Nadhani haupo sahihi. Mleta mada sidhani kama lengo lake ni kumcontrol mwanamke au mwanaume bali ni kukemea hali ya uharibifu inayotokea.
Kimsingi, kinachotokea ni matokeo ya matumizi mabaya ya uhuru. Shida moja usiyoijua kuhusu jamii ni kuwa mwanamke asipokuwa makini na maamuzi yake na matendo yake basi jamii nzima itabeba mzigo wa matendo yake.
Sehemu kubwa ya changamoto za kijamii kama uhalifu, kukosekana kwa maadili, lishe mbovu, umasikini, etc ni matokeo ya moja kwa moja yanayohusishwa na mwanamke kutosimamia majukumu yake rasmi.
Nikuulize wewe binafsi, uwe haujaoa je upo tayari kuoa binti ambaye ametoka chuoni akiwa na msururu wa wanaume aliofanya nao mahusiano yaani mfano wanaume 9?! Na amekuweka wazi?!
Au utaweza kuwa na mapenzi ya kujenga familia na mwanamke ambaye ameshatoa mimba zaidi ya 5 na amekujulisha?!
Kimsingi, mwanamke anatakiwa kutazama matendo yake na mwenendo maaan ndipo utu wake ulipojificha. Akilega huko basi anavua utu wake na kuidhoofu jamii yake.
Ukitazama mwenendo wa jamii ya sasa na miaka ya nyuma ni sawa?!
Sio kweli kuwa mwanamke ameanza kushirikishwa katika maswala ya kimaendeleo miaka hii. Bali mwanamke wa kisasa anachukia shughuli na majukumu ya kike anatamani ya kiume ili asifanye ya kike.
Miaka ya nyuma wanawake wakiwa busy na majukumu yao ndio Dunia ilikuwa ikipata maendeleo haya tuliyoyafikia. Ila sasa muingiliano huu umeanza kurudisha nyuma maendeleo sababu interest ya mwanamke katika shughuli za kiuchumi ni kutaka kuonekana sawa na mwanaume, kupata pesa kwajiri ya kuvimbiana na mwanaume na kuwa above wanawake wenzake, na muhimu zaidi kutokuwa mwanamke sababu wanaamini kuwa mwanamke ni udhaifu na kuwa mwanaume ni privilege.
Wazia Dunia ya leo wanaume tukae benchi , wanawake washike usukani shughuli zote, mwezi hawatamaliza watasema tunataka kurudi majumbani tukawe wake.
Kama hatukubaliani uharibifu ni nini, utasemaje mleta mada anakemea uharibifu?
Unaandika kama tunakubaliana uharibifu ni nini.
Hizi ideas za uharibifu nyingi zinatokana na dini na collective societal norms, ambazo sasa hivi zinakuwa challenged.
Watu wanataka kuishi kwa uhuru wao zaidi.
Wewe iunanitolea mfano kuhusu mwanamke ninayetaka kuoa, mpaka hapo usha assume kwamba kila mtu anataka kuoa au kuolewa, mpaka hapo tu ushafanya a lazy assumption.
Na habari nzima ya "majukumu ya wanawake" ni ujima na mfumodume tu. Wewe sasa hivi una rais mwanamke, hizi traditional roles zinakuwa challenged.You guys are living in the past.
Why does this have to be wanaume kukaa benchi na wanawake kushika usukani? Kwa nini isiwe watu wenye akili kushika usukani na wasio na akili kukaa benchi, bila kujali wanawake au wanaume?
Paragraph yako ya mwisho inaonesha umejaa woga wa wanawake kukutawala, na unajaribu kuwa control, kuwa gaslight, kuwasengenya, wajione hawafai. Unaogopa wanawake wanasoma zaidi, wanajiweza zaidi, unaogopa wewe utakuwa irrelevant katika dunia ambayo wanawake watakuwa na sauti zaidi.
Hii ni alama ya mwanamme asiyejiamini.
Mwanamme anayejiamini atapenda wanawake wafanikiwe, waelimike, wapige hatua, atataka hivyo kwa kuwa anaheshimu utu wao na anataka kuwa na wanawake wenye elimu na uwezo.
Sasa kama hata hatukubaliani uharibifu ni nini, mtu kajiamulia kujiishia anavyotaka, hakulazimishi kitu, hapo kuna uharibifu gani?
Wewe huoni kumuingilia mtu mzima wa chuo kwenye maisha yake ndiyo uharibifu wenyewe hapa?