KERO Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka tangu tulipe fedha ya bima mwaka 2023 hadi mwaka huu tunamaliza hatujapata bima

KERO Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka tangu tulipe fedha ya bima mwaka 2023 hadi mwaka huu tunamaliza hatujapata bima

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mhitimu wa Diploma katika chuo cha Ukutubi na Uhifadhi nyaraka School of Library and Documentation Studies (SLADS) kilichopo Dar es Salaam, chini ya Maktaba ya Taifa.

Tangu tulipoanza masomo ya Certificate mwaka 2023, tulilipa fedha kwa ajili ya bima ya afya, lakini hadi leo, tunapomaliza masomo, hatujapewa bima hiyo.

Tunapoulizia kuhusu fedha zetu ambazo ni Shilingi 50,400 kwa kila mwanafunzi, tumekuwa tukizungushwa bila kupewa majibu ya kueleweka, hadi tumemaliza masomo.

Tunaomba wahusika watueleze fedha hizo zilipelekwa wapi na kwa nini hadi tunamaliza masomo hatujapewa bima ya afya wala kurejeshewa fedha zetu?
 
Back
Top Bottom