Hapa watu wa Yanga watasema Boban....Mimi sio Kolo wala utopolo
Haruna Moshi Boban ni bonge Moja la kipaji niliyewahi mshuhudia KWA umri wangu ndio mchezaji fundi zaidi wa kitanzania katika soka.....sema wabongo hawana jicho la mafanikio ndio maana wengi wanapotea haraka,KWA umasikini wa vipaji nchini Chama anaonekana ni Balaa....Kama mwanasoka Chama anajua mpira lakini ni mchezaji wa jukwaa ni kama wale kina Antony wa Man Utd...Wabongozozo wote tujiulize kama Chama ni wa hatari kiasi hicho kwa nini Berkane alichemka?
Au Timu yake ya Zambia haimbwi kama huku Msimbazi?
Tusiwape sana sifa wageni tukasahau vya kwetu...Chama hawezi kukupa Matokeo kwenye Game chafu mara nyingi anapotea....Huyu Ibrahim Ajib angejitambua angekuwa na rekodi nzuri kuliko Chama,angalia mechi ya Juzi na wale Vipers alipata Nafasi ya kuwakimbiza mabeki lakini akashindwa kufunga hana spidi na uwezo wake wa kufikiri ulikuwa hauna namna hadi huruma eti huyo ndiochezaji hatari Tanzania....ni aibu...bado tunasafari ndefu na ligi yetu bado changa haina Quality player na quality Team.