City Garden (Mbeya) hawajui kuchoma nyama!

Siku nyingine naenda hapo SAE.
Pana dada mmoja asubuhi anapika supu ya kuku hapo Mwanjelwa Stand ya Tukuyu zamani karibu na duka la Nafuu Phone mgongo wa kuku wa kienyeji na mayai yake ndani buku tano au sita pamoja na shingo hizo pande zina lishe nzuri ni mpaka uambiwe machimbo yake...nyama choma nenda Soweto pale ukimuuliza mtu yeyote anakuonyesha jina nimesahau...
 
Mbeya wewe kula kitimoto tuu ndo wanajua kuichoma na kupika. Nyqmq zingine kula huko mikoa mingine.
 
Pole sana. City Garden ya Dar es Salaam wanajitahidi sana...
 
Nimetoka mishe mishe zangu huko baada ya safari nikaulizia wapi naweza kupata nyama/kuku choma wapambe wakaniambia wahi City Garden, iliyopo sehemu zamani maarufu kama Mafiati.

Pamoja na kabaridi nikaagiza bia baridi na kabla hata sijamaliza glasi moja, sahani ya kuku hiyoo. Kuingiza jino tu, wallahi ikawa kama manati. Vuta, vuta na wewe!

Kuku hana vingo, no marination, generally ni kama amebabuliwa tu na moto.

Nikamwita mhudumu aniitie chef. Chef akakataa kuja, ati yuko busy, kubabua kuku wengine.

Nikamshukuru mhudumu ni nikampa angalizo kuwa kuenda hapo kwa nyama/kuku choma ni mara ya mwisho na awafikishie ujumbe uongozi.
Nikaondoka.
Tukio hili ni jana tu.

Mteja ukitaka kula nyama mbichi wahi City Garden Mbeya.

Pole kwa changamoto ulipaswa kuagiza maparachichi mkuu
 
Pana dada mmoja asubuhi anapika supu ya kuku hapo Mwanjelwa Stand ya Tukuyu zamani karibu na duka la Nafuu Phone mgongo wa kuku wa kienyeji na mayai yake ndani buku tano au sita pamoja na shingo hizo pande zina lishe nzuri ni mpaka uambiwe machimbo yake...nyama choma nenda Soweto pale ukimuuliza mtu yeyote anakuonyesha jina nimesahau...
Pia kuna mmoja yupo Soweto nae ni fundi kwa kweli japo pale SAE nao wanatisha kwa mikosi.
 
Nimetoka mishe mishe zangu huko baada ya safari nikaulizia wapi naweza kupata nyama/kuku choma wapambe wakaniambia wahi City Garden, iliyopo sehemu zamani maarufu kama Mafiati.

Pamoja na kabaridi nikaagiza bia baridi na kabla hata sijamaliza glasi moja, sahani ya kuku hiyoo. Kuingiza jino tu, wallahi ikawa kama manati. Vuta, vuta na wewe!

Kuku hana vingo, no marination, generally ni kama amebabuliwa tu na moto.

Nikamwita mhudumu aniitie chef. Chef akakataa kuja, ati yuko busy, kubabua kuku wengine.

Nikamshukuru mhudumu ni nikampa angalizo kuwa kuenda hapo kwa nyama/kuku choma ni mara ya mwisho na awafikishie ujumbe uongozi.
Nikaondoka.
Tukio hili ni jana tu.

Mteja ukitaka kula nyama mbichi wahi City Garden Mbeya.
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom