SI KWELI Chupa za Chai zina vidonge vyenye Sumu ambayo ni hatari kwa Afya

SI KWELI Chupa za Chai zina vidonge vyenye Sumu ambayo ni hatari kwa Afya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu hasa wale Wataalamu Wa Chemical na Hata Physics Kwa Ujumla nataka kupata Ufafanuzi hapa Kidogo!

Chupa zetu za Kuhifadhi Joto La Vinywaji au Vimiminika Kama Chai, Kahawa au Maji Moto Ndani Imegundulika Kuna Vidonge!! Naam Ni vidonge!

Video hii inasambaa Mtandaoni Kuhusu Hili Jambo!! TFDA na TBS Lipi Neno Lenu hapa?

Nawasilisha

FF6C0E10-51BB-4AA9-BD95-07CFEF57C853.jpeg
 
Tunachokijua
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango nchini (TBS), zimetoa ufafanuzi kuhusu vidonge vinavyodaiwa kuwapo kwenye chupa ya chai ambavyo vinadaiwa kuwa na madhara kwamba si sumu na havina madhara kama inavyodaiwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hizo, vidonge hivyo si sumu bali ni vitu vilivyotengenezwa kwa kutumia karatasi ambavyo ni teknolojia ya kisasa inayotumika kutenganisha kuta mbili za chupa ili kutunza joto la kimiminika kilichowekwa kwenye chupa husika.

Hivi karibuni kumekuwepo na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vidonge vilivyomo kwenye baadhi ya chupa za chai kuwa vidonge vyenye dawa yenye madhara kwa watumiaji na video nyingine ya lugha ya kiarabu ikieleza vidonge hivyo vina madini ya asbestos.

“Tunawahakikishia wananchi kuwa bidhaa hizo ni salama kwa matumizi ya kutunza joto la kimiminika kama vile chai,”
imesema taarifa hiyo.

images

Taarifa ya TBS na TMDA
Pamoja na mambo mengine, taasisi hizo zimeonya wananchi kuepuka kusambaza taarifa kupitia mitandao ya kijamii zisizohakikiwa na taasisi hizo ili kuondoa taharuki zisizo za lazima.

Wasiwasi unaohusisha vifaa vinavyodaiwa “kuwa vidonge” uliwaji pia kuanzishwa hapa JamiiForums kwenye mjadala wenye kichwa cha habari “Hivi vidonge ndani ya chupa za chai nini kipo nyuma yake? TFDA, TBS zatoa ufafanuzimnamo Septemba 23, 2018.
Back
Top Bottom