JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tukio hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Tanganyika 2 ulioko kwenye Hoteli ya Land Mark, Ubungo jijini Dar es Salaam na kihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, walioshuhudia.
Akizungumza katika hafla hiyo mwakilishi wa Chuo hicho, Askofu Dk. Peter Rashid Abubakar anasema tuzo hizo zimetokana na uwasilishaji wa CV zao kwa chuo hicho.
"Tuzo zilizopokelewa ni heshima kwao na Taifa kwa ujumla, kinachotakiwa ni utekelezaji wa majukumu inavyotakikana ndani na nje ya nchi," alisema.
Dk Rashid ambaye ndiye mratibu wa chuo hicho kwa nchi tano ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda na nyinginezo, anawapongeza waliotunukiwa udaktari huo kwamba wamefanya kazi zao inavyotakiwa ambako anatumia fursa hiyo kuiasa jamii kuandaa CV zao ili waweze kutunukiwa udaktari huo.
Chuo hicho msingi wake ni dini na kueleza kwamba udaktari huo wa heshima ni kazi zao zimeonekana.
Anasema kwa kuwa yeye ni tawi la chuo hicho hapa nchini anatoa wito kwa vijana ili kifunguliwe chuo ili linunuliwe eneo kitakapojengwa chuo hicho.
Waliotunukiwa vyeti vya udaktari wa heshima ni pamoja na CPA, Yona Hezekiah Malundo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya mahesabu ya Y.H Malundo Company, Mkurugenzi Mkuu Jenga Africa Empowering Society Build Nation (ESBN), Dk Paul Kanijo, Mkurugenzi wa Mesodate Consultants ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Millenium Solution Development Trust Fund, Dk Emmanuel Jeremiah.
Wengine ni Dk Boniface Mbelwa na mkewe Dk Chriatian Robert Mbelwa ambao ni mke na mume.
Aidha naye Diwani wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Juliet Banigwa aliwapongeza madaktari wenzake kwa tuzo hizo za udaktari sambamba na kumshukuru Dk Rashid ambaye ni msimamizi wa chuo hicho tawi la Tanzania.
Dk Juliet anasema tuzo hizo ni furaha na heshima kubwa kwa nchi kwani wataendelea kuwainua na kuwaimarisha watu na jamii kwa ujumla.
Dk Malundo anasema udaktari aliotunukiwa atautumia kwa wasiojiweza kwa sababu ndio eneo lake kuwasaidia wenye uhitaji.
Mkurugenzi wa Jenga Africa, Dk Kanijo anamshukuru Mungu kwa sababu wamesimama muda mrefu kuitumikia jamii.
Dk Kanijo anasema tuzo hizo ni jambo jema na baraka ambako anajisikia fahari na wataongeza jitihada zaidi katika utekelezaji wa majukumu.
Dk Jeremiah anasema watatekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi ili kuimarisha ujenzi wa Taifa.