Chuo cha Excellent ni cha ovyo sana. Vijana mnaotaka kusoma Clinical Medicine hapo, msiende

Chuo cha Excellent ni cha ovyo sana. Vijana mnaotaka kusoma Clinical Medicine hapo, msiende

Sina mood

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
248
Reaction score
1,442
Hiki chuo cha excellent kwanza hata usipo-apply unashangaa umetumiwa meseji kwamba umechaguliwa hapo wakati hata ku-apply huku apply.

Hiki chuo ukiingia kusoma hakuna kuhama ukiomba uhamisho kwanza wanakukatalia kisha wanakufutia usajili kwamba hawakutambui hivyo unaanza upya kabisa

Ufundishaji ni mbovu na 99% ya walimu wanaofundisha hicho chuo ni walimu wa diploma tu hawana elimu ya MD

Kipindi cha rotation wanafunzi wanafanyiwa ubabaifu kupelekwa wodini wakati huo pesa wameshalipa
 
Ukiwa kama msomi unatakiwa kuandika mapungufu yao wapelekee wanaohusika na mambo ya vyuo vikuu kwenye usimamizi harafu watayafanyia kazi kitaalamu zaidi na isionekane ni mambo yenu ya kuua biashara...
 
Ukiapply vyuo vitatu ikiwemo hiyo Excellent vingine vyote utaweza kosa nafasi ila Excellent haijawahi kataa mtu 😊😊😊
 
Tatizo la sa hv Kwa Tz , elimu ni biashara, so hata ukifeli kama we ni mlipaji mzuri wa tuition fee, wanakufanyia manyanga uonekane umefaulu ili waendelee kubarikiwa na fedha zako
 
Hiki chuo cha excellent kwanza hata usipo apply unashangaa umetumiwa meseji kwamba umechaguliwa hapo wakati hata ku apply huku apply.

Hiki chuo ukiingia kusoma hakuna kuhama ukiomba uhamisho kwanza wanakukatalia kisha wanakufutia usajili kwamba hawakutambui hivyo unaanza upya kabisa

Ufundishaji ni mbovu na 99% ya walimu wanaofundisha hicho chuo ni walimu wa diploma tu hawana elimu ya MD

Kipindi cha rotation wanafunzi wanafanyiwa ubabaifu kupelekwa wodini wakati huo pesa wameshalipa
Usikute hulipi ada afu unalalamika huku.
 
Usikute hulipi ada afu unalalamika huku.
Hivi vyuo ukiwa unatoa ada kwa kusua sua utavichukia sana,kwenye ada wako very serious sana.

Lakini anayoyasema ni sahihi kwa asilimia kubwa,vyuo vingi vilivyoota kama uyoga kuna walimu wenye diploma
 
Serikali iliwezaje kutoa usajili hali ya kuwa hawakufata taratibu zote hapo mm lawama kwa serikali tu hakuna mwingine wa kumlaumu mwisho wa siku mgonjwa anafanyiwa operesheni matakoni badala ya mguuni
 
Kuna hawa wanaitwa nacte ni hatari sana kwa ustawi wa taifa kwani kuna vyuo hali Dar vinatoa rushwa sana
 
Tatizo la sa hv Kwa Tz , elimu ni biashara, so hata ukifeli kama we ni mlipaji mzuri wa tuition fee, wanakufanyia manyanga uonekane umefaulu ili waendelee kubarikiwa na fedha zako
Elimu ni biashara dunia nzima.

Ulaya vyuo vinalalamikiwa kwamba vinatoa scholarship kisha ukishasajiliwa unawekewa target ya juu mno kufikia ili uendelee kubaki kwenye scholarship.

Wengi hushindwa na kujikuta kuanzia mwaka wa pili wanaanza kulipa ada. Hii mbinu inakupa wanafunzi mfano 100, katika 100 waweza kuta 90 wasifikie marks katika hao 90, 70 wataendelea na wewe, next year hao 10 kuna watakaoteleza tu.
 
Asante kwa taarifa..ila hivi vyuo vya binafsi vingi ni vyakitapeli sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hivi vyuo vya CO vimekuwa vingi sana serikali iliangalie hili maana hao baadae ndio wanakuja kututibu huku mtaani watatuua jamani.
 
Back
Top Bottom