Changamoto2015
JF-Expert Member
- Oct 1, 2012
- 773
- 314
Sina lengo la kuwaharibia biashara. Lakini pia sipendi yakukute yaliyonikuta.
Kiufupi tu:
Bei ya bati geji 28 kwa metre moja ni Tshs 8500/=. Kofia Max 3 metres= Tshs 15,000/=.
kilichotokea:
Bati nilizonunua mwanzoni zimekuja nyepesi sana na kwa mujibu wa fundi sio Geji 28. Maana bati hazikutosha na hivyo ikalazimu ziongezwe zingine.
Mbili, upana (width) wa bati zilizokuja mwanzoni zinatofautiana na upana wa bati za mara ya 2.
Tatu, bati zimekuja bila muhuri wa kuthibitisha geji. Hili nimeambiwa na agent mmoja baada ya kumuelezea kilichonitokea. Akaniuliza hizo bati zimepigwa muhuri wa kuthibitisha geji? Nilipokagua sikuona muhuri.
Nne, nilipoomba risiti ya TRA nilipewa ambayo hai reflect bei halisi. Nilipohoji niliambiwa hiyo bei niliyopewa haina VAT na kama nahitahitaji yenye bei halisi basi niongeze pesa Tshs 9000 kwa metre. Kumbuka wakati huo bati zimeshatoka nipo kwenye harakati za kupakia.
Kuhusu Fundi:
Mafundi wanaiba sana bati. Ni muhimu kuwepo site wakati kazi inaendelea. Na kila siku baada ya kazi hesabu idadi ya bati zilizobaki.
Nimeyagundua haya baada ya kupungukiwa na bati, jumba ya jirani ilianza kupauliwa kabla yangu. Wiki moja baadae nami nilianza. Baada ya kuwa nimepungukiwa bati niliambiwa kwa jirani yangu kuna bati zilibaki, hivyo kikaomba namba niongee na jirani kumuomba aniuzie.
Cha ajabu nilipewa namba ya fundi na yeye ndie alikuwa muuzaji. Kufuatilia nikagundua mwenye nyumba hajui lolote na hivyo alikuwa kapigwa kama pc 10 za bati zenye urefu wa metre 5 each. Sikuweza kununua na hivyo kunilazimu kwenda tena kiwandani kununua mara ya pili.