Naomba kuibua suala linalohusu hali ya Hosteli za Dar es Salaam Institute of Technology (DIT), ambalo linaibua maswali kuhusu ubora wa mazingira ya makazi yanayotolewa kwa Wanafunzi.
Inasikitisha kuona kwamba hosteli inaweza kuwepo, lakini mazingira yake yakawa hayaridhishi. Kuwepo kwa jengo la hosteli pekee hakumaanishi mahitaji ya msingi ya Wanafunzi yametimizwa, inapaswa kuwa sehemu salama, safi, yenye mazingira yanayofaa kwa Mwanafunzi kuishi na kujiandaa kwa masomo yake.
Wanafunzi wanaenda vyuoni kutafuta elimu na kujenga maisha yao ya baadaye. Hivyo, mazingira wanayoishi yanapaswa kuwasaidia kufikia malengo hayo, si kuwa chanzo cha usumbufu na changamoto zinazoweza kuepukika.
Swali la msingi ni hili: Je, ubora wa mazingira ya hosteli unazingatiwa kwa kiwango gani, na ni nani anayewajibika kuhakikisha kwamba makazi ya Wanafunzi yanakidhi viwango vinavyostahili?
Pia soma ~ HOSTEL ZA CHUO CHA DIT