Hii yote inatokana na kung'ang'ania hii sera iliyopitwa na wakati ya watoto wetu kusoma "BURE" au kwa "MIKOPO" kutoka serikalini. Serikali itaendelea kutudhalilisha inavyotaka. Siku zote anayemlipa mwanamziki ndiye anayechagua wimbo! Natoa wito kwa WAZAZI wenzangu tujiandae kikamilifu kuwasomesha wanetu hata kama ni kwa kuchangishana wenyewe. Mbona HARUSI, MAKANISANI, ... tunachangishana kwa mamilioni? Sadaka ya Ibada moja tu pale St. Joseph siku ya Jumapili ni shs ngapi? Fedha hizi zinawasaidia wangapi?
Uongozi wa UDSM ulichelewa kuifuta hii DARUSO, to me DARUSO haikuwa ikikidhi mahitaji na matakwa ya wanachuo zaidi ya kuwa jukwaa la kuendesha siasa na kuwanyima haki wale ambayo wapo kwa nia ya kusoma. Ifike mahali wanafunzi waelewe kuwa kazi yao hapo UDSM ni kusoma na wale siyo kuendesha Chuo. Kazi za kuendesha Chuo ziachwe kwa Viongozi wa Chuo vinginevyo wanafunzi wanachukua muda mwingi kufanya yale ambayo haya wahusu kimsingi.
Bravo kwa kuifuta DARUSO
Unayosema ni ya kweli lakini napata taabu kuamini kama umeshawahi kutoka nje ya Dar es Salaam ukaushuhudia umasikini wa Tanzania. Ndugu yangu Tanzania sio Dar es Salaam pekee. Asilimia 80 ya watanzania wanategemea kilimo na wengi wao cha jembe la mkono! Wanaweza kulima ekari ngapi ili wapate chakula na ziada ya kusomesha watoto?
Ni mawazo hasi kusema kila siku mimi maskini basi nisaidie!!!
Tanzania na watu wake sii nchi maskini!
Mimi sikubali kuwa Tanzania ni maskini na kwa hiyo watu wake hawawezi kuchangia elimu ya juu ya watoto wao waliowazaa!
Hukohuko vijijini tembelea sehemu zao za starehe uone hiyo pesa kidogo wanayopata wanavyoitumia. Angalia wazee wanavyoongeza wanawake kila mwaka kwa mahari ya kumsomesha mtoto hadi chuo kikuu bila tatizo. Serikali za VIJIJI zikiwa na mipango na na uelewa wa kutosha wa wanavijiji hakuna mtoto ambaye hatasoma.
SMU,
Ukienda chuo kikuu chochote hapa nchini HAKUNA mtoto wa MASIKINI uliemuelezea hapo juu anayesoma huko. Mtoto wa masikini wa aina hiyo hatakosa msaada toka kwa ndugu, jamii au halmashauri husika. Tunaongopeana na kudanganyana sana inapofikia kueleza vipato vyetu halisi.
SMU,
Watoto wa mitaani wanatokana na sisi ambao tunafanya mapenzi bila mpangilio na kila tunayekumbana naye barabarani. Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wana mchango mkubwa tu kwa kuzalisha watoto hawa. Nakaa jirani na chuo kikuu kimoja hapa Dar. Nimeshindwa kukaa na housegirl mwaka ukaisha bila kupachikwa mimba na mmoja wanafunzi wa chuo hiki!
Watoto wa mitaani wanatokana pia na dada zetu kukimbilia mijini bila kujua huko wanakwenda kufanya nini. Wengine wanatokana na tabia na hulka ya baadhi ya makabila yetu kupenda kuwa OMBAOMBA.
Date::1/15/2009
Wabunge: Wanafunzi wote vyuo vikuu warejeshwe
Jackson Odoyo
Mwananchi
WABUINGE wameitaka serikali isimamie zoezi la kuwarejesha wanafunzi wa vyuo vikuu waliofukuzwa na kuhakikisha kwamba wote wanarudishwa masomoni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, mwenyekiti wa kamati hiyo, Omary Kwaang alisema serikali inatakiwa iwe makini katika suala hilo la kurejesha wanafunzi hao chuoni.
Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo siku moja baada ya vyuo vikuu mbalimbali nchini, kutangaza utaratibu mpya wa kuwarejesha wanafunzi waliofukuzwa mapema mwaka jana kwa sababu za mgomo vyuoni.
Moja ya taratibu hizo ni suala la kujaza fomu na kujiandikisha upya huku wakitakiwa kulipa madeni yote wanayodaiwa chuoni hapo.
Sababu kubwa iliyofanya wanafunzi hao kuanzisha migomo hiyo ni kupinga sera ya uchangiaji wa elimu, wakidai kuwa inawapa upendeleo wanafunzi wanaotoka katika familia zenye uwezo na kuwabana wale wanaotoka katika familia zisizokuwa na uwezo.
"Tunaomba serikali iwe makini katika suala hili la kurudisha wanafunzi vyuo vikuu na kuhakikisha kwamba, hakuna mwanafunzi atakayeachwa katika zoezi hili la kuwarejesha," alisema Kwaang' na kuongeza:
"Hatuoni sababu ya baadhi ya wanafunzi kurejeshwa na wengine kukataliwa. Hiyo si halali hata kidogo".
Kwaang' pia alisema hakuna sababu ya nchi kuendelea kubeba mzigo wa kusomesha watoto wanaotoka familia zenye uwezo wakati kuna watoto wanaohitaji msaada wa serikali.
"Watoto wote wenye uwezo wa kuchangia wanapaswa kuchangia masomo yao, ili serikali iendelee kuwasaidia watoto wasiokuwa na uwezo," aliongeza Kwaang'.
"Ingawa sera ya kuchangia huduma ni jambo la msingi katika jamii, kitendo cha Bodi ya Mikopo kuwagawa wanafunzi katika makundi sita kinaigawa nchi katika makundi mawili na inawaongezea wazazi mzigo."
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, George Nyatega alisema ili kukuza kiwango cha fedha zinazotolewa wakati wa mikopo, inapaswa fedha hizo zitozwe riba.
"Fedha zinazokopeshwa zinapungua thamani yake kila siku, kwa sababu hazitozwi riba, sasa basi ili hali hiyo isiendelee kuwepo inabidi wanafunzi wote wanaopewa mikopo watozwe riba," alisema Nyatega na kuongeza:
"Mikopo inatolewa bila kutoza riba na urejeshwaji wake huchukua muda mrefu (hadi miaka 10) ni dhahiri kwamba thamani yake inapungua."
"Njia pekee ya kulinda thamani ya mikopo hiyo ni kutoza riba inayolingana na mfumuko wa bei".
"Pamoja na kwamba wazo la kutoza riba halikubaliki kwa wadau, bodi itaendelea kulielezea ili liweze kueleweka," alizidi kusisitiza.
Hata hivyo Kwaang' alifafanua kwamba sera ya kuchangia iko katika sekta zote, lakini tatizo ni namna ya kuitekeleza kwani utekelezaji wake inachangia kuwagawa wanafunzi na kwamba, hali hiyo ikiachwa iendelee itawagawa watoto wa Kitanzania kwa maana kwamba kutakuwa na tabaka la watu wenye elimu na wasiokuwa na elimu ndani ya nchi moja.
"Haya makundi ya wanafunzi wanaopewa mikopo yanaongeza mzigo kwa wazazi na pili yanaleta tabaka la elimu ndani ya nchi kiasi ambacho kinatufanya tujiulize maswali mengi," alisema.
"Sera ya uchangiaji haiepukiki, lakini tatizo linalokuja hapa ni utaratibu wa kuwagawa wanafunzi hawa katika makundi sita ya uchangiaji, sasa swali la kujiuliza katika hili ni je, utaratibu huo hauwaachi wanafunzi wanaostahili ? alihoji mwenyekiti huyo.
Katika hatua nyingine, Kwaang' alisema utaratibu huo haustahili hata kidogo kwa sababu inawaongezea wazazi mizigo ambayo haistahili na kwamba inawafanya washindwe kuwasomesha watoto.
Mfumo unaotumiwa kuchambua uwezo wa kiuchumi wa wazazi wa wanafunzi hao (means testing) huwagawa wanafunzi katika makundi sita. Kundi la kwanza "A", mwanafunzi hupata mkopo kwa asilimia mia, wakati katika kundi "B", mwanafunzi hupata mkopo kwa asilimia 80 na katika kundi la tatu, mwanafunzi hupata mkopo kwa asilimia 60.
Katika kundi la tatu, mwanafunzi hupata mkopo kwa asilia 40 na kundi la mwisho linahusu wanafunzi ambao hawapati mkopo kabisa.
"Tunazingatia uwezo wao kiuchumi wa mwombaji ikiwa pamoja na historia ya elimu ya mwombaji, kiwango cha elimu ya wazazi ama walezi wake, shughuli za kiuchumi za mwombaji na wazazi au walezi," alisema Nyatega.