KERO Chuo cha Sayansi ya Afya KAM college Kimara Korogwe Dar, es Salaam kinanyanyasa wafanyakazi wake

KERO Chuo cha Sayansi ya Afya KAM college Kimara Korogwe Dar, es Salaam kinanyanyasa wafanyakazi wake

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mmiliki wa chuo anawadharau waalimu na kutukana waalimu mbele ya wanafunzi jambo ambalo linapelekea waalimu kukosa sauti kwa wanafunzi.

Mmiliki amegoma kulipa mishahara ya watumishi kwa mwezi wa July akidai hajafurahishwa na utendaji kazi japo yeye hakuwepo chuoni maana alisafiri.

Jambo lingine ni kuwa wanafunzi wanahakikishiwa kuwa watafaulu hata kama hawatosoma jambo linalosababisha wanafunzi kutokuwa watiifu na wafuatiliaji. Kila anayetaka kupaza sauti yake kuwatetea waalimu hao anaambiwa ni bora aache kazi.

Pia ukifika mwisho wa mwezi ukikaribia anaanza vitisho na anafukuza waalimu wake ili asiwalipe mishahara yao tunaomba wizara ya afya ifuatilie hili maana wanafunzi wengi wanatoka pale hawana ujuzi kabisa.
 
Hivi vyuo vya uchochoroni vifungiwe yaani hapo KAM miaka nenda rudi stori zile zile na wanafunzi wengi hapo hakuna kitu ,kuna watu wana miaka hadi 8 wanasoma diploma 😁 msiba sana huu.

Ndugu mwalimu pole sana but ukisoma afya ujue ni stress kwenda mbele popote pale utakapowekwa ni fujo.
 
Back
Top Bottom