Clautos Chama Vs Haruna Moshi "Boban" nani fundi zaidi?

Clautos Chama Vs Haruna Moshi "Boban" nani fundi zaidi?

Hapa watu wa Yanga watasema Boban....Mimi sio Kolo wala utopolo
Haruna Moshi Boban ni bonge Moja la kipaji niliyewahi mshuhudia KWA umri wangu ndio mchezaji fundi zaidi wa kitanzania katika soka.....sema wabongo hawana jicho la mafanikio ndio maana wengi wanapotea haraka,KWA umasikini wa vipaji nchini Chama anaonekana ni Balaa....Kama mwanasoka Chama anajua mpira lakini ni mchezaji wa jukwaa ni kama wale kina Antony wa Man Utd...Wabongozozo wote tujiulize kama Chama ni wa hatari kiasi hicho kwa nini Berkane alichemka?
Au Timu yake ya Zambia haimbwi kama huku Msimbazi?
Tusiwape sana sifa wageni tukasahau vya kwetu...Chama hawezi kukupa Matokeo kwenye Game chafu mara nyingi anapotea....Huyu Ibrahim Ajib angejitambua angekuwa na rekodi nzuri kuliko Chama,angalia mechi ya Juzi na wale Vipers alipata Nafasi ya kuwakimbiza mabeki lakini akashindwa kufunga hana spidi na uwezo wake wa kufikiri ulikuwa hauna namna hadi huruma eti huyo ndiochezaji hatari Tanzania....ni aibu...bado tunasafari ndefu na ligi yetu bado changa haina Quality player na quality Team.
 
mimi ni mwanachama wa lunyasi na nimewaona wote wawili katika ubora wao..haruna alikua na kipaji kikubwa sana cha mpira katika peak yake kiukweli kwangu mimi ni moja ya mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha mpira macho yangu yamewahi kumshuhudia akicheza..sisemi chama hana kipaji la hasha ila nyakati tu zinawatofautisha ..nan anacheza na kina nan kwenye nyakati gani..na simba hii ya sasa sio simba ile ya 2004-2012 nyakati ambazo haruna alikua akicheza..ila jamni boban katika peak yake acha tu jamaa ana ujua sana.
 
nakumbuka nyakati zile 2007 nadhani.. tunajazana uwanja karume kuangalia mazoezi ya timu ya taifa ya marcio maximo kucheki mavitu ya boban,..k$$$mk acheni utani jmni yule kiumbe alikua bongo bahati mbaya sana.
 
nakumbuka nyakati zile 2007 nadhani.. tunajazana uwanja karume kuangalia mazoezi ya timu ya taifa ya marcio maximo kucheki mavitu ya boban,..k$$$mk acheni utani jmni yule kiumbe alikua bongo bahati mbaya sana.
Ukoo wote wa akina Moshi walikuwa na kipaji sana.
 
Hatuna Alikuwa anajua Mpira mno mno mno.

TATIZO Hasira, Bangi yule mtu anavuta jamani.
Ushirikina mwingi
Uswahili.
Nyakati.
 
Back
Top Bottom