Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani

Na mimi nikiri....nishafanyiwa sana pepa na wanangu wakati nikiwa zangu site mikoani naendelea na harakati za kusaka tonge....nikirudi wana nao wananeemeka , usiulize iliwezekana vipi...
 
Na mimi nikiri....nishafanyiwa sana pepa na wanangu wakati nikiwa zangu site mikoani naendelea na harakati za kusaka tonge....nikirudi wana nao wananeemeka , usiulize iliwezekana vipi...
Hahahaha na wewe uende wasafi au EFm ukataje na chuo ulichofanyiwa na ukamtaje aliyekufanyia!
 
Ni warembo lkn hawana hekima wala busara, maana hekima ni kuliweka kila jambo mahala pake,,,sasa kama hawajui walichofanya ni kosa na kama haitoshi wanajisikia sifa kuongea hadharani,basi ni wapuuzi Sana
Ni warembo lakini akili hawana maana walicho ongea kinaweza waharibia maisha
 
Ila huo ni ujasiri wa hali ya juu
 
Wajinga hao, elimu yao haijawasaidia, wameshindwa kujua ubaya wa kuongea hivyo hadharani, wenyewe wanatamka kama sifa lakini si jambo jema kwao. Labda wakaushiwe ila wakiamuliwa imekula kwako.
 
Kama siti mtemvu, wema sepetu walifoji hadi vyeti na wakakiri ili washiriki miss tz na hakuna aliyewahi kuwasumbua, wewe wadhani hawa nani atawasumbua.
 
Binadamu huwa tunapaswa tujue mipaka yetu ya kuzungumza kuzingatia hadhira tunayozungumza nayo.

Katika jaribio lao la kunogesha upacha wao wameishia kuhatarisha qualifications zao. Ukute ni uongo hawajawahi hata kufanyiana hiyo mitihani ila walitakana kuongeza vionjo tu kusahau kuwa wanasikika nchi nzima.
 
Yani hapo walipo muda huu najua wanajuta kufanya interview😂😂😂😂😂
 
Muda mwingine mdomo huponza kichwa.Hawa wakiitwa chuoni kuelezea hayo maelezo watajiteteaje?
Watasema waliongea hivyo kutafuta umaarufu 'kutrend'. Kusema tu haitoshi chuo lazima kithibitishe kuwa walifanyiana mitihani kitu ambacho ni ngumu na kitaaibisha chuo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…