KWELI Chura akiwekwa kwenye maziwa huzuia yasiharibike/kuganda

KWELI Chura akiwekwa kwenye maziwa huzuia yasiharibike/kuganda

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Nauliza kuna ukweli wowote kwamba wazee wa zamani waliweka chura kwenye maziwa kuyazuia yasigande?
Je kama ni kweli ni wazee wa makabila yapi?
Kama ni kweli chura ana properties gani kitaalamu ambazo humsababisha kufanya hivyo?

1744283143210.png
 
Tunachokijua
Vyura ni Amphibia wanaoanza maisha yao ndani ya maji na baada ya kupita metamofosi wanaendelea kuishi kwenye nchi kavu, isipokuwa vyura-kucha ambao huishi majini maisha yao yote.

Madai

Kumekuwepo na madai kuwa chura hai akiwekwa kwenye maziwa husaidia maziwa hayo yasigande. Madai hayo yanaendelea kueleza kuwa hapo zamani kabla ya uwepo wa majokofu (refrigerator) walikuwa wakitumia chura na kuwaweka kwenye vyombo vyenye maziwa ili kuyafanya maziwa hayo yakae kwa muda mrefu. Tazama hapa

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imepitia tafiti na machapisho mbalimbali na kubaini kuwa madai hayo ni ya kweli. Taarifa zinabainisha kuwa kabla ya uwepo wa majokofu watu walikuwa wakitumia chura kama njia ya kuhifadhi maziwa yasiharibike haswa wakati wa joto kali.

Mbinu hii ilitumiwa zaidi na mataifa ya Finland na Urusi kuhifadhi maziwa wakati wa joto kali. Miaka ya baadae ilikuja njia nyingine ya kuhifadhi maziwa ambayo ilikuwa ni kwa kutumia mabarafu yaliyokuwa yanafuatwa huko milimani kisha kuyafukia ardhini na kisha kuyafunika kwa maganda mengi ya mbao (sawdust) hadi msimu wa baridi tena, mbinu hii ilitumiwa zaidi na matajiri huko Roma na Ugiriki ya zamani.

Ingawa watu hao walitumia mbinu hiyo lakini hawakujua sababu haswa inayopelekea chura kufanya maziwa yasigande. Tafiti mbalimbali zilikuja kufanyika baadae na kubaini kuwa chura wanatoa kemikali mbalimbali amabazo zinapelekea kupambana na bakteria pamoja na fangasi hivyo kusadia maziwa yasigande wanapowekwa kwenye maziwa.

Tafiti zilizofanyika zimebainisha kuwa ute unaotolewa na baadhi ya chura kutoka kwenye ngozi zao una uwezo wa kuua na kuzuia bakteria pamoja na fangasi. Utafiti uliofanywa na mkemia kutoka Urusi mwaka 2012 anayejulikana kwa jina la Albert Lebedev pamoja na kundi lake walifanya utafiti kuhusu ute unaotelewa na chura aina ya ‘Russian Brown’ kupitia ngozi na kubaini kuwa chura wana aina 76 tofauti za Protini na amino acid ambazo huweza kutumika kwa ajili ya kupambana na bakteria.

Licha ya kuwa ni njia iliyokuwa ikitumika hapo awali lakini haishauriwi kuitumia kwa sababu kutokana na tafiti imebainisha uwepo aina tofauti za protini na amino acid ambazo bado haijajulikana kila moja ina kazi gani hivyo inawezekana wakati mwingine huenda ikazalisha sumu kwenye chakula.
Nauliza kuna ukweli wowote kwamba wazee wa zamani waliweka chura kwenye maziwa kuyazuia yasigande?
Je kama ni kweli ni wazee wa makabila yapi?
Kama ni kweli chura ana properties gani kitaalamu ambazo humsababisha kufanya hivyo?

View attachment 3299040
Ujanja ni kuwa chura anarularuka ndani ya maziwa na mwili wake huwa baridi hivyo huyachanganya maziwa yasitulie na kuganda.
 
Halafu hayo maziwa yanakuja tena kutumiwa na binadamu ? Dah
 
Back
Top Bottom