Kufuta DARUSO si ufumbuzi na huwezi kuwa ufumbuzi hata siku moja. Nifikra ya mbuni kuficha kichwa kwenye mchanga na kudhani haonekani.
Moja ya tatizo la msingi huwa ni kuwa viongozi wengi wa chuo na hata serikali huwachukulia wanafunzi wa vyuo vikuu kama viumbe wasio na akili hata kidogo, ambayo upofu na ukiziwi wa uelewa. Jaribu kukumbuka pale mwanafunzi wa mwaka wa tano pale Muhimbili anagoma na unamfukuza bila kujiuliza kulikoni, maana yake umeona huyu ni mjinga tu, lakini ukimrudisha miezi tisa baadaye ni Daktari na wewe uliyemfukuza unakwenda kwake unaumwa AKUTIBU, unaweka maisha yako mikononi mwake!!!!!!!!!!!!!!!!!! sasa ghafla huyu amekuwa mtaalamu mpaka ukaridhika naye vipi. Hao wengine wa mwaka wa tatu ndio watakaoajiriwa hivi karibuni ili kujaza nafasi tunazoacha tunaozeeka!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Ikumbukwe hata akina Warioba waligoma wakachapwa viboko baadaye ndio Waziri Mkuu wa nchi n.k.
Kunahitajika utathimini wa kutosha hapa kabla ya kukurupuka kwa hasira tu kuwafukuza, kuvunja DARUSO hata kuandika kwamba ni wajinga.
Inanikumbusha mwaka fulani nikiwa UDSM, kulikuwa na mgomo UDSM, magazeti yakaandika wanafunzi wa UDSM wamegoma kwa vile hawajala mayai na kupewa maziwa WACHA WANANCHI NA WAZAZI WETU WACHARUKE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Lakini ukweli ULIKUWA WANAFUNZI WALIKUWA WAKIMWAMBIA MAKAMU MKUU WA CHUO KUWA ILE TAARIFA YA KWAMBA WANAFUNZI WAMEKULA MAYAI ILIKUWA YA UONGO KWA SABABU HAWAKULA (KA-UFISADI KALIKUWEKPO) Bahati nzuri baadaye watu wa usalama wa taifa wakafanya uchunguzi ikagindulika kuwa taarifa za matumizi ya Cafeteria zilikuwa na wizi mkubwa (na ilikuwa kidogo tu tufukuzwe) na aliyekuwa Mkuu wa Cafeteria aliachishwa nafasi hiyo.
Hivyo tusikimbilie ufumbuzi wa haraka haraka UNAOFICHA MAMBO MAKUBWA MAHALI, TUTAKUJA JUTA!!!!!!!!!