Chuo Kikuu Huria (OUT), mnatakatisha vyeti vya wanasiasa?

Huu ni UFUKUNYUKU !
Nape ana hoja ya kujibu hapa, kazi kwake.
Ajitokeze hadharani na kujibu hoja hizi ili kuondoa tuhuma hizi za kuwa "Waziri kihiyo."
 
Na wakati wowote anaweza kuwa waziri wa elimu, viongozi wetu wanaufanya uongozi kama ndoa, mjinga, mwelevu, kichaa wote wanaoa.
Kama yule aliyesema kwenye mkutano wa kimataifa Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na Pemba
 
Ukiwa mwanaccm hicho ni kigezo tosha cha ufaulu, ndani ya CCM akina Nape wamo wengi hasa maprofesari.
 
Rafiki yangu ana BA(Economics Option) na MBA (Finance) zote za UDSM. Ana Div I Form Four na Div II Form Six PGM (Principal Passes D-E-D) lakini walimkatalia admission Faculty of Law Undergraduate ila Faustine Ndungulile na Nape Nnauye wakapewa admission.

OUT wajirekebishe.
 
Vetting ndio hii aliyoleta mwandishi. Inawezekana alifanyiwa ila yakafukiwa ila nahisi kuna mahali kakanyaga sio ndio unaona vetting halisi zinawekwa hadharani.
Aisee watu wanajua mpaka Registration number ahahahahah
 
Kujificha kwenye kufungia mitandao hakutamsaidia kujinasua kwenye hili

Utamkuta hapo alipo anamakasiriko utadhani ni sisi tulimzuia kusoma!
Na alivyo na matusi Sasa, atakuwa anatukana-tukana tu muda huu
 
Duh..braza Mdogo wangu Nape kakufanyia nn? Maana umempenyua mno!
 
Mkuu peno hasegawa, kwanza nikupe hongera sana, you can make a very good IJ fellow kwa sababu Tanzania tuna waandishi wachache wenye uwezo huu, japo you did your homework well, but you have missed the point kuhusu dhima ya open university.

Naomba usikilize kwa makini mahojiano yangu na Prof. Bisanda.
View: https://youtu.be/MIJKOKI8MzM?si=Fgsi13P37NXcAQg5
Kisha msikilize
View: https://youtu.be/53jFg1S4dG8?si=FULPqGjkviJtc-AFHumo utapata majibu yako yote,
Hivyo Nape anakidhi sifa zote na vigezo za kudahiliwa OUT kupitia utaratibu wao wa foundation course ili kukidhi viwango, na ndicho kinachofanywa na vyuo vikuu vya Marekani, Urusi, China na India, wanakutengenezea tailor made courses mpaka unakidhi vigezo!.

Sasa muombe radhi Nape Nnauye kwa kumchafua!
P
 
Duu
 
Alianzaje kujisajili kufanya mtihani wa kidato Cha SITA wakati Hana credits za kidato Cha nne!?na akapokelewa na kufanya Kisha akapata D'z za form six!?kwamba kote amekuwa tapeli ! Navojua ili ufanye exam kidato Cha SITA lazima uwe na C tatu, simchukii nape Wala simpendi ila mleta Uzi hapa napata ukakasi,hasa hapo nilipokoti,,,, I suggest uka-edit tena
 
mkuu napingana nawewe.kwa elimu zetu za vyeti hizi hapa nchini,nape na wenzake wako sahihi kabisa,mchongo ni gamba sio matokeo ya ulicho na elimu nacho.

leo kapata ya sheria,mwaka 2027 utashangaa anavaa joho la uchumi,2030 joho la sayansi ya jamii nk.ilimradi wanapitajwa ma DR nayeye awepo.

kwa nchi zinazojitambua,huwezi kujiona dhaifu kwa kukosa elimu,lakini pia huwezi kujiona imara kwa kuwa na cheti ambacho hustahili.
 
Mambo ya Ben Sananene na kiongozi wa kitaifa...
 
bonge moja la uongo yaan D,E,D iwe division II ya 13 umesoma nchi gani weye adi uyo rafiki yako awe na two ya PGM ya D E D
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…