Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

jaman wapendwa naomba kuuliza mwenye kujua tiba ya hii hili tatizo langu, kwenye mapaja sehemu ya hips kushuka chini kidogoo nina vijipele mfano wake kama vile vipele vinaotaga nywele zinapoota au mwili unaposisimka, nividogo mno hata kuviona na vipo sehemu kidogo tu kwenye mapaja ila natamani kujua ni kitu gani naweza kutumia ili viweze kuisha kabisa, natamani mapaja yangu yote yawe vizuri maana mbele ukiniangalia panavutia ila nyuma tu kwa juu ndo kuna tatizo! Naombeni msaada tafadhali
 
Tumia benzoyl peroxide ya kupaka pamoja na retinoin vidonge kwa siku 21.
 
JINSI YA KUONDOA CHUNUSI.jpg


Dawa ya kuondoa Chunusi kwa tiba asilia

Hii ni dawa nzuri kwa wale wote wenye Chunusi, kama utafuata maelekezo vizuri utaweza kupata matokeo mazuri.

Mahitaji

Kijiko cha chai kimoja - Juice ya Viazi mbatata

Nusu kijiko cha chai - Unga wa Lozi
robo kijiko cha chai - Manjano
Jinsi ya kutengeneza

Changanya vitu vyote pamoja kisha pakaa kwenye vipele vyeusi (usipake uso mzima kwenye vipele tu). Iache kwa muda wa nusu saa au hata unaweza kulala nayo. Pakaa kila siku kwa muda wa wiki mbili. Baadae utapaka kwa wiki mara mbili mpaka uone umeondoka weusi.

MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu

nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto. Watu wenye chunusi wanashauriwa kula mlo kamili wenye vyakula vyenye

madini ya zinki,nyuzinyuzi,matunda , mboga za majani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula

vya maziwa,tumbaku,sukari,vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi.

KARANGA TIBA YA KUONDOWA CHUNISI USONI.

TIBA.1

1. Karanga Zinaondoa Chunusi Usoni na kuufanya Uso kuwa Laini na kuleta uzuri wa Sura.

Chukua Karanga kijiko kimoja kidogo zisage kisha changanya na kipimo sawa cha juisi ya ndimu Au limao halafu unapaka kila siku Usoni kabla ya kulala.

TIBA.2

KUONDOA MAKOVU YA CHUNUSI.

1. Paka ‘bleach cream’ kwenye sehemu zenye makovu, cream hii husaidia kuondoa makovu.

2. Tumia ‘scrub’ ambayo huondoa ngozi ya juu (exfoliate) kwa kupaka kwenye sehemu zenye makovu kama usoni na kwingineko ambako ni rahisi kupaka. Unaweza kufanya zoezi hilo angalau mara mbili kwa wiki.

3. Tumia bidhaa ambazo zina ‘hydroxyl acids`, hutibu ngozi yako na itaonekana nyororo. Unaweza kupata hydroxyl acidstofautitofauti za ngozi (skin care products) kama vile cleansers na lotion.

4. Pia unaweza kuyafanyia masaji makovu ya chunusi ili kuvunja mafuta yaliyoganda ambayo huleta chunusi.

5. Fanya ‘diet’, unatakiwa kula vyakula vyenye vitamin na nutrition, vinasaidia kutengeneza ngozi yako kuwa na afya
 
samahani wadau wa jamii forum,naomba mnisaidie sana kuhusu tatizo langu hili.nimekuwa nikisumbuliwa na chunusi kwa muda mrefu sana nabado haziniachi na nimeishia kua na makovu au mabaka meusi mengi usoni kiasi kwamba sipati uhuru wa sura yangu.
muda huu nipo sehemu yenye joto na ngozi yangu ina mafuta hivyo nilishauriwa nisipake mafuta lakini bado chunusi haziniachi,kila asubuhi nakuta kuna chunusi mpya zipo usoni.
nimetumia sabuni kama zoazoa,imperial,detto na family mpaka sasa lakin hazinisaiidii,naombeni mnisaidie nitumie mbinu gani,au sabuni gani nitumie au nipake mafuta tena ya aina gani.
mimi ni mwanaume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom