Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Sidhani kama kuutwa kwa DARUSO ni kumaanisha kuwa wanafunzi hawatakuwa na representation. Ni obvious kwamba kutakuwa na chombo kipya kwa ajili ya wanafunzi. Kama jinsi JUWATA ilivyokufa ikaja OTTU, TUGHE, TUICO etc... Kwa hawa wanafunzi wa UDSM kulikuwa na haja ya kufuta chama chao ikiwa ni mojawapo ya mbinu ya kuweka bayana kuwa wanakuja upya kama wanafunzi wapya. Hii ilisababishwa pia na kitendo cha kiongozi wa iliyokuwa DARUSO kuwatangazia wanafunzi kupitia vyombo vya habari kuwa wafike chuoni hata kama hawajatimiza masharti, sasa hapa kama wana JF wenzangu hamuoni kuwa the late DARUSO ilikuwa ni tatizo kwa hali ya utulivu na maelewano then labda tukubali tu kutofautiana kimawazo.
Kosa lingine ni letu wazazi. Vijana wanagoma wakiangalia uwezo wa sisi wazazi wao. Sisi tunakaa kimya kana kwamba hayatuhusu. Tunawasaliti vijana na kwa kufanya hivyo tunajisaliti wenyewe. Tunapaswa kupaza sauti zetu na kumuuliza JK, mbona watoto wa maskini wanakosa elimu wakati ulisema haitatokea hivyo?
Tujiulize pia, hivi watoto wote wanaotaka mkopo wakipewa asilimia 100 kuna shida yoyote? La msingi ni kuwabana walipe, period. Ni kama nataka kulima, naenda benki kukopa, benki inanipa hela za kulimia tu na inasema za kuipanda na kupalilia nijitegemee wakati sina uwezo huo. Je nikilima tu huo mkopo utarudi? Si bora wanikoppeshe hadi gharama za kuvuna na kuuza ili hayo mauzo ndiyo nilipe mkopo?. Serikali tumia akili.
Tatizo linakuwa gumu kwani JK, mkuu wa nchi alitoa msimamo wake mapema sana juu ya suala la sera ya uchangiaji kuwa haitabadilishwa. Ni kosa kubwa kwa rais kutoa misimamo kama hiyo kwani wewe ndiye mkuu kabisa, Sasa tuone kama hatakula matapishi yake.
Akisema sera ibaki hivyohivyo - kala matapishi yake watoto wa maskini hawatasoma. akisema ibadilishwe - kala matapishi yake maana alishasema haitabadilishwa. KAZI KWELIKWELI.
Ni mawazo hasi kusema kila siku mimi maskini basi nisaidie!!!
Tanzania na watu wake sii nchi maskini!
Mimi sikubali kuwa Tanzania ni maskini na kwa hiyo watu wake hawawezi kuchangia elimu ya juu ya watoto wao waliowazaa!
Hatimaye Chuo kikuu cha Dar es Salaam katika mkakati wa kuhakikisha kwamba wanaingia chuoni wale tu wanaostahili, kuanzia tarehe 18--23, Menejimenti ya Chuo imetoa ilani kwa watumiaji wa njia zinazopita chuoni hapo kutotumia njia hizo! kwa maana nyingine kwa mjibu wa ilani hiyo ambayo nimebahatika kuiona milango miwili ama geti mbili tu zitatumika, kuingia chuo italazimika kupita geti maji na kutoka itakuwa geti la Chuo cha ardhi, mageti mengineyo kama Changanyikeni nk hakuna ruksa hata kidogo! katika kipindi hicho! sisi wakaazi wa Changanyikeni nk tunashauriwa kutumia njia ya msewe kuelekea Ubungo na kama tunahitaji kwenda Mwenge basi njia ni Makongo juu! wanafunzi wa shule za msingi wataruhusiwa kupita katika lango la chuo kama tu watakuwa na sare zao za shule, na kwa wafanyakazi wote wa chuo watalazimika katika kipindi chote hicho kutumia vitambulisho vyao na kuwaonyesha walinzi wa chuo auxiliaries vitambulisho vyao! na kwa kada nyinginezo kama Wanajeshi wote watalazimika kutii utaratibu huo uliowekwa na Chuo, mh! ndiyo mambo hayo ya private roads nk wana exercise jurisdiction yao! Ilani haijasema kwasisi wengine ambao makulaji yetu na masuala ya chinywaji tunategemea UDASA club, Hillpark nk status yetu ni vipi? lakini pia kwa wengineo tulio na marafiki na ndugu wa karibu malekchara hapo mlimani ilani haijasema kabisa inakuwa vipi? ama kama ninashida yoyote itakayonilazimu nifike chuo itakuwa vipi? Je uamuzi uliochukuliwa umezingatia kabisa mibadala yote ambayo ingewezekana kuchukuliwa? ama ndio haya mambo ya kumeneji ki makenika? Je kulikuwa na ulazima wowote wa kutupa adhabu sisi wakazi wa pembezoni mwa chuo? ama wananchi wengine wa kawaida? ama tunapata adhabu kimtindo kwasababu ya ndugu na wadogo zetu 'jeuri'?
Chuo Kikuu hakiwezi kuendeshwa kama kambi ya jeshi. Uhuru unahitajika vyuo vikuu vyote duniani. UDSM haina wanafunzi wa kimataifa? Watavumiliaje unyanyasaji huu?
Naomba kama kuna mwenye University of Dar es Slaam Act atuwekee hapa ili tuone wenyewe kama kuna sheria zinavunjwa na hawa watawala.
Cheo ni dhamana. Maprofesa wasitumie vyeo vyao kudumaza vijana wetu. Kijana unayempangia wapi apite, nini avae, nini aseme, nani amtawale, etc., atakuwa bwege lisilo na faida yoyote kwa taifa. Maprofesa wasikubali kuwa vibaraka wa seriakali wa kugeuza UDSM iwe kama kambi ya jeshi.
Wananchi wote wanapashwa kujiuliza ni nani ana haki ya kusoma chuo kikuu: ni watoto wa matajiri tu? Ni jukumu la wananchi, na makundi maalum kama UDASA, kupigania haki sawa katika Elimu.

Hivi Mkuu wa Chuo angelikua Prof. Viktor au Prof. Peter au Prof. Mbogo-watu wapole na wastaarabu na wasio na papara na kifu fesa chuo kikuu kweli kingelikwenda njia inayokwenda sasa.
Ninadhani chini yao fedha inayozalishwa na Chuo Kikuu katika miradi yake mbalimbali ingelionekana na ingelitumika kuwalipia wale wasioweza kuafodi fuli malipoz!!
Leo katika maeneo ya Manzese tulikosa umeme kuanzia saa 12 kasoro hadi kilipoisha kipindi cha hapa na pale kinacharushwa na ITV. Ninaongelea Manzese kwa sababu wakati huo nilikuwa maeneo hayo ya Manzese. Baada ya kipindi hicho umeme ulirudi. Ninachouliza ni kwamba je kwenye maeneo mengine nchini umeme ulikuwa je? Ulikatika pia? Hata ilipofika saa moja kamili usiku wakati wa kipindi cha Taarifa ya habari cha Channel Ten umeme pia ulikatika. Chakushangaza zaidi ilipoakaribia saa 2.00 kamili jioni umeme ulikatika tena. Wakati huo ni wakati wa taarifa ya habari za ITV na TBC one. Nilijiuliza kukatika kwa umeme kulipangwa ili tusipate matukio yaliyojiri UDSM kuhusiana na udahili wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au ni tatizo la kiufundi?