Chuo Kikuu Huria (Open University of Tanzania)

Chuo Kikuu Huria (Open University of Tanzania)

Nina changamoto ya uelewa wa utaratibu kidogo wa OUT UNI,nimetumiwa email juzi ya admission letter MBA ya logistic ambayo sikuiomba mi niliomba MBA in accounting and Auditing so inawezekana nikabadili kozi? Na niko mbali na regional center

Na usajili naweza fanya kwa mbali bila kufika regional center? Regional center yangu ni Arusha
 
Usajili unafanya popote. Course pia unabadilisha.
Kifupi ni kama vyuo vingine tu
 
Nina changamoto ya uelewa wa utaratibu kidogo wa OUT UNI,nimetumiwa email juzi ya admission letter MBA ya logistic ambayo sikuiomba mi niliomba MBA in accounting and Auditing so inawezekana nikabadili kozi? Na niko mbali na regional center

Na usajili naweza fanya kwa mbali bila kufika regional center? Regional center yangu ni Arusha
Inawezekana kubadili kikubwa wasiliana na admission office
 
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (kwa Kiingereza: Open University of Tanzania) ni chuo kikuu kinachotoa kozi za cheti, stashahada na shahada kupita masomo ya mbali (Distance Learning). Makao makuu yako Dar es Salaam, Tanzania. Chuo Kikuu Huria kina takribani wanafunzi 70,000 kutoka ngazi mbalimbali za kitaaluma.

Historia
Kilianzishwa mwaka 1992 kwa kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992. Sheria hiyo ilipata nguvu ya utendaji rasmi tarehe 1 Machi 1993 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 55 ya gazeti lake rasmi.

Mwaka 1994, Januari 19 Makamu Mkuu wa kwanza wa Chuo alishika madaraka na mwezi huohuo walisajiliwa wanafunzi wa awamu ya kwanza.

Mwaka 2007 kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kilianza kutumia sheria na taratibu zake za ndani ya chuo toleo la mwaka (2007) katika shughuli zake za kiutawala.

Taaluma
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa stashahada, diploma na shahada mbalimbali kupitia elimu ya kimtandao au elimu ya masafa ya juu kwa njia ya tehama au nyenzo nyingine mbalimbali za kiteknolojia. Shughuli za chuo zinafanyika na kutoa huduma katika viwango vya utendaji na usimamiaji wa baraza la vyuo vikuu Tanzania (TCU). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatoa programu takribani 125.

Vituo
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina vituo kwenye mikoa zaidi ya 30 nchini Tanzania; hii ni kujumlisha na vituo vya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar (Unguja na Pemba), Kenya vituo viwili (Chuo cha Egerton na Njoro), Rwanda (eneo la Kibungo), Uganda na Namibia (Chuo cha Triumph).

Vituo vingine vya mashirikiano ya ndani ni ACDE-TCC (African Council for Distance Education- Technical Collaboration Committee), CECED (Centre for Economics and Community Economic Development), SADC ODL CoS TE (SADC Centre of Specialization in Teacher Education).

Chuo Kikuu Huria kina vituo vya kusomea takribani 69 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vitivo
Ina:

•Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii
•Kitivo cha Elimu
•Kitivo cha Sheria
•Kitivo cha Uongozi wa Biashara
•Kitivo cha Sayansi, Teknolojia na Masomo ya Mazingira
•Taasisi ya kuyaendeleza masomo
•Taasisi ya Teknolojia ya Elimu
•Kurugenzi ya Huduma za Mikoa
•Kurugenzi ya Utafiti na Masomo ya baada ya Shahada
Hivi inawezekana kusoma degree mbili tofauti kwa mwaka wa masomo huo huo? Yani Nina maana kwamba mtu unasoma degree A,UDOM na wakati huo huo unasoma degree B Open university, je inawezekana?
 
Hivi inawezekana kusoma degree mbili tofauti kwa mwaka wa masomo huo huo? Yani Nina maana kwamba mtu unasoma degree A,UDOM na wakati huo huo unasoma degree B Open university, je inawezekana?
Hapo inawezekana japo hairuhusiwi kwa wakati mmoja kuwa na masomo sehemu mbili tofauti.
 
Wakuu mimi ni form 4 .... naomba kuuliza,je naweza kupata nafasi ya kuanza certificate hapo OUT?
Na je wanatoa Faculty zipi (kama nitapewa listi nitashukuru sana)
 
Back
Top Bottom