1. Sea salt inakuwa imetokana na kuvukisha maji ya bahari wakati ile ya mawe inachimbwa kutoka miamba inayodhaniwa kuwa ilitokea baada ya habari au maziwa ya zamani kukauka
2. Chumvi ya bahari huwa inakuwa na rangi nyeupe au off-white wakati zile za miamba kama Himalayan salt zinakuwa na rangi mbalimbali kutokana na aina ya madini yaliyomo
Zinaweza kuwa nyeupe, pink, nyeusi, brown nk
3. Wingi wa madini inategemeana na asili ya eneo ambapo chumvi husika imetolewa na pia mchakato wa kuisafisha
4. Chumvi ya bahari inaweza kuwa na uchafu hasa plastik ndogondogo (microplastics) wakati zile za mawe hazijachafuliwa na uchafuzi wa bahari wa kisasa
5. Chumvi ya miamba kama himalayan salt inaweza kuwa bora zaidi kwa matumizi ya kawaida na tiba kuliko ya bahari
View attachment 3311453