Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT) Chatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi wake dhidi ya COVID19 NA COVID21

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT) Chatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi wake dhidi ya COVID19 NA COVID21

Corona: Wizara ya Elimu yaukana waraka wa Prof. Elifas Tozo Bisanda Makamu wa Chuo Kikuu Huria (OUT)
 
Sasa naona Taifa limeanza kuamka.

Baada ya viongozi wa kanisa kuonyesha njia kwa kukataa Jina la Mungu lisitumike kisiasa kwa watu kukwepa uwajibikaji kwenye issue ya Korona. Wasomi wetu nao sasa wameanza kuvunja ukimya juu ya suala la korona kwa kuzitaka jumuia zao zichukue tahadhari..
Corona: Wizara ya Elimu yaukana waraka wa Prof. Elifas Tozo Bisanda Makamu wa Chuo Kikuu Huria (OUT)
 
Ni vema kuchukua tahadhari dhidi ya Deportivo kweli anaua Sana

Vaa barakoa , osha mikono kwa maji tiririka, zingatia umbali social distance
 
THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA

OFFICE OF THE VICE CHANCELLOR

P.O. Box 23409 Tel: 255-22-2668992/2668445 Dar es Salaam, Tanzania Fax: 255-22-2668759

http://www.out.ac.tz E-mail: vc@out.ac.tz


WARAKA WA TAHADHARI YA MAAMBUKIZI YA COVID 19 NA 21


8 Februari 2021, Dar es Salaam,​



Ndugu Wafanyakazi na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,

Nianze kwa kuwatakieni heri ya mwaka mpya, kwani tangu mwaka huu uanze hatujaweza kukutana. Tumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutuvusha salama. Wapo wenzetu wengi ambao hawakuweza kuvuka, siyo kwamba walitenda maovu zaidi yetu sisi. Ni kwa neema na rehema za Mungu tu, kwamba sisi bado tupo hai hata leo.

Nachukua fursa hii kuwatahadharisha wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, kuwa hali ya maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu, au Covid 19/21, inazidi kushamiri mahali pote nchini mwetu. Ni budi kila mmoja wetu achukue tahadhari, kama inavyoelekezwa na viongozi wetu wa kitaifa. Ugonjwa huu inaeleweka, hauna tiba katika mahospitali yetu. Hata nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza zimeshindwa kuutibu. Chanjo inayopigiwa upatu, haijathibishwa kama inaweza kuuzuia. Wapo waliochanjwa na bado wameugua.

Hata hivyo, imethibitishwa kuwa taratibu za kijadi kama kujifukiza (Nyungu) zinaleta ahueni kwa walioathirika, ingawa haimaanishi kwamba virusi vile vitakufa. Pia dawa zilizobuniwa na wataalamu wa kitanzania kama vile Covidol na Nimricaf zinaonekana kutoa unafuu zikitumiwa pamoja na Nyungu. Inakuwa ni vigumu sana kuepuka maambukizi ikiwa hatuzingatii masharti ya kujikinga, ikiwepo kuepuka mikusanyiko ya watu kama vile harusi, misiba, viwanja wa michezo, masoko, na kadhalika. Watanzania wengi wanadhani ugonjwa huu utawapata wengine, wasitambue kuwa hata pale wanapopata maambukizi, huwa wamekuwa wazembe kujilinda.

Ni muda mfupi upo kuanzia mtu anapopata maambukizi hadi kuugua na kushindwa kupumua, hali inayolazimu mgonjwa kupelekwa hospitali ili awekewe hewa ya oksijeni kwa gharama kubwa akisubiri kufa! Tumepoteza watu wengi, na tungojee maafa makubwa zaidi kama hatutabadilika.

Naandika hapa kwa uchungu sana, ninapohesabu watu ambao wamefariki katika siku chache zilizopita. Wasomi na wasio wasomi. Wazee na hata vijana. Tutaendelea kupuuzia maelekezo ya viongozi wetu hadi lini? Wiki hii ilitangazwa kuwa ni wiki ya kupiga nyungu kitaifa. Je? Wewe umechukua hatua gani, kupiga nyungu, wewe na familia yako? Je? Unavaa barakoa unapokuwa kwenye mikusanyiko ya watu? Unapoenda sehemu za ibada? Unapoenda sokoni? Unapokuwa darasani? Unapopanda daladala? Na kadhalika. Je, unanawa kwa sabuni au kwa kutumia vitakasa mikono mara kwa mara? Kwa wale tunaoshika nyaraka maofisini tujitahidi kuvaa gloves, ama tutumie vitakasa mikono mara kwa mara. Kama hufanyi haya, basi ujihesabu kama mhanga mtarajiwa wa homa ya mapafu. Madereva pia wasituweke katika hatari, kwa maana wasizurure ovyo wanapokuwa hawatuendeshi. Ni vema madereva wakakaaa katika maeneo ya ofisi zao badala ya kuzurura ovyo, la sivyo itabidi viongozi waanze kujiendesha wenyewe.

Kwa upande wa wanafunzi wanaoingia chuoni, tunasisitiza kuwa wakae majumbani na kusoma kwa mtandao (Online). Hatutaruhusu wanafunzi na wageni kuingia kwenye kampasi zetu bila sababu maalum, kama kuja kuchukua vyeti au kufanya “clearance”. Na pale inapobidi waingie, watakiwe kuvaa barakoa wakati wote. Waende kule wanakotakiwa kwenda, na si kuzurura kila mahali. Utaratibu ufanyike kuwasaidia wanaotaka kutumia maktaba kama ni lazima, Wengi wanaitumia maktaba yetu kama mahali pa kujisomea tu. Maelekezo haya ni kwa ajili ya makao makuu, vituo vyote vya mikoa na vituo vya uratibu vilivyoko nchini.

Kuhusu vikao, ratiba ya vikao itaendelea kama ilivyopangwa, lakini vikao vyote vitafanywa kwa njia ya mtandao wa Zoom, isipokuwa Baraza la Chuo ambalo sina mamlaka nalo. Tutafanya Mkutano Wa Baraza la Wafanayakazi uliokuwa umepangwa kuwa tarehe 15 Februari huko Morogoro, kwa njia ya Zoom. Kamati Tendaji ya Baraza pia itafanya mkutano wake kwa Zoom siku ya Ijumaa, tarehe 12 Februari. Tayari kuna baadhi ya wajumbe wanaumwa, na hatuwezi kuhatarisha maisha ya watu wengine. Pia Baraza la Serikali ya Wanafunzi (USRC) lililopangwa kufanyika mkoani Mara, tarehe 17-19 Februari, litaendeshwa kwa Zoom. Waandaaji wa mikutano hii watapata link ya vikao kutoka kwa Eng, Petro Sanga na kuisambaza kwa wakati kwa washiriki wote.

Tunatoa tahadhari kwa wote wanaokusudia kusafiri nchi za nje, kuwa kipindi hiki siyo salama sana kusafiri. Nchi nyingi zina maambukizi ya Covid, hata ukipimwa ukakutwa huna maambukizi, unaweza ukawa “carrier”. Tutahitaji wanaotoka nje kujitakasa kwa kupiga nyungu na kujitenga angalau kwa wiki moja.

Nimetoa maoni yangu, kama ushauri, nikiwa nawajibika pia kama kiongozi, kuwalinda wale wote ninaowaongoza. Asanteni sana, Mungu awalinde, tumalize huu mwaka salama.


Prof. Elifas Tozo Bisanda

MAKAMU MKUU WA CHUO, CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA​

Umefanya kazi ya kiutume Prof. Bisanda, ubarikiwe sana kwa ujumbe huu, nina amini umeokoa watu wengi indirectly,
 
Mabibi na mabwana hii ni habari njema kutokea Open University of Tanzania.

Baada ya Chuo kikuu cha Dar es salaam kufanya kweli na kuwataka wote katika mazingira ya Chuo hicho kuzingatia tahadhali zote zilizopo kuhusiana na covid19, OUT nao wamefanya hivyo hivyo.

Kwa mujibu wa matangazo kupitia BBC, OUT wanawataka wote kunako mazingira ya Chuo kuhakikisha masharti yote ya kujikinga na corona yanazingatiwa.

Ama kwa hakika pongezi kwao sana, kama tutakavyowapongeza serikali pia watakapoona umuhimu wa kutuhami sisi wananchi ambako ni kwa mujibu wa wajibu wao kabisa.

UDSM walionyesha njia wengine kazi kwetu.

Ninawasilisha.
Inasikitisha sana Waziri wa Wizara husika ambaye ni msomi katika kada ya afya yupo against juhudi za wasomi hawa
 
Juzi nimepoteza ndugu wawili na tuliokuwa msibani wote tupo kwenye dozi za NIMRCAF wanne wapo kwenye oxygen. Hali ni mbaya.
Poleni sana mkuu...
M/Mungu awafanyie wepesi ... kwenye kipindi hiki kigumu!
 
Nitakuwa wa mwisho kumtupia jiwe Prof. Bisanda
 
A
naona huyu makamu wa chuo huria ,anajisahau.aliempa takwimu za kwamba ugonjwa umeshamili nchini Ni nani? hao wasomi anaodai akiwahesabu ambao wamekufa na covid tukimwambia atupe hiyo orodha atatupa? nadhani humu jf yumo,aandae majibu majibu sahh mapema kbsaa.
Acha utoto basi watu wanajadili mustakabari wa taifa afu we unaleta izi mambo zako. Uki kaa kimya unapungukiwa nini??
 
A

Acha utoto basi watu wanajadili mustakabari wa taifa afu we unaleta izi mambo zako. Uki kaa kimya unapungukiwa nini??
nilishaapa kwa jina langu si coment tena thread za covid.tangu Jana natekeleza kiapo chapo.na hapa sija coment.
 
Back
Top Bottom