Chuo Kikuu cha Dar es salaam kitafute mwekezaji awasaidie kuprinti vyeti vya wahitimu

Chuo Kikuu cha Dar es salaam kitafute mwekezaji awasaidie kuprinti vyeti vya wahitimu

Nchi yetu kila kitu kinahitaji ubinafsishaji; mfano mdogo sana na chuo kikongwe cha Dar es salaam. Mwezi wa pili tuliona wanafunzi wakilalamika hadi kutaka kuandamana ndipo wakatoa vyeti. Leo tena kampuni yetu inafanyisha usahili wanafunzi wa UDSM wanakuja na matokeo. Ukiuliza wanakujibu wameambia vyeti haviwezi kuprintiwa mpaka miezi mitatu hadi mitano toka wamalize chuo.

Waziri wa elimu na viongozi wa chuo hiki kikongwe tatizo lipo wapi? Technology imekuwa sana sasa hivi; mnashindwa nini kuandaa vyeti kama vyuo vingine duniani? Kweli taifa linahitaji miezi mitatu hadi minne kuchapisha cheti?

Au labda ninyi mliosoma hiki chuo mtuambie vyeti vyenu vinaugumu gani kuprinti?

We need reform in our education sector; hawa watu wasioweza kuprinti vyeti kwa wakati unadhani wakipewa taasisi kubwa inayosimamia sekta binafsi wataweza kuendesha? Yawezekana hata sekta nyingine zinabinafsishwa kwa sababu viongozi wasomi awajaelimika......1990 tulikuwa tunasubiri vyeti miezi miwili leo 2023 watu wanakaa siku mia plus
Si wanasemaga vinakuwa printed nje ya nchi? Ila hapana asee... Ubora ni hafifu sana!
 
Chuo cha hovyo hicho. Kinazidiwa TEKU mara 1000 mbali ya kuwa ni chuo chenye CV kubwa, chuo gani kimetuzalishia mafisadi wakubwa ambao hawana mchango wowote kwa WATANZANIA, chuo ambacho hata leo kinazidi kushamirisha CCM Badala ya kushughulika na uhalisia wa maisha. Umaskini walionao Watanzania kwa karne hii umechochewa na chuo hicho.
 
Kuna tatizo kubwa la paperwork.na data entry katika vyuo vingi ikiwemo udsm, cbe, mambo ndio yaleyale ya kuchelewa kupata vyeti as if cheti ni kitu hakitengenezeki haraka
 
Back
Top Bottom