Chuo kikuu Cha Dar es Salaam kimpe Rais Samia Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa

Chuo kikuu Cha Dar es Salaam kimpe Rais Samia Udaktari wa Heshima katika uongozi na mahusiano ya kimataifa

Hatimaye maneno na maombi yangu yametimia japo naamini Ni kwa utashi wa chuo na uongozi wa chuo na siyo kwamba Ni kwa ushauri wangu maana naamini Rais Samia alistahili kupewa heshima hii
 
Nitaanzisha kampeni rasmi mama kupewa hicho unacholiita PhD kama atafanikisha upatikanaji wa katiba mpya tu na sio vinginevyo!!

Wenye akili wanaandika hivi;-

"Mzee Warioba ajumuishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchakato wa katiba mpya ukamilike"
Tayari kashapewa Leo hii. Mungu Ni mwema
 
Ww utakuwa ni mzee lazima, wazee ndio mlilishwa huo utapeli uitwao sera. Kama mngekuwa na sera hii nchi ingekuwa masikini hivi? Mawakala hao ambao wakurugenzi wanagoma kuwaapisha? Narudia tena, uchaguzi na sera ziko hapo Kenya, hapa kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Napenda kukutaarifu kuwa Chuo kikuu Cha Dar es salaam kimetambua mchango wa mh Rais na kumtunuku Udaktari wa heshima
 
Wewe aliyekuroga ana roho mbaya sana ! yaani kaondoka na ubongo wote kakuachia frem tu .
Udsm imetambua mchango wa mh Rais kwa Taifa letu na kumpa heshima hii ambayo nilipendekeza. Wewe Ni Nani upinge chuo kikubwa Kama Udsm? Nenda kalime kyela huko nitakuja unipe Mchele kidogo nami nitakupa karanga za kwetu
 
Aisee...
Utakuwa ulifata huu ushauri na kujichukulia..

3.Bachela ya Chawa with Uking'asti
8.Bachelor of Postology

Kashapewa Tayari,
 
Hatimaye maneno na maombi yangu yametimia japo naamini Ni kwa utashi wa chuo na uongozi wa chuo na siyo kwamba Ni kwa ushauri wangu maana naamini Rais Samia alistahili kupewa heshima hii
And so maisha yako sasa yatakuwa malaini kama maini!.
Hakuna kukatika katika umeme, maji, mfumuko wa bei nk nk
 
Napenda kukutaarifu kuwa Chuo kikuu Cha Dar es salaam kimetambua mchango wa mh Rais na kumtunuku Udaktari wa heshima

Yaani chuo kikuu cha Daresalam nayo ni mjadala wakimpa rais wa nchi heshima ya udaktari, hicho si cheo anaamua tu na kupewa hapo hapo? Angepewa na Havard University wangalau ingekuwa mjadala.
 
Ndugu zangu hayo Ni mapendekezo yangu binafsi baada ya kuwa nimekaa kwa muda mrefu nikifuatilia utendaji kazi wa mh Rais Samia na kufikiria namna mh Rais wetu mpendwa alivyoipokea na kukabidhiwa nchi yetu Katikati ya wingu zito la majonzi na simanzi kubwa ya kuondokewa na Rais wetu Hayati Daktari John Pombe Magufuli

Ndugu zangu ilikuwa Ni mshituko mkubwa Sana kwetu watanzania kuondokewa na Rais aliyepo madarakani, kwani hakuna aliyekuwa akiwaza Wala kufikiria Wala kuota Kama Jambo lile linaweza kutokea, maana kwetu watanzania lilikuwa Ni Jambo geni sana ambalo halijawahi kutokea,

Hapa shukurani zangu za kipekeee kabisa lazima liviendee vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vilivyohakikisha kuwa mipaka yetu na nchi yetu inaendelea kuwa salama kabisa, lakini pia Namshukuru mwenyezi Mungu ambaye siku zote amekuwa nasi watanzania kwa kutuvusha salama salmini katika kipindi kigumu, lakini pia nawashukuru viongozi wetu wastaafu na hata waliopoo madarakani waliohakikisha nchi inakuwa na utulivu na wanatuongoza watanzania kuvuka salama katika bonde lile la uvuli, Asante pia kwa watanzania kwa namna ambavyo tulibaki watulivu na kuungana Kama Taifa mpaka mwisho wa kuhitimisha safari yake Hayati Magufuli katika nyumba yake ya Milele kule CHATO

Ndugu zangu macho yetu watanzania ndani na nje ya mipaka yetu yakaelekezwa kwa Mama huyu shupavu, mwenye moyo wa huruma upendo na unyenyekevu ulio jaa hekima busara Subira na Aliyejaa hofu ya Mungu, mwenye upendo wa kweli kwa watu na mzalendo wa dhati kwa nchi yetu, msikivu na mwenye kumaanisha kile akitamkacho, mwenye kuchuja maneno na kuchunga ulimi wake

Mh Rais wetu mpendwa Taratibu akaanza kufufua na kuinua matumaini ya watanzania ambayo wakati huo Tulikuwa Tumetoka kwenye majonzi na mshituko, akaanza kuwa mfariji wetu, Akaanza kutufuta machozi, Akaanza kutushika mikono kutunyanyua tulipo kaa ili tuanze safari ya Kuendelea kazi ya kuijenga nchi yetu kwa kauli yake ya kazi iendelee, Akaanza kutuunganisha watanzania kukabili maadui wetu wa ujinga umasikini maradhi Rushwa na ufisadi

Kuna watu walikuwa wamekata Tamaa, Kuna watu walikuwa wanatamani hata kuona kila baya linaipata Tanzania, lakini mama huyu Hodari akazizima roho hizo chafu na kupanda mbegu za upendo na uzalendo katika mioyo watanzania, Ndio maana unaona Leo hii Taifa Ni moja likisonga kwa pamoja,

Hivyo ndugu zangu kwa kuyawaza hayo Nikaona kuwa Ili kuonyesha kutambua mchango wa Rais huyu Hodari haina budi kwa Chuo Kama UDSM kumpa Udaktari wa Heshima mh Rais wetu mpendwa katika uongozi na mahusiano ya kimataifa, sote Ni mashahidi namna mh Rais wetu alivyoliongoza vyema Taifa letu kutoka katika kipindi hicho na namna maendeleo mbalimbali yalivyopatikana, kwani Tumeona namna miradi mingi ilivyojengwa na hata kuendeleze Ile iliyokuwa imeanza kujengwa

Tumeona namna alivyojenga umoja wa kitaifa na mshikamano wa watanzania, Tumeona namna nchi yetu ilivyopata mafuriko ya watalii pamoja na wawekezaji baada ya kuimarisha diplomasia yetu, Tumeona namna alivyoimarisha demokrasia na mahusiano mema na vyama vya upinzani kwa kuwachukulia wapinzani Kama wadau wa maendeleo na kuamini kuwa tunaweza tukatofautiana lakini bado tukaijenga nchi yetu kwa pamoja na tukajivunia mafanikio yetu kwa pamoja

Ni vyema atunukiwe na kupewa heshima hiyo ili Kuendelea kumpa faraja ya kusonga mbele zaidi na kuliinua Taifa hili kiuchumi, Nimependekeza UDSM maana najuwa ndio chuo kikongwe hapa nchini ambacho huwezi ukakiweka kando katika maendeleo tuliyoyafikia Leo hii kupitia wasomi wake waliopita na kupikwa pale,

Niseme tu ukweli Mimi LUCAS Mwashambwa Kama kijana nimetokea kuvutiwa na kuridhishwa Sana na uongozi wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani, Ni Imani yangu kuwa ombi hili litapokelewa na kutafakariwa vyema, Apewe tu maana Anastahili kupewa, Ametutoa pagumu Sana watanzania mpaka kufika hapa tulipo, maana amepokea nchi kipindi Cha mdororo wa uchumi Duniani

Kazi iendeleee, Mh Rais Samia Ndiye Joshua wetu atakayetufikisha Kanaan, Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka na wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
Hongera zake Dr Samia 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221130-131150.png
    Screenshot_20221130-131150.png
    168.5 KB · Views: 1
  • Screenshot_20221130-131127.png
    Screenshot_20221130-131127.png
    233.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom