivyo kikaomba namba niongee na jirani kumuomba aniuzie.
Cha ajabu nilipewa namba ya fundi na yeye ndie alikuwa muuzaji. Kufuatilia nikagundua mwenye nyumba hajui lolote na hivyo alikuwa kapigwa kama pc 10 za bati zenye urefu wa metre 5 each. Sikuweza kununua na hivyo kunilazimu kwenda tena kiwandani kununua mara ya pili.
 
Ujenzi ni vita siyo lele mama!! Survey kabla ya kufanya chochote, ukianza kujenga unakuwa na experience yote!! Pole sana kwa yaliyokukuta na asante kwa info nzuri
 
Ujenzi ni vita siyo lele mama!! Survey kabla ya kufanya chochote, ukianza kujenga unakuwa na experience yote!! Pole sana kwa yaliyokukuta na asante kwa info nzuri

Asante mkuu! We acha tu yaani unajifunga mkanda ili kujikwamua lakini unarudishwa nyuma na wahuni wengine.

Kuna mchina mmoja pale jina lake linaanzia na K...N kwa kushirikiana na mbongo mmoja mfanyakazi wa pale jina lake linaanzia na H..A ndio wanaocheza michezo hii michafu kuwatia watu hasara.
 
Kwanini hukununua ALAF?

Bottom line, mara nyingine, tumia wataalamu wakuwakilishe. Ikitokea mapungufu, unawabana kimkataba. Ujenzi si kila mtu anaweza kusimamia.
 

Jaribu kurudia kusoma na kuelewa alichoandika mleta hoja, usikurupuke kucomment!
 
bati kutokutosha si uthibitisho wa kuwa si gaji 28, ref hoja ya kwanza.ungeeleza wepesi wake tu ukoje
 
Haya yote yatakwisha endapo mafundi watakuwa waaminifu wanapopewa hela ya kwenda kununua material na kuacha ubadhilifu...
 
Haya yote yatakwisha endapo mafundi watakuwa waaminifu wanapopewa hela ya kwenda kununua material na kuacha ubadhilifu...

Mafundi lazima ubanane nao hapo kwa hapo. Otherwise utaumizwa tu. Na ukiwabana sana huwa wanatabia ya kubebanisha bati ili kukukomoa. Fundi jinga sana.
 
Mafundi lazima ubanane nao hapo kwa hapo. Otherwise utaumizwa tu. Na ukiwabana sana huwa wanatabia ya kubebanisha bati ili kukukomoa. Fundi jinga sana.

Sasa fundi kama huyo anamkomoa nani kama sio ujinga....mimi ninavyojua fundi anapata kazi kulingana na ubora wa kazi zake nikiwa na maana kuwa ubora wa kazi ndio unaomtangaza....sasa kama anafanya kazi kwa kumkomoa bosi lazima atakuwa na mtindio wa ubongo...kwa kuwa akija kukutembelea jamaa anaweza akavutiwa na ujenzi wako na akataka ajenge kama wewe..sasa hapo si ndio unamuonganishia dili moja kwa moja...
 

Read between the lines utaelewa kwamba sijanunua bati kwa jirani baada ya kugundua zinauzwa na fundi. Na hivyo kunilazimu niende kutoa order mara ya pili kiwandani. Na ndipo nilipogundua hayo mapungufu.

Mkuu usipende kukurupuka kutoa comments kama huwezi kusoma kuelewa kilichoandikwa.

Kuhusu suala la kutumia wataalamu sidhani kwamba kila mtu anaweza kufanya hivyo kulingana na gharama na vilevile sio guaranteed kwamba fundi mtaalam akiharibu kazi unaweza kumuwajibisha na kufidia hasara. Kwa upande mwingine hao mafundi unaowaita ni wataalam ndio hao wanatumia mafundi wetu wa kawaida huku mtaani.

Wao wanakuwa madalali wa kuja kukagua kazi. Unamlipa yeye milioni 2, naye anatafuta fundi wa kumlipa laki 6 kwa kazi yote mwanzo mwisho.

Kiufupi kama huna uwezo wa kuajiri registered company yenye proven track record ni bora kufanya kazi mwenyewe direct na mafundi hawa hawa bila kupitia ma middleman wa VETA wanaojiita mafundi wataalam na kazi hawajui ( la hasha is wote).
 
bati kutokutosha si uthibitisho wa kuwa si gaji 28, ref hoja ya kwanza.ungeeleza wepesi wake tu ukoje

Nimeeleza bati zilizoleta mara ya kwanza ukifananisha na za mara ya pili kwa wepesi na upana ( width) zinatofautiana. Na fundi mwenyewe kanithibitishia kwamba geji ni tofauti.
 

ALAF nawakubali,walinihudumia mwaka 2010 sijajutia bidhaa zao....ukitaka fundi wa ukweli mwenye uelewa wa viwango vya mabati na mtaalam wa kuezeka nyumba nitafute
 
ALAF nawakubali,walinihudumia mwaka 2010 sijajutia bidhaa zao....ukitaka fundi wa ukweli mwenye uelewa wa viwango vya mabati na mtaalam wa kuezeka nyumba nitafute

kweli mkuu hapa najilaumu kwanini sikwenda kununua ALAF. Hawa wachina wahuni sawa na wabongo wauza mbao wa buguruni, yaani ujanja ujanja tu.
 
Bati ngapi zilitosha nyumba? Nyumba ya ukubwa gani?
 
Read between the lines utaelewa kwamba sijanunua bati kwa jirani baada ya kugundua zinauzwa na fundi. ...

Mkuu, hiyo btwn the line umeitumia vibaya. Hebu soma hiyo sentensi ya mwisho kwenye mada yako. Haihitaji between the lines. Ibadili au ongezea kuwa mwishowe hukununua hizo bati za wizi.

Kuhusu wataalamu, gharama ya kuletewa bati za kubumba, mara hazitoshi, na hapo ni bati. Nondo, cement, mbao, etc. Ujenzi hugharimu mara mbili kwa kuhofia wataalamu ilhali we si mjuzi wa ujenzi.

Kukaa site kukodoa macho hakuzuii kupigwa. Mafundi wajanja sana. We ajiri kampuni tu. Wala usiwaze mkuu. Tofauti haiwagi kubwa.
 
Pole mkuu, umenikumbusha nyumba moja ya fundi INA mabati ya rangi tofauti sita yamechanganywa migongo mipana na migongo midogo . yule bwn ni fundi ukimuuliza anadai eti yy anapenda kuwa tofauti
 
Mkuu nilinunua TAZARA kiwanda kinaitwa AFR-INA UNITE DEVELOPMENT CO. LIMITED

P.O BOX 2007

PUGU ROAD

TIN: 120-146- 556

Sikijui mkuu......

Nilidhani ALAF , nawafahamu kiasi fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…