Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, umetaka wanafunzi zaidi ya 2000 kurudia mtihani ingawa walishafanya mtihani huo wa semister ya 2.Chanzo ni kutolipa ada ya kufanya mtihani, hii sio haki.
Uongozi umeshindwaje kutambua toka kipindi chote hadi wamefanya mtihani na matokeo yameshatoka. Na istoshe, wazazi watatoa wapi kiasi cha pesa cha ada, maana mtihani ni tarehe 23 mwezi huu na wanafunzi wapo likizo.
Mifumo ya vyuo na wanafunzi wamefanya mtihani kwa sababu ya mifumo yao mibovu hadi mtu anapata namba ya kufanya mtihani. Je, Jamii Forums nani wa kumlaumu?
Wasaidieni wadau, hali sio nzuri na hii sio haki.