A
Anonymous
Guest
Nilihitimu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Mwaka 2025 katika Shahada ya Bachelor of Science in Telecommunication Engineering, kero yangu ni kuhusu fedha za overpayment ambazo tulipaswa kurejeshewa baada ya kumaliza masomo.
Baada ya kuhitimu, wahitimu tuliandika barua za kuomba kurejeshewa fedha hizo. Kwa upande wangu, kiasi ninachodai ni takribani Sh milioni 2.7. Barua yetu ilipitia kwa Mhasibu wa College na baadaye ikaenda kwenye Utawala Mkuu kupitia Masijala kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Tatizo ni kwamba hadi sasa, licha ya mwaka mwingine wa masomo kuanza, bado hakuna fedha ambazo tumerudishiwa. Kila tunapofuatilia tunaambiwa tu kwamba “file lako bado”, lakini hatupewi maelezo ya wazi kuhusu lini fedha hizo zitalipwa au mchakato umefikia hatua gani.
Kinachotuumiza ni kwamba fedha hizo tulizilipa wakati wa masomo na tulitarajia kwamba baada ya kubainika kuwa ni overpayment, zingerudishwa kwetu kwa wakati. Sasa tupo mtaani baada ya kuhitimu, na kwa kweli fedha hizo zingetusaidia sana katika kuanza maisha na kukabiliana na changamoto tulizonazo baada ya kumaliza chuo.
Sio mimi pekee ninayekabiliwa na changamoto hii. Wapo wahitimu wengine tulioandika maombi ya kurejeshewa fedha hizo, lakini hadi sasa hakuna hata mmoja ambaye amerejeshewa. Tunaomba chuo na mamlaka husika zilifuatilie suala hili na zitupatie majibu ya wazi kuhusu fedha zetu.
Taarifa ya Chuo ~