KERO Chuo cha City College jijini Mwanza kinanyanyasa Wanafunzi

KERO Chuo cha City College jijini Mwanza kinanyanyasa Wanafunzi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna chuo cha afya kinaitwa City College Mwanza kinawanyanyasa sana Wanafunzi na Wazazi, Wanafunzi wanafukuzwa hovyohovyo kisa hawakamilisha michango.

Mfano chuo kimefunguliwa mwezi Novemba tarehe 23, 2025. Wanawafukuza wanafunzi wote ambao hawajakamilisha malipo ya awamu ya pili.

Sasa inakuwaje ndani ya miezi miwili mzazi au Mlezi akamilishe malipo ya awamu mbili. Mhula bado haujaisha lakini unalazimisha mzazi au mlezi alipe ada yote ya mhula michango yake. Sababu yao kubwa ni chuo hakina pesa.

Pili; Chuo kinawatoza wanafunzi elfu 60 kuwa ni malipo ya bima ya afya. Wakati bima ya afya kwa wanafunzi ni 50,400.

Tunawaomba wahusika wanafunzi wale walikuwa na nafasi sawa na wenzio waliyovyuo vingine binafsi na Serikali.

Busara kidogo zitumike kwa kuwapatia wanafunzi muda wa kuwataarifu Walezi au Wazazi wao kuwa kufikia tarehe fulani Chuo kimeagiza niwe nimelipa kiasi fulani cha fedha.

Ila hili la malipo awamu nne. Lakini unalazimisha malipo ya awamu mbili ndani ya miezi miwili au mitatu halijakaa sawa.

2026-02-10 09.20.20.jpg
 
Lipeni ada acheni kulialia bwana,kuna muda mnavionea hivi vyuo...hapo kuna walimu,miundombinu ,umeme,maji na kodi za serikali vyote vinataka pesa sasa ninyi mmekaa likizo miezi 4 hamkujua kama kuna ada? Wakati unaomba kudahiliwa hapo hamkujua gharama zao?

Na mkikosa huduma hapo mtaanza tena kulalamika utadhani wao walimu wanafundisha bure.

Hata serikali huko tuliosoma kama hujakamilisha ada hupati huduma na hapo ndo serikali sasa fikiria mtu binafsi anafanyaje?.

Mwisho jaribu kufanya biashara halafu watu wapate bidhaa kwa kukopa au bure uje usimulie hapa.
 
Na wakimbie wakalipe ada haraka sana asubuhi hii sio kutia huruma kwenye mali za wengine .

Case closed
 
Lipeni ADA kwa wakati tena nusu mhula mzima, kuna gharama za uendeshaji chuo huyo anae wafundisha analipwa, bado SAMIA anataka KODI, Acheni kutia huruma mwanafunzi ukimchekea atasoma miaka 3 bila kulipa hata 100, harafu utasikia eti nitalipa siku nikija kuchukua cheti Je ukiferi uka disco nani ale hasara
 
Back
Top Bottom