KERO Chuo Kikuu cha SAUT boresheni ukumbi uendane na idadi ya Wanafunzi, tunajazana sana Ukumbini

KERO Chuo Kikuu cha SAUT boresheni ukumbi uendane na idadi ya Wanafunzi, tunajazana sana Ukumbini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
saut.jpg

Hiki unachokiona kwenye picha hapo siyo kwamba watu wapo kwenye shoo ya muziki, hapo ni Ukumbini katika Chuo Kikuu cha SAUT au Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino Tanzania (St. Augustine University of Tanzania - SAUT MAIN CAMPUS).

Wanafunzi tumejaa katika Ukumbi wa chuo kiasi kwamba wengine wamesimama, tupo hapo kwa ajili ya masomo na sio jambo la 'fun', hivi hapo kitaeleweka kitu kweli darasani?

Hii ni taasisi kubwa kielimu na kwa sifa, hiki kinachoendelea, sio sawa, mazingira yanatakiwa kuboreshwa na kuwa ya kisasa ili yaendane na hadhi ya chuo.

Pia soma ~ Canteen za Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT ) Mwanza zimechakaa, hazifai kwa matumizi
 
Back
Top Bottom