Chuo Kikuu Huria (Open University of Tanzania)

Wakuu mimi ni form 4 .... naomba kuuliza,je naweza kupata nafasi ya kuanza certificate hapo OUT?
Na je wanatoa Faculty zipi (kama nitapewa listi nitashukuru sana)
Unaweza kuanza certificate kama walau Una D nne form four kama Maelekezo ya NACTE yalivyo.
 
Wakuu mimi ni form 4 .... naomba kuuliza,je naweza kupata nafasi ya kuanza certificate hapo OUT?
Na je wanatoa Faculty zipi (kama nitapewa listi nitashukuru sana)
Nakushauri kutembelea website Yao utapata kila kitu.
www.out.ac.tz
 
Hivi inawezekana kusoma degree mbili tofauti kwa mwaka wa masomo huo huo? Yani Nina maana kwamba mtu unasoma degree A,UDOM na wakati huo huo unasoma degree B Open university, je inawezekana?
Hauwezi kusoma shahada mbili kwenye vyuo viwili vilivyo chini ya TCU.
TCU Hawawezi kukupa admission mbili Kwa wakati mmoja lazima uwe deregistered chuo kimoja ili uombe kingine na kama umepata viwili au zaidi Kwa wakati mmoja lazima uconfirm kimoja.
 
Rafiki yangu amedahiliwa ktk foundation course ila ishu za uchumi zimemkalia vibaya kidogo, hivyo anahitaji kufahamu inawezekana akafanya malipo mwakani na kuanza kusoma?
Kama anaweza alipe first payment 210,000 then asajiri kozi zake aanze kusoma taratibu.
Au asajiri kozi chache aanze kusoma
 
Hivi kuna Faculty ya Procurement pale au Pablic relation mwenye kujua anijuze tafadhali
Kuna kozi ya Procurement and Supply Chain Management kuanzia Cheti mpaka shahada iko kitivo cha usimamizi wa biashara.
Pia kuna kozi ya Mass communication ambayo Mtu Wa Public Relations pia inamfaa iko ngazi ya Cheti mpaka Shahada ya uzamivu.
Public Relations yenyewe haipo.
 
Naomba kujua mahali kilipo chuo kikuu huria kwa Dar es Salaam
 
Habar, vip kwa wanaomba transfer-(NACTE) mnawapokea ? Social work nta level 5 march intake ?????
 
Mimi naomba kuuloza kuwa , kuna kozi ya foundation katika chuo cha open university of Tanzania, je mtu akisoma kozi hiyo na kuomba chuo kikuu akapata , je upande wa mkopo wa heslb anaweza kupewa au atasoma kwa gharama zake? Je akifaulu ataruhusiwa kusoma chuo chochote au ni out tu?
 
Hiyo kozi unajisomesha wala sio gharama sana tena ndani ya mwaka mmoja...jipange tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hiyo kozi unajisomesha wala sio gharama sana tena ndani ya mwaka mmoja...jipange tu.

#MaendeleoHayanaChama
Yaani namaanisha baada ya kumaliza kusoma hiyo Foundation course, nikiomba kusoma Bachelor Degree chuo chochote kilichopo Tanzania naweza kupata? Na je nikiomba mkopo kutoka heslb nitapewa?
 
Yaani namaanisha baada ya kumaliza kusoma hiyo Foundation course, nikiomba kusoma Bachelor Degree chuo chochote kilichopo Tanzania naweza kupata? Na je nikiomba mkopo kutoka heslb nitapewa?
Ndio unaweza kupata mkopo mana moja ya kigezo cha kupata mkopo ni kuwa admitted na chuo kwa masomo ya shahada..vigezo vingine hutolewa na bodi hivyo jitahidi kufahamu vigezo vya bodi kwa mwaka husika.

Shukrani kiongozi wangu
 
Safi sana Shukrani kwa ufafanuzi mzuri 🙏
 
Makao makuu yake sio Dar es salaam ni Pwani Kibaha kwa mathius kushoto kama unaenda morogoro ina range 3km kutoka barabara ya lami kimepakana na makao makuu ya Efatha ministry
 
Makao makuu yake sio Dar es salaam ni Pwani Kibaha kwa mathius kushoto kama unaenda morogoro ina range 3km kutoka barabara ya lami kimepakana na makao makuu ya Efatha ministry
Ni kweli panaitwa bungo ila temporary headquarters ni kinondoni ambako mambo mengi hufanyika hapo
 
Ninajiandaa kusoma Shahada ya Sociology Lakini cha kuhuzunisha about Open University ni kwamba yaani ni ngumu kupata taarifa za kozi yako na msaada mfano ningetegemea kuona kuna Group hata la Telegram la Open university Students mahali ambapo wana share vitu vingi ikiwemo pastpapers kuelekezana na kutiana moyo ila naona ni kama giza
 
Baada ya kutafuta bila mafanikio Group linalowaunganisha wanafunzi wa centers zote na kozi zote wa Chuo kikuu huria cha Tanzania nimeamua kutengeneza Link kwa ajiri ya wanafunzi wa Chuo kikuu huria ili kuwaleta pamoja waweze kusaidiana katika kupeana moyo, kujadiri mambo mbali mbali lakini pia kupeana msaada wa ki masomo. Wanafunzi wakiwa kwenye group kwa pamoja wataweza kupeana msaada wa wakati yaan ontime help.

Link ya Telegram: Open University Of Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…