Waga
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 322
- 14
Good, safi sana
tena saaaaaaaaaaaana, lazima watanyooka tu warudi wakagome tena then waone nini kitatokea.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Good, safi sana
Hebu na tufanye assessment ya nini hao DARUSO walichofanya lets say for the past 10 years.
Mwenye data na atoe...Mimi niiinonayo ni kila siku kuitisha mikutano ya migomo tu.....
Kuna data zozote zinazoonyesha kama serikali ya wanafunzi inamsaidiaje wanafunzi wa kawaida wa mwaka wa kwanza?? Kam zipo na za kujitosheleza then tunaweza kutajadili tofauti, kama hakuna...Then ni sawa tu kufungiwa.
Na si vitambulisho pekee tu, washurutishwe kuvaa na sare sasa...Napendekeza suruali/sketi za kijani mpauko na mashati ya kahawia ili waonekane vizuri wakipita mahali....
Ndio nilitaka kuuliza na mimi kazi za Daruso....tatizo la wale vijana nasikia Chadema waliwadanganya asa ona madhara wanayoyapataHebu na tufanye assessment ya nini hao DARUSO walichofanya lets say for the past 10 years.
Mwenye data na atoe...Mimi niiinonayo ni kila siku kuitisha mikutano ya migomo tu.....
Kuna data zozote zinazoonyesha kama serikali ya wanafunzi inamsaidiaje wanafunzi wa kawaida wa mwaka wa kwanza??....
kwikwikwikwikwikwiNapendekeza suruali/sketi za kijani mpauko na mashati ya kahawia ili waonekane vizuri wakipita mahali....
1. sasa watanzania tunawaiga Makaburu na sera yao ya apartheid kwani wabantu ktk maeneo yaliyotengwa ( reserved bantuland) walitakiwa kuvaa vitambulisho.
2. Kuna tatizo gani kama mtu ataingia darasani halafu asifanye mtihani? Siono haja ya watu kuonyesha vitambulisho ndio aingie darasani.
3. "PhD holders are people who are very deep in the ocean but at a very shalow water to the extent that their backs are seen". Usomo wao uko wapi ktk masuala madogo kama haya?
Jamani sio kila wakati tuwe watu wa kutoa lawama tu pasipo na sababu za msingi, chuo kuamua kuifuta daruso mimi naona wapo sahihi kabisa maana hiyo daruso ilishapoteza mwelekeo wake na ikabakia kuanzisha migomo isiyokuwa na msingi, WHY nimesema hivi:-
Hebu nambieni shuo kimetoa masharti kwa mwanafunzi anayetaka kurejea chuoni ni lazima ajaze forms za kuomba kudahiliwa upya na awe ameambatanisha risiti za ada na awe amemaliza ada yote then azitume kwa registre kabla ya tar 2 january 2009,, wapo waliotimiza haya masharti na wapo wengine walijaza forms na kutokulipa ada wakitegemea chuo watalegeza masharti na watarudi bila kumalizia ada kama ilivyokuwa huko nyuma kwenye migomo mingine, chuo kwa kuwaonea huruma wakawaongezea muda wale ambao walisubmit forms bila kumaliza ada wakawapa mpaka tar 15 january 2009 then tar 16 up 2 17 jan watatoa batch ya pili ya majina ya wale walioweza kufikisha sifa za kurudishwa chuoni, sasa kilichotokea ni kwamba chuo wamekuwa na msimamo mmoja tu kuwa atakayemaliza ada ndiye atakayeruhusiwa kurudi chuo, na asiye maliza basi huyo hataki kusoma. na kwa kiasi kikubwa wanafunzi wameweza kwenda kulipa ada ili waweze kurejeshwa chuoni, sasa haya yaliyopelekea chuo kuamua kuifuta DARUSO ni kwamba:- Juzi tu hapa huyu raisi wa wanafunzi somebody Machibya ameenda kufanya pressconference kuutangazia uma wa wanafunzi wote kuwa ifikapo tarehe 19 January 2009 wanafunzi wote waripoti chuoni wawe wamemaliza ada au hawajamaliza ada waende chuoni na wataingia darasani kama kawaida, sasa hebu niambie wewe ambaye unalaumu why DARUSO imefutwa hii ni kutafuta haki au kutafuta choko choko zisizo na msingi kwa serikali?? Wewe ni nani mpaka utake kutengua maamuzi ya wakuu wako ambao wanakufundisha hapo chuoni na utake kutengua maamuzi ya serikalli? kanini usingekuwa mpole tu? na alipoulizwa kama yeye amelipa au la akasema kwa kujiamini kabisa kuwa hajalipa na hatalipa na chuoni atarudi tu sasa hii ni haki?? wanafunzi wenzako 8000 wameenda kulipa ada wewe unautangazia uma kuwa hutalipa ada na chuoni utarudi tu who are you?? Chuoni kila mtu alienda kwa wakati wake na usia alipewa na wazazi wake na anapofuikuzwa anaondoka peke yake kurudi kwa wazazi wake peke yake hakuna solidarity tena zaidi ya kujawa na hofu utaenda kujibu nini kwa mzazi wako ambaye ni mkulima. Sasa chuo ndo kimeshaamua hivyo no way hakuna DARUSO mpaka hapo itakapotungwa sheria mpya na si daruso tu hakuna society yoyote ya wanafunzi inayotambulika kwa sasa mpaka hapo chuo kitakapotoa utaratibu mpya na kutangaza kwenye gazeti la serikali out off that unajitafutia kuumia tu,, mbaya zaidi nasikia kwamba wamevunjiwa sehemu yao pale nje walipokuwa wanakaanga chips na bar yao walikuwa wanasubiriwa wamalize stock ya vinywaji vilivyopo the waifunge kabisa na ofisi zao walishaambiwa watoe wanachokiona ni chao watafute sehemu nyingine si kwenye majengo ya chuo.
Na pressconference aliyoifanya huyu raisi wa DARUSO ndo imepelekea chuo kutoa maamuzi ya kuwataka wanafunzi wavae kitambulisho watakachopewa upya maana inspection inaanzai getini, unafika pale unaangalia jina lako lipo unaruhusiwa kuingia ndani ya chuo kwa ajili ya registration na unatakiwa kukiacha pale kitambulisho chako cha zamani,, ukiangalia hii yote ni kutaka kuwabana wale ambao wamegoma kulipa ada na wanataka kuja kusoma bure na ndo hao hao waanzisha migomo isiyokuwa na msingi, hebu tufikirie kwanza kabla ya kulalama tu kuna ncho ambayop inatoa elimu bure kwa sasa hivi? ukinambia sweedn, Finland, Norwey nitakucheka maana hao wanakusomesha lakini joto ya jiwe utakuja kuiona huko mbele ukishamaliza shule na umepata kazi so SERA YA UCHANGIAJI KATIKA ELIMU NA AFYA NI LAZIMA na tena nashangaa kwa nini tunakomalia elimu tu na tusikomalie afya iwe free....
Ni hayo tu waungwana si vyema tukaegamia upande mmoja tu kila wakati, madogo wanachemka na ni lazima kaka zao hapa JF tuwaelekeze maana nasi tulipita hapo
Date::1/14/2009
Daruso yafutwa, sheria mpya UDSM zatangazwa
Latifa Karugila na Hussein Kauli
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeweka masharti magumu ya kudhibiti usajili wa wanafunzi waliodahiliwa upya kuingia chuoni hapo kuanzia Januari 19, mwaka huu.
Vile vile, kimetangaza rasmi kufutwa kwa sheria za chuo zinazotambua kuwepo kwa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho (Daruso).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Makamu Mkuu wa chuo (Taaluma), Profesa Makenya Maboko, ilionyesha kuwa wanafunzi wote watakaotimiza vigezo vya kujiunga tena na chuo, watapewa vitambulisho vipya pamoja na taratibu za namna ya kuishi chuoni hapo.
Profesa Maboko alieleza kwenye taarifa hiyo kuwa, mwanafunzi atakayekutwa ndani ya chuo bila ya kuvaa kitambulisho atakuwa amesababisha uvunjifu wa amani na utulivu, hivyo atachukuliwa hatua za kisheria juu ya kitendo hicho.
"Wanafunzi watakaokuwa wamevaa vitambulisho hivyo ndio watakaoruhusiwa kuingia darasani," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Ili kutekeleza masharti hayo, Profesa Maboko alisisitiza kuwa kila mwanafunzi atakayekamilisha taratibu za usajili atapaswa kupatiwa kitambulisho kipya, vinginevyo hatatambuliwa kama mwanafunzi aliyetimiza vigezo vya kujiunga tena na chuo.
Akizungumzia kuhusu Serikali ya Wanafunzi wa UDSM (Daruso), Profesa Maboko alisema taasisi zote za wanafunzi zilizokuwa zikitambuliwa na sheria ya chuo ya mwaka 2007, kabla ya kusimamishwa kwao, hazitatambuliwa tena.
Alisema taasisi hizo zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho.
"Taasisi mpya za wanafunzi zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho," aliongeza Profesa Maboko.
Wanafunzi waliosajiliwa upya watatakiwa kuripoti chuoni hapo kuanzia Januari 19 hadi 22, mwaka huu, kwa utaratibu maalumu uliotolewa na chuo.
Source: Mwananchi 15/01/2009
Uongozi wa UDSM ulichelewa kuifuta hii DARUSO, to me DARUSO haikuwa ikikidhi mahitaji na matakwa ya wanachuo zaidi ya kuwa jukwaa la kuendesha siasa na kuwanyima haki wale ambayo wapo kwa nia ya kusoma. Ifike mahali wanafunzi waelewe kuwa kazi yao hapo UDSM ni kusoma na wale siyo kuendesha Chuo. Kazi za kuendesha Chuo ziachwe kwa Viongozi wa Chuo vinginevyo wanafunzi wanachukua muda mwingi kufanya yale ambayo haya wahusu kimsingi.
Bravo kwa kuifuta DARUSO
Nini kifanyike; kwa nini serikali isiwashirikishe kuchangia hawa wanafunzi kwa njia ya mikopo na wahakikishe hiyo mikopo inarudi as soon as they are employed after their education? Tuachane na mikopo waliyokuwa wanatoa mwanzo maana na yenyewe walikuwa wanapeana tu, na sidhani kama hela zote huwa zinarudi; na kama zote zilikuwa zinarudi kwa nini zisizungushwe kwa wanafunzi hawa wanaoandamana kila siku?
Kama wanataka wanafunzi wachangie basi wawapunguzie masaa ya darasani na wa create part-time jobs for the students so they afford it!Period!
Kosa lingine ni letu wazazi. Vijana wanagoma wakiangalia uwezo wa sisi wazazi wao. Sisi tunakaa kimya kana kwamba hayatuhusu. Tunawasaliti vijana na kwa kufanya hivyo tunajisaliti wenyewe. Tunapaswa kupaza sauti zetu na kumuuliza JK, mbona watoto wa maskini wanakosa elimu wakati ulisema haitatokea hivyo?
Tujiulize pia, hivi watoto wote wanaotaka mkopo wakipewa asilimia 100 kuna shida yoyote? La msingi ni kuwabana walipe, period. Ni kama nataka kulima, naenda benki kukopa, benki inanipa hela za kulimia tu na inasema za kuipanda na kupalilia nijitegemee wakati sina uwezo huo. Je nikilima tu huo mkopo utarudi? Si bora wanikoppeshe hadi gharama za kuvuna na kuuza ili hayo mauzo ndiyo nilipe mkopo?. Serikali tumia akili.
Tatizo linakuwa gumu kwani JK, mkuu wa nchi alitoa msimamo wake mapema sana juu ya suala la sera ya uchangiaji kuwa haitabadilishwa. Ni kosa kubwa kwa rais kutoa misimamo kama hiyo kwani wewe ndiye mkuu kabisa, Sasa tuone kama hatakula matapishi yake.
Akisema sera ibaki hivyohivyo - kala matapishi yake maana watoto wa maskini hawatasoma. akisema ibadilishwe - kala matapishi yake maana alishasema haitabadilishwa. KAZI KWELIKWELI.