Hatimaye Chuo kikuu cha Dar es Salaam katika mkakati wa kuhakikisha kwamba wanaingia chuoni wale tu wanaostahili, kuanzia tarehe 18--23, Menejimenti ya Chuo imetoa ilani kwa watumiaji wa njia zinazopita chuoni hapo kutotumia njia hizo! kwa maana nyingine kwa mjibu wa ilani hiyo ambayo nimebahatika kuiona milango miwili ama geti mbili tu zitatumika, kuingia chuo italazimika kupita geti maji na kutoka itakuwa geti la Chuo cha ardhi, mageti mengineyo kama Changanyikeni nk hakuna ruksa hata kidogo! katika kipindi hicho! sisi wakaazi wa Changanyikeni nk tunashauriwa kutumia njia ya msewe kuelekea Ubungo na kama tunahitaji kwenda Mwenge basi njia ni Makongo juu! wanafunzi wa shule za msingi wataruhusiwa kupita katika lango la chuo kama tu watakuwa na sare zao za shule, na kwa wafanyakazi wote wa chuo watalazimika katika kipindi chote hicho kutumia vitambulisho vyao na kuwaonyesha walinzi wa chuo auxiliaries vitambulisho vyao! na kwa kada nyinginezo kama Wanajeshi wote watalazimika kutii utaratibu huo uliowekwa na Chuo, mh! ndiyo mambo hayo ya private roads nk wana exercise jurisdiction yao! Ilani haijasema kwasisi wengine ambao makulaji yetu na masuala ya chinywaji tunategemea UDASA club, Hillpark nk status yetu ni vipi? lakini pia kwa wengineo tulio na marafiki na ndugu wa karibu malekchara hapo mlimani ilani haijasema kabisa inakuwa vipi? ama kama ninashida yoyote itakayonilazimu nifike chuo itakuwa vipi? Je uamuzi uliochukuliwa umezingatia kabisa mibadala yote ambayo ingewezekana kuchukuliwa? ama ndio haya mambo ya kumeneji ki makenika? Je kulikuwa na ulazima wowote wa kutupa adhabu sisi wakazi wa pembezoni mwa chuo? ama wananchi wengine wa kawaida? ama tunapata adhabu kimtindo kwasababu ya ndugu na wadogo zetu 'jeuri'?