Chuo Kikuu cha Biashara (CBE) chamtunuku David Kafulila ngao ya heshima kwa kusimamia ukuzwaji wa sera za Uchumi Jumuishi nchini

Chuo Kikuu cha Biashara (CBE) chamtunuku David Kafulila ngao ya heshima kwa kusimamia ukuzwaji wa sera za Uchumi Jumuishi nchini

Mheshimiwa David Kafulila aingie Bungeni hapo Mwakani panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu.
 
View attachment 3101816

Chuo kikuu Cha Usimamizi wa Fedha na Biashara Cha CBE nchi Tanzania kimemtunuku Mhe David Kafulila ngao ya heshima kwa uchapakazi wake uliotukuka kwa Taifa.

Mkuu wa Chuo hicho Prof Edna Luoga asema Chuo hicho kimeamua kutoa ngao hiyo ya kutambua juhudi za Kafulila katika kumpata mwekezaji atakayejenga mabweni katika Chuo hicho yatakayoweza kuchukua wanafunzi elfu 12 kwa mara moja kwa sharti la Ubia ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi kuishi mbali na eneo la Chuo hicho jambo ambalo hupunguza ari na nguvu za Masomo kwa wanafunzi hao.

David Kafulila ambae ni Mkurugenzi mkuu wa Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi Tanzania PPP amekuwa akisistiza lazima ifike mahali ambapo Serikali ipunguziwe mzigo katika Utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa miradi yenye sura ya kibiashara ili kuifanya Serikali itekeleze baadhi ya miradi yake ya maendeleo nje ya bajeti yake ( Outside the government balance sheet)
Prof namjua, ni mtu makini, kwao Morogoro, na baba yake alikuwa prof, ila ngao hutolewa kwenye mechi za ngao ya hisani, kwa nini huyu muha sijui mrundi anahangaika kujipromote mitandaoni?
 
Bweni la wanafunzi 12?
Hilo ndio limemfanya atunikiwe??
Kuna huyo tajiri hapo akigawa "lim paper"

Kuna nyakati naona kabisa mfumo wa elimu wa kikoloni ulikuwa ni bora kuliko huu unaotumika sasa.

Maana hata vijana wengi kuunda sentensi moja ya kiingereza iliyokamilika hawawezi.
IMG_20240920_134352.jpg
 
Kafulila asisitize Serikali iuze Shirika la ndege (ATCL), asisitize wawekezaji binafsi katika umeme kuondoa monopoly ya TANESCO
ChoiceVariable
Kwa nini Serikali iuze ATCL? Hao wawekezaji Binafsi si wanzishe shirika lao, kama ilivyo Precision? Ethiopian Mpaka leo linamilikiwa na Serikali, na linafanya vizuri. KQ Serikali imeongeza %age ya umiliki....Usafiri wa anga ni strategic area kwa serikali kuumiliki, sio kuachia watu binafsi kama walivyoachiwa ATC kwa wale SAA wakati ule - si uliona kilichtokea?
 
Uko sahihi kabisa, ATCL iendeshwe kwa ubia
Hakuna haja ....wawekwe tu right people to the right positions....Emirates mpaka leo hawana mbia...na linafanya vizuri..Tusikariri jamani...Wapo watu wenye uwezo, hata ikibidi tuwaajiri kutoka nje - na kupewa malengo, kama sisi hatuna uwezo
 
View attachment 3101816

Chuo kikuu Cha Usimamizi wa Fedha na Biashara Cha CBE nchi Tanzania kimemtunuku Mhe David Kafulila ngao ya heshima kwa uchapakazi wake uliotukuka kwa Taifa.

Mkuu wa Chuo hicho Prof Edna Luoga asema Chuo hicho kimeamua kutoa ngao hiyo ya kutambua juhudi za Kafulila katika kumpata mwekezaji atakayejenga mabweni katika Chuo hicho yatakayoweza kuchukua wanafunzi elfu 12 kwa mara moja kwa sharti la Ubia ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi kuishi mbali na eneo la Chuo hicho jambo ambalo hupunguza ari na nguvu za Masomo kwa wanafunzi hao.

David Kafulila ambae ni Mkurugenzi mkuu wa Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi Tanzania PPP amekuwa akisistiza lazima ifike mahali ambapo Serikali ipunguziwe mzigo katika Utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa miradi yenye sura ya kibiashara ili kuifanya Serikali itekeleze baadhi ya miradi yake ya maendeleo nje ya bajeti yake ( Outside the government balance sheet)
Safi sana CBE
 
Back
Top Bottom