CIA inamtesa Putin vikali, yaanza maandalizi ya kumtoa rasmi Kremlin

Alafu nyuklia unaiacha wapi?!
Tatizo mnafikiri nuclear ndio ufumbuzi wa kila kitu. Ata leo vita ya nuclear ikitokea ni lazima mshindi atapatikana na maisha yataendelea haijalishi madhara kiasi gani yatakuwa yametokea.

Dunia ilishapigwa na gharika ya Nuhu na ikaangamiza kila kitu isipokuwa wateule wachache waliokuwa ndani ya safina.

Hii Dunia aliyeiumba ni Mungu na atakayeiangamiza ni yeye peke yake na wala sio Mmarekani au Mrusi na hayo mabomu yao.

Hayo mabomu ya nuclear ni hatari ila Dunia ni hatari na kubwa kuliko hao.

Mrusi arubaini yake ikifika mbona atachapika tu na apo ndipo utajua cha kujivunia hapa Dunia sio hayo michuma chuma ila Mungu pekee
 
Hiki ndicho unachoweza kusema, Marekani sasa yaanzisha propaganda za kwamba Putin ana mpango wa vita ya muda mrefu ili waendelee kupeleka misaada ya kivita na kifedha, lengo likiwa ni kuyakomboa maeneo yote ya Ukraine yaliyotekwa na Urusi na hatimaye kuingia Moscow moja kwa moja na kumfurusha Putin Kremlin kadri siku zinavyoenda.

Hii inaonyesha kwamba mipango ya Wamagharibi imekwiva na kuhakikiwa vizuri.
_________________________________________

Putin anajiandaa kwa vita vya muda mrefu- Marekani

Vladmir Putin anajiandaa kwa vita vya muda mrefu nchini Ukraine, huku hata ushindi katika eneo la mashariki hautamaliza mzozo huo, idara ya kijasusi ya Marekani imeonya.

Onyo hilo linakuja huku mapigano makali yakiendelea katika eneo la mashariki, ambako Urusi inajaribu kuchukua eneo.

Moscow ilielekeza nguvu mpya kwa wanajeshi wake kuteka eneo la Donbas baada ya Ukraine kukataa majaribio ya kuchukua mji mkuu wake wa Kyiv.

Lakini licha ya hayo, vikosi vyake vimesalia katika mkwamo, taarifa za kijasusi za Marekani zilisema.

Avril Haines, mkurugenzi wa ujasusi wa kitaifa, aliiambia kamati ya Seneti ya Marekani iliyosikiza Jumanne kwamba Bw Putin bado ana nia ya "kufikia malengo zaidi ya Donbas", lakini kwamba "anakabiliwa na kutofautiana kati ya matarajio yake na uwezo wa sasa wa kijeshi wa kawaida wa Urusi".

Aliongeza kuwa rais wa Urusi "pengine" alikuwa akitegemea msaada wa Marekani na EU kwa Ukraine kudhoofika huku mfumuko wa bei, uhaba wa chakula na bei ya nishati ikizidi kuwa mbaya.

Hata hivyo, rais wa Urusi anaweza kugeukia "njia kali zaidi" huku vita vikiendelea - ingawa Moscow ingetumia tu silaha za nyuklia ikiwa Bw Putin ataona "tishio lililopo" kwa Urusi.

Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Ulinzi Scott Berrier aliambia kikao hicho kwamba Warusi na Waukraine walikuwa "katika mkwamo kidogo".

Katika mapigano ya hivi punde zaidi, Ukraine inadai kutwaa tena makazi manne katika eneo la kaskazini-mashariki la Kharkiv.

Cherkasy Tyshky, Ruski Tyshky, Rubizhne na Bayrak wote yalinyakuliwa kutoka kwa Urusi, vikosi vya silaha vya Ukraine vilisema.

Rais Volodymyr Zelenskiy alisema mafanikio ya Ukraine yanasukuma hatua kwa hatua vikosi vya Urusi kutoka Kharkiv, ambayo imekuwa ikishambuliwa tangu vita hivyo.

Lakini alisema Waukraine "hawapaswi kuunda mazingira ya shinikizo nyingi za maadili, ambapo ushindi unatarajiwa kila wiki na hata kila siku".

Contents na kichwa Cha habari ni tofauti....pole
 
Naona mnaichukulia Russia kimchezo mchezo. Msifikili kabisa Russian hana hizo silaha kali kama hizo mnazojaribu kumpa Ukraine na tena za Russian zinaweza zikawa kali na za maangamizi makubwa zaidi. Jinsi USA inavyompushi mrusi, hii vita inaweza ikaja kuwa ya kihistoria.
Marekani ina chuki kubwa sana na Russia na anatumia nguvu nyingi sana kuieneza lakini hatafanikiwa. Anaona Russia ndio taifa pekee linalomchelewesha kuitawala dunia atakavyo
unahisi kutawala dunia kitu kidogo ?
 
Na ndicho kitakachotokea, Ukraine itakua Russia's Vietnam. Mwishowe sitashangaa Urusi akiamua kuondoa majeshi yake kimyakimya au atumie tactical nuclear weapons kumaliza mzozo kuondoa fedheha. Kumbuka mpaka sasa wamagharibi wanatenga kabisa fedha kuendesha hiyo Vita ili ipiganwe hata miaka ili uchumi wa Urusi uanguke
shida ni kwamba uanyezungumzia anategemewa kwa asilimia nying sama ku stabilize uchum wa dunia had ngano za kulia chapat na supu pale Ngamu,hydom,nduguti na dongobesh jamaa anazalisha.
shida ili umuue mtu ni kuacha kununua anachouza sasa ikiwa stillna finance nyie nyie bas utabir wako huu navouona kama kweli kutaenda kutokea shift katika geopolitics za dunia kwa kiwango cha kutisha,kutazuka blackmarket zitazopiga hela ndefu sana naabilionea weng sion faid kwa west kurefusha labda watengenzea ges yao na walime wenyewe ngano yao madin mengine waache kuvaa vito wavae saa za mikanda ya chuma
 
Wewe ni wale watu wanajuwa sana kuandika na kupangilia maneno ya maandishi yenu ila pumba grade one. Sources
Acha kushusha watu kazi zao kama wewe hufuwatilii maswala ya kisiasa ni wewe ila jana kwepi Al-Jazeera walimuonyesha huyo mama na alisema hiki amendika unabisha google hilo jina youtube upate taarifa
 
Lakini pia Urusi inachukua maeneo muhimu kila kukicha. Inamalizia kuchukua Odesa. Imeshachukua mariupol. Sio kila landmass ni muhimu katika nchi. Russia wameshaifungua Ukraine isipakane na bahari.
Wameshachukua maeneo muhimu wa uchimbaji wa chuma, makaa ya mawe na metali zingine. Wamechukua pia maeneo yenye reserves za natural gas pale Crimea na pwani yote iliyopakana na Donbas.
Sasa nani anafaidika? Anayepanda vipande vya ardhi vyenye rasilimali au anayetuma silaha bila kufaidika chochote?
Urusi wameanza kusambaza ruble katika maeneo ya Mariupol, Kherson, Zaporishia, Melitopol na Donbas.
Wameshafungua balozi za LPR na DPR mjini Moscow na mabalozi wameteuliwa.
Nini maana ya gains kiutawala, kiuchumi na kimkakati kama sio hizo?
Hayo yote yanarudishwa Ukraine muda si mrefu, ukusikia may 9 bwana Putin alivyolialia kuwa wanataka kumvamia
 
shida ni kwamba uanyezungumzia anategemewa kwa asilimia nying sama ku stabilize uchum wa dunia had ngano za kulia chapat na supu pale Ngamu,hydom,nduguti na dongobesh jamaa anazalisha.
shida ili umuue mtu ni kuacha kununua anachouza sasa ikiwa stillna finance nyie nyie bas utabir wako huu navouona kama kweli kutaenda kutokea shift katika geopolitics za dunia kwa kiwango cha kutisha,kutazuka blackmarket zitazopiga hela ndefu sana naabilionea weng sion faid kwa west kurefusha labda watengenzea ges yao na walime wenyewe ngano yao madin mengine waache kuvaa vito wavae saa za mikanda ya chuma
Zitatafutwa njia mbadala
 
Hizo ni Propaganda za US! US anachofanya ni kujenga hofu na vitisho ili aendelee kupeleka silaha zilizokwisha kazi ili zikatupwe Ukraine.
 
Siyo kutupwa tu bali zinaenda kufagia kabisa jeshi la Urusi, ikipendeza zaidi ni kufagia had Kremlin
 
Kichwa cha habari na Yale yaliyomo... Ni tofauti kabisa.
 
Lakini pia Urusi inachukua maeneo muhimu kila kukicha. Inamalizia kuchukua Odesa. Imeshachukua mariupol. Sio kila landmass ni muhimu katika nchi. Russia wameshaifungua Ukraine isipakane na bahari.
Wameshachukua maeneo muhimu wa uchimbaji wa chuma, makaa ya mawe na metali zingine. Wamechukua pia maeneo yenye reserves za natural gas pale Crimea na pwani yote iliyopakana na Donbas.
Sasa nani anafaidika? Anayepanda vipande vya ardhi vyenye rasilimali au anayetuma silaha bila kufaidika chochote?
Urusi wameanza kusambaza ruble katika maeneo ya Mariupol, Kherson, Zaporishia, Melitopol na Donbas.
Wameshafungua balozi za LPR na DPR mjini Moscow na mabalozi wameteuliwa.
Nini maana ya gains kiutawala, kiuchumi na kimkakati kama sio hizo?
Hiya Mauripol pi?
 
Tatizo mnafikiri nuclear ndio ufumbuzi wa kila kitu. Ata leo vita ya nuclear ikitokea ni lazima mshindi atapatikana na maisha yataendelea haijalishi madhara kiasi gani yatakuwa yametokea.

Dunia ilishapigwa na gharika ya Nuhu na ikaangamiza kila kitu isipokuwa wateule wachache waliokuwa ndani ya safina.

Hii Dunia aliyeiumba ni Mungu na atakayeiangamiza ni yeye peke yake na wala sio Mmarekani au Mrusi na hayo mabomu yao.

Hayo mabomu ya nuclear ni hatari ila Dunia ni hatari na kubwa kuliko hao.

Mrusi arubaini yake ikifika mbona atachapika tu na apo ndipo utajua cha kujivunia hapa Dunia sio hayo michuma chuma ila Mungu pekee
Excellent!

Ungeandika haya maandishi kwa herufi kubwa.
 
shida ni kwamba uanyezungumzia anategemewa kwa asilimia nying sama ku stabilize uchum wa dunia had ngano za kulia chapat na supu pale Ngamu,hydom,nduguti na dongobesh jamaa anazalisha.
shida ili umuue mtu ni kuacha kununua anachouza sasa ikiwa stillna finance nyie nyie bas utabir wako huu navouona kama kweli kutaenda kutokea shift katika geopolitics za dunia kwa kiwango cha kutisha,kutazuka blackmarket zitazopiga hela ndefu sana naabilionea weng sion faid kwa west kurefusha labda watengenzea ges yao na walime wenyewe ngano yao madin mengine waache kuvaa vito wavae saa za mikanda ya chuma
Unamuona west wa kawaida mbele ya Russia? Unaijua west vizuri?
 
Back
Top Bottom