Lipeni ada acheni kulialia bwana,kuna muda mnavionea hivi vyuo...hapo kuna walimu,miundombinu ,umeme,maji na kodi za serikali vyote vinataka pesa sasa ninyi mmekaa likizo miezi 4 hamkujua kama kuna ada? Wakati unaomba kudahiliwa hapo hamkujua gharama zao?
Na mkikosa huduma hapo mtaanza tena kulalamika utadhani wao walimu wanafundisha bure.
Hata serikali huko tuliosoma kama hujakamilisha ada hupati huduma na hapo ndo serikali sasa fikiria mtu binafsi anafanyaje?.
Mwisho jaribu kufanya biashara halafu watu wapate bidhaa kwa kukopa au bure uje usimulie hapa.