Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kina mchango gani katika kusaidia kupunguza ajali nchini?

Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kina mchango gani katika kusaidia kupunguza ajali nchini?

Alluu

Senior Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
127
Reaction score
142
Nimeangalia hali ya usalama wa abiria katika vyombo usafiri wa umma kwa maana mabasi na wale ambao tunatumia vyombo binafsi na wadau wengine wanaotumia barabara nchini, ni kwamba kumekuwa na wimbi kubwa la ajali katika kipindi hiki kifupi cha Januari hadi March hii 2022.

Ukiangalia vyanzo vya ajali hizi kwa maana moja au nyingine unaweza kusema malori ya mizigo na mabasi ya abiria yamechangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ajali hizi, ambazo zimeleta madhara makubwa yakiwemo vifo, majeruhi na uharibifu wa vyombo vya usafiri na miundombinu iliyohusika na hata sehemu nyingine nyumba za wananchi ambazo zimehusishwa katika baadhi ya ajali hizi.

Sasa hoja ya msingi hapa ni kuwa tunacho chuo cha NIT, je kimetoa mchango gani hadi sasa kusaidia kupunguza ajali nchini?

Kwa baadhi ya nchi zilizoendelea, unaweza kuona kuwa ajali zinapotokea kunakuwa na uchunguzi wa kitaalamu (Ukiacha huu wa Vyombo vya Usalama kama Traffic Police n.k) na matokeo yake kufanyiwa kazi ilikuzuia au kupunguza kutokea kwa ajali ambazo chanzo chake kimefanyiwa uchunguzi na taarifa hizi kuwekwa public/wazi kwa jamii ili kujifunza kutokana na ajali hizi kwa lengo la kupunguza kutokea kwa ajali kutokana na elimu na marekebisho kadhaa kama ni sheria au usimamizi wa sheria.

Naomba maoni yenu na je tunawezavipi kuhakikisha ajali hizi zinapungua ili kuokoa maisha ya Watanzania wasio na hatia ambao wanafariki na kupata vilema kutokana na madhara ya ajali hizi?
 
Acha watu waendelee kula per Diem. Ajali kawaulize bodaboda
 
Back
Top Bottom