Chumvi ya Neel (Neel salt) ni biashara ya nani?

Watu na malkia wao, sijui mlimtolea Mali kiasi gani?
 
...kila mfanyabiashara anatamani bidhaa yake itumiwe na kila mtu duniani kama ikibidi,
"Inelastic", fafanua mkuu wengine commerce tuliishia form two
lastic = hii ni lugha ya uchumi na masoko ambayo kwa maneno yasiyo rasmi ni kunyumbulika, kuvutikana kama mpira wa manati, kuongezeka urefu au ujazo, wingi, utumiaji wa bidhaa sokoni. Inelastic ni kinyume lastic, maana yake isiyonyumbulika wala kubadilika wala kuongezeka urefu, ujazo, ukubwa, wingi, uhitaji, n.k. Mfano, kama bei ya sukari ikipunguzwa bei (price) watu wengi zaidi wanaweza kununua sukari zaidi na kunywa chai, na kama bei ya bia ikiongezwa zaidi juu wateja wa bia wanaweza kupungua sana, hivyo bidhaa zote zenye tabia kama hiyo ya kunyumbulika/kubadilikabalika uhitaji wake kwenye soko kutokana na bei na matangazo zinaitwa "elastic goods". Lakini chumvi haina tabia hiyo kwakuwa mahitaji na uhitaji wa chumvi upo tu palepale hata kama bei ya chumvi itapunguzwa au kuongezwa, itatangwa au haitatangazwa, ndiyo maana wataalamu wetu humu ndani wameiweka chumvi kwenye kundi la bidhaa ambazo "inelastic" kwakuwa bei au matangazo hayawezi kuathiri matumizi wala ununuzi wa chumvi madukani.

Anachofanya mmiliki wa neel salt ni kutangaza tena na tena na tena brand yake ya Neel salt kwenye masikio na macho ya watumiaji wa chumvi ili kila mtu anapokwenda sokoni asiseme naomba chumvi badala yake asememe naomba neel sawa na wale wanaoita OMO sabuni zote za unga, au Kiwi dawa zote za viatu, au panadol dawa zote za maumivu kwa kuwa wao walizitangaza na kuzisambaza saaaana bidhaa zao hizo kwanjia tofautitofauti.

Nadhani mkuu nimesaidia kidogo japo mimi hili sio chimbo langu kabisaa.
 
....umeelezea vizuri sana kaka, ila hapo ulipoifananisha na omo ndo kidogo si sawa. Ila chumvi na Panado zipo category moja ya inelastic.
Kwa nini Panadol/Hedex zinatangazwa sana ? .....jibu: unaifanya Brand kuwa common, but you must always focus in distribution. Otherwise, consumer wataambiwa ipo Panadol ya Keko.
Kuitangaza sana Panadol haitafanya watu wanunue tu hata kama huumwi bali itakuwa a trusted choice. Hivyo volume (mauzo mengi) yanategemea distribution na si matumizi makubwa.
Tukirudi kwenye chumvi, yale yale tu, sasa hivi wengi wa wanunuzi uswahilini wanaiita chumvi ya majuto.
Kwahiyo shida tayari hapo, brand ya neel salt haitashika tena bali majuto na hilo si jambo poa.
 

Read the below. Its not the product, its the BRAND

Tata Salt’s Promotional Strategies

My brother, you can promote ANYTHING. Soma jinsi promotion ilivyofanywa kubadilisha tabia ya wanawake wasiovuta sigara, kuanza kuvuta sigara

Torches of Freedom: Women and Smoking Propaganda - Sociological Images
 
Sijakataa kwamba haitakiwi kuifanyia chumvi promotion au kui brand chumvi.
Nilichojaribu kuonyesha na kuainisha ni budget waliotumia wakati huo huo hawajajiimarisha katika distribution na hawa clear exclusivity !
Tata salt ilikuwa chumvi ya kwanza ya iodine (Hiyo ni exclusivity)
Wanajitofautisha sokoni. Nimesema humu at least wangekuwa na exclusive product portfolio pia labda inge match na nguvu wanazo tumia.
 
Wewe uko mbali sana na ukweli, duniani kote hata nchi zilizoendelea hawanunui bidhaa bila kufahamu umiliki wake, nani kutengeneza, viwango, expiry date, kodi nk. Wewe unafakamia tu. Ndio maana bidhaa zetu zinashindwa kupenya kwenye masoko ya nje.
Tanzania utamaduni huo haupo
 
Nimesoma hiyo mikakati yote miwili ambayo wametumia hao wa iodinized salt wa India na mikakati ya Edward Bernal ndugu yake na Segmund Freud ya kuimarisha mkakati wa wanawake kuvuta sigara ili kuimarisha soko lao. Hiyo ya Bernal ndo balaa zaidi kwnza kitendo cha kukifanya kitu kilichokuwa unathorized public issue mpaka kuwa authorized si mchezo. Thank you very much mkuu!
 
Sidhani kama nimewahi kuona tangazo la chumvi duniani kokote kabla ya haya ya bongo, huyu jamaa ni moron au genius time will tell.
Mtu unaweza kununua chumvi kwa matangazo ya Majuto?
 
wakati wa sikuu mauzo ya soda yanaongezeka kwasababu ni kipindi ambacho watu wengi wanapata angalau soda moja au hata watoto 3 kugawiana soda moja tofauti na chumvi ambayo inaliwa na kila mtu kila siku siku zote. tuko watu 55,000,000 nchini kama kila mtu atakula 3g per day (kwenye chakula, nyamachoma, chachandu, maembe mabichi, mahindi ya kuchoma mijini, matango, mtori) ni sawa na kuuza chumvi kiasi cha 55,000,000 x 3g = 165,000Kg, sawa na tani 165 za chumvi kwa siku. Haya ni matumizi makubwa sana kuliko biashara ya sukari na soda zako ambazo wanywaji hawazidi hata 5m kwa siku hapa nchini.
 
Hata mimi itanibidi nijue ni biashara ya nani, maana mwanangu hataki chumvi yoyote nyumbani zaidi ya Neel salt[emoji13] [emoji13]
 
Kwani akiomba picha ya majuto itumike kwenye pakti ya chumvi ya neel si sawa tu pia?
 
Huwezi kuanza na distribution kabla ya awareness. Sisi sote hatujui amejipanga vipi kwa distribution, ni mapema mno kumkosoa kuhusu distribution. Yeye ni lazima anatumia model na theory fulani iliyofanikiwa katika biashara hii ya neel salt.
 
Daaah....theory zako za ajabu ajabu sana. Ungetulia ufundishwe, hii ni fani kama fani nyingine.
Nilichojaribu mimi ni kuwa critic kwa approach ambayo amechukua Marketing Manager wa kampuni hiyo. Budget aliyotumia au anayotumia ni kubwa sana bila kutengeneza miundo mbinu ya usambazaji ya uhakika.
By the way jamaa aliyefanya hivyo ni mhindi na amewahi kuuza sabuni ya unga. Na sabuni ya unga ipo katika group la fmcg.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…