Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kitamtunuku Rais wa Tanzania, John Magufuli Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa kutokana na uongozi wake hasa ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Akizungumza leo Jumatano Novemba 20, 2019 Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee amesema shahada hiyo itatolewa kesho katika mahafali ya 10 ya chuo hicho.
“Shahada hii itatolewa kwa Rais kwa uongozi wake uliotukuka hususan katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuwekeza katika elimu, miundombinu, mawasiliano, nishati, utalii na kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa," amesema.
Amesema mwaka 2010 shahada hiyo ilitolewa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Rashid Kawawa (marehemu).
Profesa Bee amesema wahitimu 6,488 watatunukiwa Astashahada, Shahada, Stashahada ya juu, Shahada ya Umahiri, na Shahada ya Uzamivu.