Chuo Kikuu Marekani chawatuza watano Tanzania

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
WhatsApp Image 2024-12-08 at 13.52.13_ca041467.jpg
MWISHONI mwa wiki, Tanzania ilipokea heshima ya aina yake kwa watanzania watano waliotunukiwa udaktari wa heshima ya Chuo Kikuu cha Read Impact kilichopo Colorado nchini Marekani.

Tukio hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Tanganyika 2 ulioko kwenye Hoteli ya Land Mark, Ubungo jijini Dar es Salaam na kihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, walioshuhudia.

Akizungumza katika hafla hiyo mwakilishi wa Chuo hicho, Askofu Dk. Peter Rashid Abubakar anasema tuzo hizo zimetokana na uwasilishaji wa CV zao kwa chuo hicho.
WhatsApp Image 2024-12-08 at 13.52.14_1fd96ec2.jpg

WhatsApp Image 2024-12-08 at 13.52.14_02277cd9.jpg
Dk Rashid anasema baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo hivi karibuni watakabidhiwa vyeti vya utambulisho kutoka katika chuo hicho ili waendeleze gurudumu la maendeleo ya Taifa.

"Tuzo zilizopokelewa ni heshima kwao na Taifa kwa ujumla, kinachotakiwa ni utekelezaji wa majukumu inavyotakikana ndani na nje ya nchi," alisema.

Dk Rashid ambaye ndiye mratibu wa chuo hicho kwa nchi tano ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda na nyinginezo, anawapongeza waliotunukiwa udaktari huo kwamba wamefanya kazi zao inavyotakiwa ambako anatumia fursa hiyo kuiasa jamii kuandaa CV zao ili waweze kutunukiwa udaktari huo.

Chuo hicho msingi wake ni dini na kueleza kwamba udaktari huo wa heshima ni kazi zao zimeonekana.

Anasema kwa kuwa yeye ni tawi la chuo hicho hapa nchini anatoa wito kwa vijana ili kifunguliwe chuo ili linunuliwe eneo kitakapojengwa chuo hicho.

Waliotunukiwa vyeti vya udaktari wa heshima ni pamoja na CPA, Yona Hezekiah Malundo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya mahesabu ya Y.H Malundo Company, Mkurugenzi Mkuu Jenga Africa Empowering Society Build Nation (ESBN), Dk Paul Kanijo, Mkurugenzi wa Mesodate Consultants ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Millenium Solution Development Trust Fund, Dk Emmanuel Jeremiah.

Wengine ni Dk Boniface Mbelwa na mkewe Dk Chriatian Robert Mbelwa ambao ni mke na mume.

Aidha naye Diwani wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Juliet Banigwa aliwapongeza madaktari wenzake kwa tuzo hizo za udaktari sambamba na kumshukuru Dk Rashid ambaye ni msimamizi wa chuo hicho tawi la Tanzania.

Dk Juliet anasema tuzo hizo ni furaha na heshima kubwa kwa nchi kwani wataendelea kuwainua na kuwaimarisha watu na jamii kwa ujumla.

Dk Malundo anasema udaktari aliotunukiwa atautumia kwa wasiojiweza kwa sababu ndio eneo lake kuwasaidia wenye uhitaji.

Mkurugenzi wa Jenga Africa, Dk Kanijo anamshukuru Mungu kwa sababu wamesimama muda mrefu kuitumikia jamii.

Dk Kanijo anasema tuzo hizo ni jambo jema na baraka ambako anajisikia fahari na wataongeza jitihada zaidi katika utekelezaji wa majukumu.

Dk Jeremiah anasema watatekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi ili kuimarisha ujenzi wa Taifa.
 
Dini? Mambo ya hovyo hayo hata wewe ukiwa ana hela ya joho unapata
 
Naona taaluma imevamiwa na TCU ipo kimya. Huu ni uhuni tu, hapo unatoa pesa yako kisha unatunukiwa.

Kwa wasiofahamu tu, Tuzo (degree) ya heshima kutoka chuo kikuu chochote duniani haikupi status ya kuitwa Doctor.
Watu pekee wenye privilege ya utambulisho wao wa jina kuanza na Prefix ya Doctor (Dr) ni wawili tu.
1. Mhitimu wa shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu (yaani Bachelor of Medicine)
2. Mhitimu wa shahada ya juu (shahada ya tatu!), yaani shahada ya uzamivu, ikimaanisha shahada ya falsafa (Doctor of philosophy, PhD).

Kwa lugha rahisi, hukusoma na kufaulu katika shahada hizo, huna sifa ya kuitwa au kujiita Daktari. Hata mama yetu pale ikulu hana sifa wala haki ya kuitwa au kujiita Doctor.

Mfano mzuri ni Mwalimu Nyerere, japokuwa aliwahi kutunukiwa degree za heshima ya udaktari zaidi ya 10, lakini hakuwahi kujiita wala kukubali kuitwa Dr. Nyerere.
 
Mimi nilifikiri kama Taifa mwaka huu tumevuna wahitimu watano kutoka Harvard University, kwenye fani za uchumi, nk! Kumbe ni ujinga tu.
 
Naona taaluma imevamiwa na TCU ipo kimya. Huu ni uhuni tu, hapo unatoa pesa yako kisha unatunukiwa.

Kwa wasiofahamu tu, Tuzo (degree) ya heshima kutoka chuo kikuu chochote duniani haikupi status ya kuitwa Doctor.
Watu pekee wenye privilege ya utambulisho wao wa jina kuanza na Prefix ya Doctor (Dr) ni wawili tu.
1. Mhitimu wa shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu (yaani Bachelor of Medicine)
2. Mhitimu wa shahada ya juu (shahada ya tatu!), yaani shahada ya uzamivu, ikimaanisha shahada ya falsafa (Doctor of philosophy, PhD).

Kwa lugha rahisi, hukusoma na kufaulu katika shahada hizo, huna sifa ya kuitwa au kujiita Daktari. Hata mama yetu pale ikulu hana sifa wala haki ya kuitwa au kujiita Doctor.

Mfano mzuri ni Mwalimu Nyerere, japokuwa aliwahi kutunukiwa degree za heshima ya udaktari zaidi ya 10, lakini hakuwahi kujiita wala kukubali kuitwa Dr. Nyerere.
Mkuu, huku ni kujidanganya. Ni kama ule mchezo wa watoto kucheza ki-baba baba na ki-mama mama. Huku ni kujidang'anya kwa sababu hazijulikani sehemu za maana.
 
Naona taaluma imevamiwa na TCU ipo kimya. Huu ni uhuni tu, hapo unatoa pesa yako kisha unatunukiwa.

Kwa wasiofahamu tu, Tuzo (degree) ya heshima kutoka chuo kikuu chochote duniani haikupi status ya kuitwa Doctor.
Watu pekee wenye privilege ya utambulisho wao wa jina kuanza na Prefix ya Doctor (Dr) ni wawili tu.
1. Mhitimu wa shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu (yaani Bachelor of Medicine)
2. Mhitimu wa shahada ya juu (shahada ya tatu!), yaani shahada ya uzamivu, ikimaanisha shahada ya falsafa (Doctor of philosophy, PhD).

Kwa lugha rahisi, hukusoma na kufaulu katika shahada hizo, huna sifa ya kuitwa au kujiita Daktari. Hata mama yetu pale ikulu hana sifa wala haki ya kuitwa au kujiita Doctor.

Mfano mzuri ni Mwalimu Nyerere, japokuwa aliwahi kutunukiwa degree za heshima ya udaktari zaidi ya 10, lakini hakuwahi kujiita wala kukubali kuitwa Dr. Nyerere.
Tanzania ina idadi kubwa ya wapumbavu,na sifa ya mpumbavu iko bayana kupitia maneno ya Baba wa taifa.

"Huwezi muelimisha mpumbavu akaacha upumbavu wake"Mwl. Nyerere

Licha umetoa Elimu hii muhimu wapumbavu hawawezi elewa,zaidi watakuona una wivu.
 
Read Impact ni chuo cha kimataifa kama Harvad, Yale, Mississippi, Ohio au nacho ni chuo kidogo tu huko marekani? Maana hata bongo vimeibuka vyuo vya ajabu ajabu vinatoa shahada za heshima
 
Back
Top Bottom