Ndio maana AFrika maradhi na vifo kila siku vinaongezeka!! Hivi wewe raia wa kawaida ambae hujawahi kupeleka tangazo redioni hata siku moja halafu unaichukia Clouds, unazani unawapunguzia nini kama sio kujitia stress zisizo na msingi?! Najua kuna wengine watasema hiyo Clouds ipo juu kwa ajili ya wasikilizaji, but whether you like or not, Clouds inachukiwa na wana-JF pekee ambao wengi wao ni wale wanaotaka kuchanganya siasa na burudani!!! Pamoja na some JF members, wengine wanaoichukia Clouds ni wasanii waliochuja ambao kila wanapochuja lawama wanazipeleka kwa Clouds!! Kutokana na upuuzi wao, hawaamini kwamba watasikika hadi nyimbo zao zipigwe Clouds!!! Yaani wasanii wa kibongo wapo tayari nyimbo zao zisipigwe radio zote lakini zipigwe Clouds, na zisipopigwa huko, NONGWA!