Chuo kikuu Cha Dar es Salaam kimpe Rais Samia Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa

Heshima toka chuo kikuu cha Daresalam ina hadhi gani?
 
Ni kweli maana ni chuo cha mchongo hivyo hata wakimpa ni sawa tu.
Ila ndugu yangu Tindo nakwambia kuwa ipo siku Kama Mwenyezi Mungu anatujaria uhai utakuja uje hapa jukwaani kuomba mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Arudi kutuongoza hata Kama atakuwa amesha staafu utumishi wake kwetu watanzania Kama Rais wa nchi,

watu aina ya mama Samia wenye moyo wa upendo kwa watu wake huwa Hawazaliwi kila siku hapa Duniani, Mama Samia no zawadi kwetu watanzania, Najuwa wengine hamuioni thamani yake kwa kuwa tupo Naye na munaona Ni Haki yenu kwa kila kitu akifanyacho na kwamba hastahili kupongezwa, siku itafika mtayakimbia maneno yenu wenyewe
 
Sisi tunataka katiba bora sio mtu. Sifa zetu tunapeleka kwenye katiba na sio mtu. Kama katiba bora imemshinda, msifie ww unayepata ugali kwa huruma yake.
 
Kutambua mchango wake mh Rais wetu kiuongozi katika kulitumikia Taifa letu
Tunavyo vyuo vikuu zaidi ya 10 ikiwemo Mzumbe tunakoambiwa alisomea; why single out UD?

Kwanini hiyo digrii asipewe na chuo alichosomea?!
 
Sisi tunataka katiba bora sio mtu. Sifa zetu tunapeleka kwenye katiba na sio mtu. Kama katiba bora imemshinda, msifie ww unayepata ugali kwa huruma yake.
Kenya hapo mnawasifia kuwa Wana katiba Bora na Ni hapo hapo kenya ambapo Odinga analia Lia kuwa haki haijatendeka, Katiba itasimamiwa na watu, Hivyo hata katiba iwe Bora lakini Kama hakuna utashi wa watu kuiheshimu na kuifuata Basi itakuwa Ni kazi bure, Tumuunge mkono Rais wetu kwa kuendesha nchi yetu kwa kufuata misingi ya Sheria na utawala bora
 
Hatuangalii nani analia, tunaangalia mchakato mzima ulivyokuwa. Raila alipata hadi nafasi ya kudhibitisha madai yake kwenye mahakama huru na akashindwa. Matokeo na mwenendo wa uchaguzi wa Kenya ulikuwa bora mara elfu ya huu wetu.
 
Kwani udaktari wa heshima una nini. Hii tabia ya vyuo kugawa digrii za udaktari wa heshima kama njugu imechangia pia kudidimiza heshima na ubora wa vyuo, kwa mfano UDOM imekuwa ni digrii mill kubwa Tanzania
 
Walioanzisha mfumo huo wa kutambua michango ya watu katika maeneo tofauti tofauti siyo wajinga
 
Unafikiri hata ninyi hapa mtaacha kulia Lia?
Hatuangalii nani analia, tunaangalia mchakato mzima ulivyokuwa. Raila alipata hadi nafasi ya kudhibitisha madai yake kwenye mahakama huru na akashindwa. Matokeo na mwenendo wa uchaguzi wa Kenya ulikuwa bora mara elfu ya huu wetu.
 
Walioanzisha mfumo huo wa kutambua michango ya watu katika maeneo tofauti tofauti siyo wajinga
Huo mfumo wa kutoa digrii za honoris causa haufanyi kazi yake hivyo unavyotaka wewe. Mimi niko kwenye kamati ya kutafuta, kutathmini na kupendekeza honoree wa chuo chetu ambaye hupata heshima hiyo ya honoris kwa kila semester. Hizo hazitolewi kwa vigezo vidogo kama unavyotaja hapo.
 
Siyo kila kitu cha kuchangia, mengine yapite tu
 
Tume siyo inayochagua Bali kazi yake Ni kumtamgaza mshindi, Sasa nyie mnazani mtatangazwa na Nani kuwa Ni washindi wakati wananchi walishawapuuza baada ya kuwa mmekosa Sera ajenda na hoja zenye ushawishii kwa wananchi wanyonge, Hamuwezi mkapata kura kutoka kwa watanzania wa Sasa,
Hatulii kama maigizo bali vilio vya haki, ndio maana tunahitaji katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kama hutaona CCM ndio wanalia.
 
Kwa taarifa yako siku tume itakuwa huru baada ya machafuko, ndio utajua kuwa CCM sio chama cha kizazi hiki. Hizo porojo za sera kawapeni wale mifugo mnaowabeba kwenye malori na kuishia kuwalisha propaganda mfu. Ukiona chama kinategemea vyombo vya dola, na tume isiyo huru ya uchaguzi kukaa madarakani kwa shuruti, basi ujue kimefikia mwisho wa uwezo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…