Chuo Kikuu cha Biashara (CBE) chamtunuku David Kafulila ngao ya heshima kwa kusimamia ukuzwaji wa sera za Uchumi Jumuishi nchini

Safi
 
Vyuo huwa vinatoa digrii za heshima hayo ya ngao Chuo kutoa ndio nayasikia leo

Ngao mara nyingi hutolewa na machifu kwa mhusika

CBE wameanza kutoa ngao kama chuo?
Ipo siku kitatoa kombe la mbuzi
 
Zile Blocks E, F na G unazifahamu vema?

CBE ASA club je?

Elimu Kiganjani Mabweni ni mambo ya Ujima ya akina Mabibo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mabweni yanajengwa wapi, Mwanza, Dodoma au Dar kote huko kuna CBE
 
Kafulila asisitize Serikali iuze Shirika la ndege (ATCL), asisitize wawekezaji binafsi katika umeme kuondoa monopoly ya TANESCO
ChoiceVariable
TANESCO kutafutiwa washindani wengine nakubaliana na wewe, ATCL kubinafsishwa haiwezekani.

Kila taifa duniani linakuwa national carrier yake binafsi, shirika la ndege lenye kumilikiwa na taifa.
 
Vikiitwa vya jalalani wanahamaki, unatoaje tuzo kwa proposal? Mradi ukiyeyuka kama kawaida ya wabongo unarudi kumnyan'ganya?
 
Nishati ndio inaweza kupokea wawekezaji wengi bila ya tatizo kuja kutokea mbele ya safari. Kila serikali makini inamiliki shirika lake binafsi la ndege.

Wanaita national carrier, lazima iwepo. Mwalimu Nyerere alipofariki 1999 alifuatwa na ndege ya ATC iliyoongozwa na RIP Mazula kule Uingereza, ingekuwa ni aibu kwa serikali kukodisha ndege ya Precision kuufuata mwili wa Nyerere.

Yapo mengi yanayofanywa na ndege inayomilikiwa na serikali, linapokuwepo shirika lenye kumilikiwa na serikali inakuwa ni heshima kwa nchi.
 
Kajitahidi kufanya nini au mnaridhika na maneno tu, katika yote aliyowahi kusema ni mradi upi umezinduliwa au kukamilika?
Najitahidi namna ya kukujibu ,ila nashindwa hata nimsaidie wapi huyu tumbili wa werema...hamna kitu pale.
 
Karne hii mnajenga Hostel?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Wanazidi ku-diviate kwenye jukumu la msingi badala ya kuongeza majengo waongeze vitivo waweze kupata kipato zaidi hostels achia sekta binafsi huko wawekeze kumaintain hostels ni gharama zaidi ya madarasa
 
Hata TTCL ni majanga sana, haya ndiyo maeneo ayatupie macho sasa ili kuleta ufanisi na tija
Anahangaika na petty issues asikike wakati shirika kama ttcl liko/lilikuwa kwenye uwezo wa kufanya biashara ya data/ Internet na kupata faida mara dufu kabla hata ya makampuni mengine hayaweka mkazo huko
 
Kafulila ni mtu mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…