Chukua tahadhari unapokwenda kununua bati kwenye kiwanda cha wachina TAZARA

Chukua tahadhari unapokwenda kununua bati kwenye kiwanda cha wachina TAZARA

Ni jukumu lako kuwa makini kila unapofanya manunuzi ya kitu chochote hasa ukizingatia utapeli na wizi na badhaa feki ndio vinatawala bongo.
 
Ni jukumu lako kuwa makini kila unapofanya manunuzi ya kitu chochote hasa ukizingatia utapeli na wizi na badhaa feki ndio vinatawala bongo.

Kweli mkuu, lengo la thread ni kuwataadharisha wengine wasije kuingia kwenye trap kama hii. Sidhani kama ni jambo zuri kukaa kimya kwa vile mimi nimeumizwa basi niache na wenzangu waumie.
 
tatizo uwa tunawaamini sana mafundi
kuna siku fundi mmoja alimpigia tajiri yake kuwa zile basi 110 walikadiria QS kwenye BOQ hazitoshi,jamaa akaenda kuhakikisha akukuta kweli zinapelea kama bati 25,alipompigia QS wake akasema ni uongo akamshauri tajiri apande juu ya paa akague bati,kuangalia vizuri akakuta bati zaidi 30 kapandisha mbilimbili ili baadae ashushe mzigo fundi aweze kuuza
jamani hawa mafundi wengi ni matapeli usiwahamini ata kidogo
 
bati kutokutosha si uthibitisho wa kuwa si gaji 28, ref hoja ya kwanza.ungeeleza wepesi wake tu ukoje
kama ni mimi ningechukua bati 2 ningeenda TBS na tume ya faily competition huyu mchina angelipa mpaka misumari.Nafikiri wakati umefika kwa watanzania kulalamika kwa vitendo na sio maneno.Ingekuwa Kenya au Nigeria hicho kiwanda hakika muda huu ni story nyingine kulalamika huku akusaidii kwani ata dakika hii watanzania wengine wanatapeliwa live.Hakika ningekuwa mie mziki wake mchina angejuta.
 
Kwanini hukununua ALAF?
Hizo bati mlizoiba jirani zilifanana na za kwako? Umelaumu hao wachina ila na wewe ni kule kule tu. Ulinunuaje bati jirani bila kuongea na mwenye nyumba?

Bottom line, mara nyingine, tumia wataalamu wakuwakilishe. Ikitokea mapungufu, unawabana kimkataba. Ujenzi si kila mtu anaweza kusimamia.
Mtoa hoja kakuambia aligoma kununua za jirani baada ya kugundua ni za wizi, kama hukuelewa ungeuliza kwanza. haraka za nini?
 
Mtoa hoja kakuambia aligoma kununua za jirani baada ya kugundua ni za wizi, kama hukuelewa ungeuliza kwanza. haraka za nini?

Nilichangia kabla hajahariri. Mwanzo iliishia "... Kufuatilia nikagundua mwenye nyumba hajui lolote na hivyo alikuwa kapigwa kama pc 10 za bati zenye urefu wa metre 5 each". (mkolezo ni mimi nimeweka).

Sasa iko vizuri inaeleweka hakununua.
 
Sina lengo la kuwaharibia biashara. Lakini pia sipendi yakukute yaliyonikuta.

Kiufupi tu:

Bei ya bati geji 28 kwa metre moja ni Tshs 8500/=. Kofia Max 3 metres= Tshs 15,000/=.

kilichotokea:
Bati nilizonunua mwanzoni zimekuja nyepesi sana na kwa mujibu wa fundi sio Geji 28. Maana bati hazikutosha na hivyo ikalazimu ziongezwe zingine.

Mbili, upana (width) wa bati zilizokuja mwanzoni zinatofautiana na upana wa bati za mara ya 2.

Tatu, bati zimekuja bila muhuri wa kuthibitisha geji. Hili nimeambiwa na agent mmoja baada ya kumuelezea kilichonitokea. Akaniuliza hizo bati zimepigwa muhuri wa kuthibitisha geji? Nilipokagua sikuona muhuri.

Nne, nilipoomba risiti ya TRA nilipewa ambayo hai reflect bei halisi. Nilipohoji niliambiwa hiyo bei niliyopewa haina VAT na kama nahitahitaji yenye bei halisi basi niongeze pesa Tshs 9000 kwa metre. Kumbuka wakati huo bati zimeshatoka nipo kwenye harakati za kupakia.

Kuhusu Fundi:

Mafundi wanaiba sana bati. Ni muhimu kuwepo site wakati kazi inaendelea. Na kila siku baada ya kazi hesabu idadi ya bati zilizobaki.
Nimeyagundua haya baada ya kupungukiwa na bati, jumba ya jirani ilianza kupauliwa kabla yangu. Wiki moja baadae nami nilianza. Baada ya kuwa nimepungukiwa bati niliambiwa kwa jirani yangu kuna bati zilibaki, hivyo kikaomba namba niongee na jirani kumuomba aniuzie.
Cha ajabu nilipewa namba ya fundi na yeye ndie alikuwa muuzaji. Kufuatilia nikagundua mwenye nyumba hajui lolote na hivyo alikuwa kapigwa kama pc 10 za bati zenye urefu wa metre 5 each. Sikuweza kununua na hivyo kunilazimu kwenda tena kiwandani kununua mara ya pili.

Ndugu pole, je kuna uwezekano wa kununua bati bila kupita kwa wakala maana nimeongea na wakala mmoja kaniambia atanifanyia sh 10500 per m naona kama ananipiga parefu..
 
Ndugu pole, je kuna uwezekano wa kununua bati bila kupita kwa wakala maana nimeongea na wakala mmoja kaniambia atanifanyia sh 10500 per m naona kama ananipiga parefu..

Kibaya zaidi hawa wapigaji hawasogei po pote, wakishapiga wanaishia Kimboka, mitaa ya Buguruni kwenye maduka ya mbao, kumejaa vibaka, kama unanunua mbao treated nenda na futi kamba yako kabisa. La huwezi bora uende TWICO.
 
-------------------------------------------------------------------------------
 
sina lengo la kuwaharibia biashara. Lakini pia sipendi yakukute yaliyonikuta.

Kiufupi tu:

Bei ya bati geji 28 kwa metre moja ni tshs 8500/=. Kofia max 3 metres= tshs 15,000/=.

Kilichotokea:
Bati nilizonunua mwanzoni zimekuja nyepesi sana na kwa mujibu wa fundi sio geji 28. Maana bati hazikutosha na hivyo ikalazimu ziongezwe zingine.

Mbili, upana (width) wa bati zilizokuja mwanzoni zinatofautiana na upana wa bati za mara ya 2.

Tatu, bati zimekuja bila muhuri wa kuthibitisha geji. Hili nimeambiwa na agent mmoja baada ya kumuelezea kilichonitokea. Akaniuliza hizo bati zimepigwa muhuri wa kuthibitisha geji? Nilipokagua sikuona muhuri.

Nne, nilipoomba risiti ya tra nilipewa ambayo hai reflect bei halisi. Nilipohoji niliambiwa hiyo bei niliyopewa haina vat na kama nahitahitaji yenye bei halisi basi niongeze pesa tshs 9000 kwa metre. Kumbuka wakati huo bati zimeshatoka nipo kwenye harakati za kupakia.

Kuhusu fundi:

Mafundi wanaiba sana bati. Ni muhimu kuwepo site wakati kazi inaendelea. Na kila siku baada ya kazi hesabu idadi ya bati zilizobaki.
Nimeyagundua haya baada ya kupungukiwa na bati, jumba ya jirani ilianza kupauliwa kabla yangu. Wiki moja baadae nami nilianza. Baada ya kuwa nimepungukiwa bati niliambiwa kwa jirani yangu kuna bati zilibaki, hivyo kikaomba namba niongee na jirani kumuomba aniuzie.
Cha ajabu nilipewa namba ya fundi na yeye ndie alikuwa muuzaji. Kufuatilia nikagundua mwenye nyumba hajui lolote na hivyo alikuwa kapigwa kama pc 10 za bati zenye urefu wa metre 5 each. Sikuweza kununua na hivyo kunilazimu kwenda tena kiwandani kununua mara ya pili.

kwa kuwasaidia wengine ingebidi kuwaripoti tbs
 
Nimeeleza bati zilizoleta mara ya kwanza ukifananisha na za mara ya pili kwa wepesi na upana ( width) zinatofautiana. Na fundi mwenyewe kanithibitishia kwamba geji ni tofauti.

hivi cement ya SOL iloandikwa made in China ni imported au ya Mbagala?

japo hawachakachui uzito ni 50 Kg kamili, ukifungua mifuko tofauti cement ina rangi tofauti
 
Ndugu pole, je kuna uwezekano wa kununua bati bila kupita kwa wakala maana nimeongea na wakala mmoja kaniambia atanifanyia sh 10500 per m naona kama ananipiga parefu..

Ndio mkuu inawezekana, mimi nilinunua bila kupitia kwa wakala. Kuna jamaa mwingine aliniambia kuna kiwanda kingine cha bati maeneo ya TABATA. Nasikia wao ni wageni na bado hawajaanza mambo ya uchakachuaji kama hawa wakongwe. Endapo nitapata details zao nitaweka hapa.
 
hivi cement ya SOL iloandikwa made in China ni imported au ya Mbagala?

japo hawachakachui uzito ni 50 Kg kamili, ukifungua mifuko tofauti cement ina rangi tofauti
Sina uhakika mkuu mimi nilitumia cement ya Nyati pamoja na Twiga. Tofali nilinunua hivyo sijui walitumia cement gani lakini zipo imara.
 
kwa kuwasaidia wengine ingebidi kuwaripoti tbs

Mkuu kuna wakati fulani nilipata tatizo nikaenda ku report polisi. Sina hamu kwa jinsi suala langu lilivyoshughulikiwa na polisi. Yaani nafuatilia fedha zangu nilizotapeliwa na lakini jambo la ajabu ninaombwa rushwa na askari ili kwenda kumkamata mtuhumiwa.

Sina hakika kama TBS kuna ufanisi wa hivyo, maana kuna thread humu kuhusiana na importation ya cement TBS wanalalamikiwa kwa ukiritimba.
 
Kwanini hukununua ALAF?
Hizo bati mlizoiba jirani zilifanana na za kwako? Umelaumu hao wachina ila na wewe ni kule kule tu. Ulinunuaje bati jirani bila kuongea na mwenye nyumba?

Bottom line, mara nyingine, tumia wataalamu wakuwakilishe. Ikitokea mapungufu, unawabana kimkataba. Ujenzi si kila mtu anaweza kusimamia.

Hivi umesoma kweli kabla ya kutoa comment?
 
Ndio mkuu inawezekana, mimi nilinunua bila kupitia kwa wakala. Kuna jamaa mwingine aliniambia kuna kiwanda kingine cha bati maeneo ya TABATA. Nasikia wao ni wageni na bado hawajaanza mambo ya uchakachuaji kama hawa wakongwe. Endapo nitapata details zao nitaweka hapa.

Mkuu, washauri watu waende ALAF au kwa wakala wao. Hawa wageni tena wachina ni majanga kwenye ubora.

Kwa yale mabati kigae waende Nabaki. Nyumba ni uwekezaji mkubwa sana maishani. Haina haja kubahatisha au kujaribu vya bei chee. Mara nyingi rahisi aghali!
 
Back
Top Bottom