Wadau wa JF Doctor,
Nina mdogo wangu anasumbuliwa na chunusi za mda mrefu sana, kama kuna mtu anayejua dawa ambyo itamsaidia bila kubadilisha rangi ya ngozi yake atusaidie.
Asubuhi njema.
================
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
1.Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu
3.Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
4.Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
5.Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
6.Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
7.Punguza mawazo
Chunusi ni tatizo sugu linalosababishwa na
Mambo kadha wa kadha. Tafiti nyingi za kisayansi zimeshafanywa na zinaendelea
mpaka leo kutafuta mbinu au tiba ya haraka kwa tatizo hili.
Kimila, wengi husema chunusi ni dalili ya kutunikiwa kupendwa na mtu aliyeko mbali na usiyemfahamu (secret admirer), eti basi ndio maana unatokwa na chunusi (tabasamu basi kidogo).
Wapo wanaosema zipo chunusi za kupevusha yai la hedhi kwa wanawake na wasichana pindi tarehe za mzunguko wake zinapokaribia.
Chunusi za namna hii humtoka
Mtu kamoja tu na kuwa haijifichi kabisa huku chache huwatoka katika masikio na wengine
ndani ya pua. Matokeo ya tafiti za kisayansi za kiutaalam imegundua kwamba chunusi husababishwana kuongezeka kwa uzalishwaji wa 'Testosterone hormone' na mafuta ya mwili 'sebum' wakati wa mabadiliko ya kimwili.
(Sebum ni aina ya mafuta kama nta yanayozaliwa kwenye vinyweleo chini ya ngozi yako). Chunusi pia husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo ya kisaikolojia pamoja na lishe iliyojaa sukari nyingi na mafuta.
Bidhaa kama Manjano (Turmeric),
Giligilani, nyanya, ndimu, Aloe Vera, Zinc na Vitamin ‘A’ ni vitu vya asili vinavyo weza kutibu chunusi. Kuna baadhi ya bidhaa ambazo hazishauriwi kutumiwa hasa kama
mtu unatatizo la kiafya au mjamzito hivyo unatakiwa kuwasiliana na daktari wako kwa
ushauri kabla ya kutumia hizi vitamin na dawa.
T1PS MUHIMU ZA KUZINGATIA
1. Hakikisha unaacha kama sio unapunguza vyakula vyenye mafuta sheteshete na sukari
nyingi mpaka utakapomaliza tiba yako. Mfano chipsi, vitumbua, chapati, keki, biskuti, pipi,
soda, nk uviache au upunguze mpaka utakapopona chunusi.
2. Umeshasikia mara nyingi kuwa “maji ni tiba”, jenga tabia ya kunywa maji angalau glasi 8 kwa kutwa nzima.
3. Osha uso wako mara mbili kwa siku. Usinawe uso wako mara kwa mara kama samaki. Tumia sabuni iliyoandikwa ‘mild soap’ (mfano Protex Acne Soap au gentle facial wash) na maji ya vuguvugu wakati wa kuosha uso wako.
4. Tumia cream au lotion yenye ‘benzoyl peroxide’ ndani yake. Ukienda pharmacy
(duka la dawa) unaweza kuulizia kwa muhudumu.
5. Usijaribu kuzitumbua chunusi mwenyewe maana unaweza kusukuma ‘infection’
ikaingia zaidi ndani ya ngozi yako ambayo itasababisha uvimbe mwingine na wekundu
kujitokeza. Kama unataka kuzitumbua chunusi zilizoiva ni vyema uende ‘Professional
salon’ ukafanyiwe ‘facial treatment’ kitaalam.
6. Kama unahitaji kuondoa chunusi kwa ajili ya shughuli maalum kama harusi au mkutano
ukiwa kama mtoa mada, nenda kwa daktari wa ngozi ‘dermatologist’ akusaidie
kukupatia tiba ya chapchap. Maana anaweza kukuandikia dawa za antibiotics za kumeza
au za kupaka – itategemea na hali ya chunusi na ngozi yako.
7. Jaribu kujizuia kugusa uso wako na mikono kila mara. Ukiwa unaongea kwenye
simu jaribu kuzuia simu isiguse uso wako – kunaweza kukawa na ‘sebum’ juu ya ngozi
yako itakayokuathiri .
8. Hakikisha unanawa mikono yako mara kwa mara kila unapotoka chooni au kila baada ya
masaa kadhaa. Unaweza pia kutumia ‘antibacterial hand gel’. Mikono yako mara
zote iwe misafi.
9. Unapotaka kugusa uso wako mara zote, hakikisha umenawa mikono yako na sabuni
hasa kabla ya kupaka lotion, cream au make-up.
10. Kama una vaa miwani, inatakiwa zipanguswe mara kwa mara maana zinaweza
zoa 'sebum' kwenye ngozi yako.
11. Ngozi yako intakiwa ipumue. Kama chunusi ziko mgongoni, kwenye mabega au
kifuani, hakikisha unavaa nguo zisizobana. Kama inakubidi kuvaa nguo za kubana hakikisha ni safi na unazifua mara kwa mara.
12. Usiende kulala na make-up usoni. Tumia make-up isiyokuwa na mafuta au soma label
iliyoadikwa ‘Oil free’.
13. Nywele zako zinazogusa usoni ziwe safi wakati wote au zisiguse uso wako kabisa
maana na zenyewe pia zina uwezo wa kuzoa ‘sebum’ na kuambukiza sehemu zingine
ambazo chunusi hazijatokea.
14. Epuka na jua kali maana mionzi mingi ya jua kwenye uso au ngozi yako huleta jasho na
kuzalisha ‘sebum’.
15. Hakikisha foronya ya mto wako unabadilisha kila baada ya siku moja au mbili. Inashauriwa kama una chunusi zifuliwe kila siku - hasa kama usiku unatokwa na jasho
usoni wakati wa kulala. Kuna uwezekano mkubwa wa ‘sebum’ kubakia kwenye foronya
na kuambukiza sehemu zingine za ngozi yako.
MziziMkavu anasema,
Dawa ya kuondoa Chunusi kwa tiba asilia
Hii ni dawa nzuri kwa wale wote wenye Chunusi, kama utafuata maelekezo vizuri utaweza kupata matokeo mazuri.
Mahitaji
Kijiko cha chai kimoja - Juice ya Viazi mbatata
Nusu kijiko cha chai - Unga wa Lozi
robo kijiko cha chai - Manjano
Jinsi ya kutengeneza
Changanya vitu vyote pamoja kisha pakaa kwenye vipele vyeusi (usipake uso mzima kwenye vipele tu). Iache kwa muda wa nusu saa au hata unaweza kulala nayo. Pakaa kila siku kwa muda wa wiki mbili. Baadae utapaka kwa wiki mara mbili mpaka uone umeondoka weusi.
MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu
nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto. Watu wenye chunusi wanashauriwa kula mlo kamili wenye vyakula vyenye
madini ya zinki,nyuzinyuzi,matunda , mboga za majani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula
vya maziwa,tumbaku,sukari,vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi.
KARANGA TIBA YA KUONDOWA CHUNISI USONI.
TIBA.1
1. Karanga Zinaondoa Chunusi Usoni na kuufanya Uso kuwa Laini na kuleta uzuri wa Sura.
Chukua Karanga kijiko kimoja kidogo zisage kisha changanya na kipimo sawa cha juisi ya ndimu Au limao halafu unapaka kila siku Usoni kabla ya kulala.
TIBA.2
KUONDOA MAKOVU YA CHUNUSI.
1. Paka ‘bleach cream’ kwenye sehemu zenye makovu, cream hii husaidia kuondoa makovu.
2. Tumia ‘scrub’ ambayo huondoa ngozi ya juu (exfoliate) kwa kupaka kwenye sehemu zenye makovu kama usoni na kwingineko ambako ni rahisi kupaka. Unaweza kufanya zoezi hilo angalau mara mbili kwa wiki.
3. Tumia bidhaa ambazo zina ‘hydroxyl acids`, hutibu ngozi yako na itaonekana nyororo. Unaweza kupata hydroxyl acidstofautitofauti za ngozi (skin care products) kama vile cleansers na lotion.
4. Pia unaweza kuyafanyia masaji makovu ya chunusi ili kuvunja mafuta yaliyoganda ambayo huleta chunusi.
5. Fanya ‘diet’, unatakiwa kula vyakula vyenye vitamin na nutrition, vinasaidia kutengeneza ngozi yako kuwa na afya